
Mtunzi: Halfani Sudy
SEHEMU YA TATU
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
"Au unahamu…..?" Dokta Kilumba nae aliuliza swali lililoelea hewani, bila kutanabaisha Dokta Yusha alikuwa na hamu ya nini.
"Mbona siwaelewi ndugu zangu" Dokta Yusha aliongea kwa sauti ndogo iliyokuwa ikiashiria kutoelewa kinachoendelea.
"Naitwa Tamaa Karimu, unaitwa Yusuph Shaweji,
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
sina undugu na wewe na wala sijawahi kuwa na undugu Na wewe, labda hawa wenzangu ndio ndugu zako"
"Nani, mimi nitakuwa na ndugu kama huyo?" Dokta Sharifa alirukia kwa mtindo wa swali.
"Lazima niwe makini, kuna kitu kinaendelea" Dokta Yusha alijionya mwenyewe kimoyomoyo.
Wakati wanaongea na Dokta Yusha, lile kundi la wauaji walikuwa wamejipanga vizuri kule katika chumba cha kuhifadhia maiti. Tayari kwa kulinda usalama ili wale madaktari waje kufanya mchezo wao hatari. Mchezo wa kutoa mioyo ya maiti ! Pale walikuwa wanamchanganya tu Dokta Yusha ili kupoteza umakini wake, na kuwapa nafasi kundi la Six killers wajipange vizuri kule katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Na walifanikiwa !
Lile anguko la Mwanasheria lilimpeleka moja kwa moja kule kwenye kibonde kidogo lilipoingia gari la Mzee Mpaukha, na kujikuta ameulalia mwili wa mpambe wa Bi harusi,
"Mamaaaaaa"
Mwanasheria alipiga kelele kali sana. Akiwa amemlalia Hasina, macho yake mbele yake alikutana na picha mbaya sana. Picha ya kutisha.
"Ni nini hii, inamaana tumekufa wote" Mwanasheria alijiuliza mwenyewe. Pombe haziongopi kabisa, Mwanasheria alijiona kama na yeye alikuwemo katika ile gari iliyopata ajari, na sasa watu wote wamekufa, akiwemo na yeye. Yalikuwa mambo ya ajabu sana.
Alijiinua taratibu toka katika mwili uliojeruhiwa vibaya sana, mwili wa Hasina, akasimama wima, huku akiwa anayumbayumba, Mwanasheria aliangalia vizuri eneo lote lile la ajari. Japo kwa shida kutokana na giza na kwa macho ya ulevi, lakini alitambua vizuri madhara makubwa yaliyotokea mahali pale.
"Ni nini hii?" Alijiuliza mwenyewe Mwanasheria. Mara akili zake za kilevi zilimtuma kufanya kitu. Alitoa simu yake mkononi na kupiga simu, alipiga simu kwa Robert, alikuwa ni rafiki yake kipenz.
"Hallo Robert" Aliongea kwa sauti ya kilevi.
"Nambie Mwanasheria, mbona usiku sana" Robert aliongea kwa sauti iliyoonesha alikuwa anatoka usingizini.
"Tumepata ajari rafiki yangu"
"Ajari ?"
"Ndio wenzangu wote wamekufa nimebaki mimi peke yangu"
"Ulikuwa na kina nani"
"Siwajui"
Pombe zilimfanya Mwanasheria ajione kama naye alikuwemo katika ile ajari.
"Sehemu gani imetokea hiyo ajari?"
"Mtaroni"
"Come on Mwanasheria be serious"
"Kweli my friend"
"Ulikuwa unatoka wapi mwanasheria?"
"Kilabuni"
Robert alitoa msonyo mrefu na kukata simu. Akihisi Mwanasheria alikuwa katika maruweruwe yake baada ya kunywa pombe za kutosha.
Upande wa Mwanasheria, ulibaki na mshangao, kwanini rafiki yake kipenz Robert kamkatia simu wakati yeye anamueleza jambo muhimu na zito sana.
Mwanasheria alianza kupiga kelele, na maneno ajari na balaa yakisikika mara kwa mara katika kelele zake.
Majirani na lile eneo walisikia walisikia vizuri sana kilio kile cha Mwanasheria, lakini nani katika mji ule alikuwa hamjui Mwanasheria, nani angekithamini kilio cha mlevi yule, kila mtu alipuuzia kilio cha mlevi, Mwanasheria. Lakini Mwanasheria hakupuuza, alizidi kupiga kelele…
Kule hospitali Kivinje hali ya mviziano iliendelea. Baada ya Dokta Yusha kukaa pale kwa muda mrefu, bila simu yake kupigwa, bila kumuona aliyempigia simu, aliamua kuondoka. Huku kichwani alikuwa anawaza, atamwambia nini Nasra na kumuelewa, atawaambia nini wazazi wake. Alitoka nje na kumkuta dereva wa ile pikipiki amesinzia, alimuasha na kupanda.
Wakaondoka.
Wakati wanaondoka walipishana na gari moja lililoingia kwa kasi sana mle hospitali, almanusra liwagonge.
Walipofika Singino, simu ya Dokta Yusha iliita, kuangalia namba ni ya ile sauti ya kizee iliyompigia mwanzo…
Sasa, akawa anajishauri, apokee ama asipokee ile simu.
"Hebu simamisha pikipiki kidogo" Dokta Yusha alimwambia dereva wa pikipiki ile kwa sauti kubwa. Pikipiki ikasimamishwa.
Dr Yusha aliipokea simu ile na kuisikia sauti ileile ikimsisitiza aende Kivinje kumsaidia mgonjwa wake.
"Mbona nimetoka hapo hospitali muda huu?" Dokta Yusha aliuliza kwa sauti yenye kukereka.
"Tupo huku nyuma, karibu na jengo la kuhifadhia maiti"
"Sasa mbona nilipofika niliipiga hii simu ilikuwa haipatikani"
"Simu iliisha chaji, yaani hapa nimeilazimisha tu kuiwash…"
Simu ikakatika.
Dokta Yusha aliamini kweli, simu ya yule jamaa haikuwa na chaji, maana ndomana hata sasa ilizimika kutokana na tatizo hilo.
"Turudi hospitali" Alimuamuru yule dereva pikipiki. Yule kijana aligeuza pikipiki haraka, yeye alikuwa kazini, na aliamini ujira wake unaongezeka kila inavyoongezeka safari.
Kule Kivinje, Tano alikuwa hajafanikiwa Mpango wake, hadi Dokta Yusha anapanda pikipiki na kuondoka, hakuiona nafasi sahihi ya kumuua daktari yule kijana. Wakati Dokta Yusha anaondoka Tano alijishauri, amfate Dokta Yusha na kumuua njiani ama afanyaje. Mwishowe aliamua kumrudisha tena Dokta Yusha kwa kutumia ile simu. Na alifanikiwa, Dokta Yusha alikuwa njiani anarudi.
Tano alijificha nyuma ya jengo la kuhifadhia maiti la Hospitali ile, na kisu chake mkononi. Akisubiri kwa hamu ujio wa Dokta Yusha. Daktari wakiyeamini angekuwa kikwazo katika Mpango wao walioupanga usiku wa siku ile.
Muda mfupi baadae, Pikipiki aliyopanda Dokta Yusha iliwasiri pale Hospitali. Dokta Yusha alishuka kwenye ile pikipiki. Siyo kwa haraka sana kama mwanzo. Akawa anaelekea upande wa kushoto kilipo chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ile.
Dokta Yusha alikaribia kabisa kile chumba cha kuhifadhia maiti.
Ghafla, alisikia kelele kali sana zikitoka kule mapokezi.
"Uwiiiiiiii, jamani tusaidieni, tumeamua vibaya saaaaana, tusaidieni, madaktariiiiii, tunakufaaaa…." Zilikuwa kelele kali sana. Kelele ambazo zilisababisha Dokta Yusha abadiri uelekeo. Toka kwenye kifo kurudi katika uhai. Dokta Yusha alitimka mbio kurudi kule mapokezi, alikosikia makelele ya mtu akiomba msaada. Alipofika pale alimtambua vizuri sana mpiga kelele, alikuwa Mwanasheria, mlevi maarufu sana Kilwa Masoko. Taratibu alianza kupunguza mwendo akijua Mwanasheria yupo katika makelele yake ya kawaida ya pombe. Lakini kadri ya alivyokuwa anamsogelea Mwanasheria, umakini wake uliongezeka.
Mwanasheria alitapakaa damu mwili mzima, huku kundi dogo la watu likiwa limemzunguka. Dokta Yusha alijitahidi kupenya kundi la watu wale na kumfikia mlevi yule.
"Vipi Mwanasheria?" Baada ya kumkaribia Dokta Yusha lilimtoka swali.
Mwanasheria alimwangalia Dokta Yusha na kumtambua.
"Tumepata ajari Dokta, sote tumekufa" Mwanasheria alitoa kauli iliyomchekesha kila mtu.
"Come down Mwanasheria, wewe hujafa"
"Nimekufa Dokta, nimekufaaaaaa" Alisema kwa sauti kubwa sana.
Dokta Yusha aliona pale hawawezi kuelewana.
"Hao wenzako wako wapi?"
"Wapo humo Dokta" Mwanasheria alisema huku akionesha kwa kidole chumba kulichokuwa karibu na pale walipokaa.
Kwa mwendo wa taratibu Dokta Yusha alielekea kule chumbani. Alikutaba na balaa.
Mwili wa kwanza kuuona ni wa rafiki yake kipenzi, mke wake kipenzi, Nasra. Alienda mbele ya mwili ule uliolazwa vibaya sakafuni na kuuinamia. Dokta Yusha aliona ufa mkubwa sana katika kichwa cha mpenzi wake , pale alipojigonga na jiwe baada ya ile ajari ya kizembe kutokea. Aligusa upande wa kushoto wa kifua cha Nasra, mapigo ya moyo yalikuwa yanapiga kwa mbali sana. Akajua kosa lolote litasababisha ampoteze mke wake.
Alinyanyuka taratibu, huku chozi likimdondoka na kuufata mwili wa pili, alikuwa ni mkwewe, mama Mpaukha. Hakuhitaji kumgusa sehemu yeyote kutambua kama mkwewe kipenz alikuwa amefariki. Aliusogelea mwili wa tatu, mwili wa Alex. Dereva wa Mzee Mpaukha. Alimuona na damu nyingi sana, huku mabaki ya vioo yakiwa yamebaki katika mwili ule. Ilikuwa ni picha mbaya sana kuiangalia. Akausogelea mwili wa nne, wa Hasina, mpambe wa bibi harusi. Aliona mbonyeo mkubwa katika upande wa kulia wa kichwa kile. Pale alipojigonga na kioo Wakati Musa alipojaribu kukata kona ile kali. Mwisho aliusogelea mwili wa Mzee Mpaukha, mwili ambao haukuwa na tofauti sana na mwili wa dereva Musa. Nao mahali ya vioo yalikuwepo katika mwili ule.
"Balaa" Dokta Yusha alijisemea mwenyewe.
"Jamani tunakufaaa" sasa ndio alizisikia kelele za Mwanasheria kule mapokezi.
Dokta Yusha alitoka nje kumwangalia Mwanasheria alikuwa ameumia sehemu gani. Alimfikia Mwanasheria na kumkagua mwili mzima. Mwanasheria hakuwa na jeraha lolote zaidi ya zile damu zilizompakaa. Dokta Yusha akawaza labda Mwanasheria kaumia ndani kwa ndani. Wakati akimwangalia Mwanasheria ndipo alipomuona Fred kwa mbali, rafiki yake wa siku nyingi. Na ndiye alikuwa mpambe wake wa harusi siku ile.
"Vipi Fred"
"Ebana wameumia vibaya sana, afadhali nimekuona, nimewafata madaktari mpaka nyumbani kwao, hawapo, sijui wameenda wapi?"
"Kwani kilitokea nini Fred?" Dokta Yusha aliuliza kwa sauti yake yenye kwikwi.
"Mimi kanipigia simu huyo jamaa anayelia, muda mfupi tu nilipofika nyumbani kutoka kwenye sherehe, sijui hata namba yangu aliitoa wapi, yeye alikuwa analia tu, huku akisema wote wamekufa. Alinielekeza mahali ilipotokea ajari. Nilienda haraka kwa gari, na kukuta familia ya Nasra wamepata ajari mbaya sana ya gari aisee, majeruhi wako ndani huko" Fred alisema bila kujua kama Dokta Yusha kashaingia mle ndani na kujionea mwenyewe athari za ajari ile.
Kule nyuma ya chumba cha kuhifadhia maiti, Tano alikuwa anasubiri ujio wa Dokta Yusha. Alikuwa amejiandaa vema kumuua Dokta Yusha pindi atakapotokea tu. Alijibanza konani na kisu chake mkononi. Hakujua kabisa kuwa kwa wakati ule Dokta Yusha alikuwa amesahau kabisa habari ya simu ya mtu yule.
Tano alisubiri na kusubiri.
Alfajiri, mji wa Kilwa Masoko, waliamka na habari kuu mbili.
Habari ya kwanza ilikuwa ni kutokea kwa ajari katika kona inayoelekea mtaa wa Lumumba. Vijiwe vyote vinavyojadiri habari ngumu waliijadiri sana habari hiyo. Habari iliyohusisha ajari mbaya waliyoipata familia ya Mzee Mpaukha.
Habari ya pili ni kukimbia kwa bwana harusi katikati ya sherehe. Habari iliyopambwa na kusimuliwa vizuri sana na mafundi wa kusimulia. Tena wengine hawakuwepo hata katika ile sherehe yenyewe lakini ndio walikuwa wasimuliaji wakubwa. Vijiwe vyote vya waambea waliipa sana 'airtime ' habari hii ya bwana harusi kukimbia katikati ya sherehe kuliko habari ile ya ajari.
Kule Kilwa Kivinje majeruhi wote sasa walikuwa wodini. Dokta Yusha alifanya kazi kubwa sana usiku ule.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi