
Mtunzi: Halfani Sudy
SEHEMU YA KUMI NA TATU
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Inamaana yule mwanaharamu hajafika pale hospitali. Sasa wote mnaenda wodini kumchukua yule mzee na yule dada na mtaenda kule ICU kumchukua yule mfu. Leo ndio siku yao ya kufa!. Vifo vibaya sana, ambavyo havijawahi kushuhudiwa na Dunia hii. Hakikisheni hamfanyi kosa lolote vijana " "Sawa Bosi"
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
Six Killers waliitikia kwa pamoja. Wakaondoka. Safari ya kuelekea hospitali Kilwa Kivinje ilianza. Six killers wakiwa na hasira sana na Dokta Yusha. Mtu ambaye anataka kuwakosesha usingizi. Wakati wao wanaelekea Kilwa Kivinje hospitali, Dokta Yusha akiwa na Mwanasheria mlevi na wagonjwa wao walikuwa nd'o wanakipita kijiji cha Mandawa wakielekea mkoani Lindi. Nia yao ni kuwapeleka wagonjwa wao katika hospitali misheni ya ndanda, Mtwara. Six killers walienda moja kwa moja katika wodi waliolazwa Mzee Mpaukha na Hasina.
Waliingia kwa mbwembwe kubwa sana. Lengo ni kuwabeba wale wagonjwa na kwenda kuwaua vibaya sana, na kuwatoa moyo kule katika chumba cha kuhifadhia maiti. Walikuta wodi ipo tupu!. Hakukuwa na mgonjwa yeyote pale wodini. Moja alichukua simu yake na kumpigia Don Genge kumtaarifu habari hizo mbaya kabisa, habari ambazo ni chungu kutoka katika mdomo wa Moja, zilikuwa chungu kusikiwa na sikio la Don Genge. "Bosi hakuna mtu humu wodini" Moja alisema kwa fadhaha bila hata kumsalimia Bosi wake. "Unasemaje wewe!" Don Genge aliuliza kwa ghadhabu. "Hakuna mtu Bosi hapa wodini, jamaa itakuwa katuwahi" Moja aliongea kwa utulivu sasa.
"Huyo kijana aliyepewa kazi ya kulinda hapo yupo?" "Tunae hapa" "Afe yeye leo, na moyo wake utolewe, afe kifo sawa na tulichopanga kuwaua wale mbwa!" Don Genge aling'aka simuni. Yule kijana alianza kutetemeka. Muda uleule Six killers walimgeukia. Hawakuwa na mas'hara hata kidogo. Walimsukasuka kwa nguvu, safari kuelekea katika chumba cha kuhifadhia maiti ilianza. Walikuwa wanaenda kumuua yule kijana! Wahenga waliwahi sema, siku zote mshahara wa dhambi ni mauti. Kijana aliponzwa na Mwanasheria mlevi, mlevi anayetumia akili sana katika mambo yake, mlevi ambaye watu wengi walikuwa wanamdharau, bila kujua uwezo wake wa juu wa akili aliokuwa nao.
Kijana aliingia katika kesi asiyoijua mwanzo wala mwisho. Hakuwekea uzito maagizo aliyopewa na Dokta Zaidi Kilumba, hakujua kama kosa lolote la aina yoyote ile lingegharimu maisha yake. Hakupewa tahadhari hiyo na Dokta Kilumba, labda angepewa hiyo tahadhari angekuwa makini zaidi. Au labda angeikataa kabisa ile kazi ya kifo. Lakini ilikuwa bahati mbaya sana kwake, hakutahadharishwa awali pia hakupewa muda wa kujitetea, ili kuelezea kitu gani kilitokea, kwanza kundi la Six killers hawakuwa na muda huo, muda wa kumhoji yule kijana dhaifu, walikuwa na haraka isiyo na kifani. Ilikuwa lazima wamtafute Dokta Yusha, ilikuwa lazima wapate mioyo kumi na tano siku hiyo. Kumbuka walibaki wanne sasa, ukiondoa wale madaktari vibaraka na manesi wafata mkumbo.
Kumbuka Tano alikuwa mgonjwa, Sita alienda kusikojulikana. Walikuwa lazima wajigawe vizuri ili kufanikisha mipango yao..ilikuwa lazima wawepo wa kuhakikisha zoezi la utoaji moyo linaendelea kama kawaida, pia wawepo wa kuhakikisha zoezi ambalo lilikuwa gumu sana kwa sasa, zoezi la kumtafuta Dokta Yusha na wenzake linafanikiwa. Yule kijana asiyekuwa makini, na kuzidiwa akili na mlevi, aliuawa kwa kunyongwa shingo na Moja wa Six Killers, na kutolewa moyo kikatili na Dokta Sharifa Juma. Tatu na Nne walibaki pale hospitali, kulinda usalama wa pale, Moja na mbili ndio walienda kuwasaka wakina Dokta Yusha, kuwasaka mahala pasipojulikana. Ghafla, simu ya Don Genge iliita. Aliangalia katika kioo cha simu yake, kilisomeka..... Kifo! Don Genge alipokea ile simu huku akiwa na hofu kuu.
"Hallo Bosi" Don Genge aliita simuni kwa sauti yake yenye hofu. "Nipe maendeleo ya project yetu Don Genge" "Mambo yako sawa Boss, ingawa kuna kidudu mtu katuingilia kidogo katika mipango yetu" "Ni nani huyo Don Genge? na kaiingilia vipi hiyo project?" "Anaitwa Dokta Yusha, amegundua kila kitu tunachokifanya huyo jamaa ni mjanja sana aisee" "Na na bado anaendelea kupumua mpaka sasahivi?" "Ndio Bosi anapumua, ingawa naamini anamalizia pumzi zake za mwisho" "Six killers wanasemaji?" "Wanajaribu kupambana vijana, ila bado hali haijakaa sawa mpaka sasa, mmoja ni missing in action, na mmoja ni majeruhi" "Nani aliyepata majeruhi, na nani missing in action?" "Majeruhi Tano, missing in action Sita" "Lazima ufanye kitu Don, usiache hali ikawa namna hiyo, vipi kuhusu mzigo?" "Mzigo uko wa kutosha, tutausafirisha kesho asubuhi" "Fanya hivyo Don, mzigo umepungua sana huku, na tuna oda nyingi sana" "Nitafanya hivyo" "Sawa jamaa, huyo jamaa sijui Dokta nani anastahili kifo kabla hajatoa taarifa kwa jeshi la polisi au mahala popote ambako itakuwa si salama kwetu" "Nimekuelewa Bosi, nitahakikisha tunamziba mdomo" Simu ikakatwa.
Kifo, alikuwa ndio Mkurugenzi mkuu wa mradi huu kitaifa. Mradi wa kutoa mioyo ya maiti. Mioyo ambayo ilikuwa inatumika katika utengenezaji wa sumu hatari na kali zaidi duniani, Sumu ya Proxine! Sumu ambayo, ukiigusa bila ya kuwa na kizuizi chochote kinachofuata ni kifo! Kifo baada ya dakika thelathini tu. Sumu ambayo ilikuwa inatengenezwa nchini Ujerumani, lakini malighafi za kutengeneza sumu hiyo zilikuwa zinatoka Tanzania. Sumu ya Proxine, sumu hatari iliyopigwa marufuku kutumika dunia mzima lakini vikundi vya kigaidi vilikuwa vinaitumia kwa siri, na huipata kwa gharama kubwa sana. Hiyo ndio kazi ya mioyo hii ikiyochukuliwa na kundi la Six killers likiongozwa na jasusi wa najasusi Don Genge.
Unaweza ukasema utoaji wa mioyo wa maiti haukuwa na madhara sana kama asemavyo Don Genge, lakini je hivyo ndivyo wanavyopaswa kufanyiwa maiti, na je matumizi ya sumu ya Proxine, yalikuwa hayadhuru watu wasio na hatia? (Kumbuka riwaya ya Angamizo) Dokta Yusha na msafara wake uliingia katika hospitali ya misheni ya Ndanda, wote wakiwa hoi kwa uchovu wa safari. Moja kwa moja walienda kwenye hospitali hiyo kubwa ya misheni. Wagonjwa walichangamkiwa walipofika nje tu ya hospitali hiyo. Manesi wenye vitoroli waliwapokea haraka haraka na kuwapeleka wodini. Kwa umakini na kasi walipewa huduma zinazojitajika. Huduma zilizomridhisha sana Dokta Yusha. Alikuwa na furaha usoni, ingawa furaha yake ilisinyaa akikumbuka madhila ya watu wale wabaya aliowaacha huko Kilwa.
*****
Baada ya wiki moja, Mzee Mpaukha alikuwa mzima kabisa. Nasra na Hasina waliendelea kuwa wafu kitandani. Huku Hasina akifumba na kufumbua macho yake bila ya kuongea lolote. Akiba ya pesa aliyokuwa anaweka Dokta Yusha ilimsaidia sana katika kipindi kile kigumu kilichohitaji awe na pesa za kutosha. Huko Kilwa Masoko, kundi la Six killers lilikuwa katika hali ngumu sana. Wiki nzima walimsaka Dokta Yusha bila mafanikio yoyote. Six killers walianza kuingiwa na hofu labda Dokta Yusha amefichwa sehemu fulani baada ya kwenda kutoa taarifa Polisi na muda wowote watakuja kukamatwa na mipango yao kuwa hadharani, pamoja na kuwa na fikra hizo lakini hawakusumbuliwa kabisa na Polisi.
Hali iliyowaaminisha kwamba askari Polisi hawakuwa wanajua lolote. Six killers waliendelea kufanya kazi zao, lakini wakiwa na wasiwasi mkubwa sana. Dokta Yusha alikuwa ameichukua furaha yao na kwenda kuificha mahali kusikojulikana. Walijua ipo siku isiyokuwa na jina mambo yatakuwa mabaya sana kwao. Upande wa Tano wa kundi la Six killers hali yake iliendelea vizuri. Sasa alianza kufanya mazoezi madogo madogo ishara kwamba goti lake lilianza kupata nafuu. Aliendelea kutibiwa kwa siri kwenye ile nyumba yao iliyopo kule porini Ngome. Sita wa Six killers walimtafuta sana, lakini hawakuweza kupata, na wala hawakupata fununu wapi amekwenda. Hawakuwa na hisia kabisa kwamba kiti cha kifo ndiyo sababu ya kifo cha Sita.
Ukweli ni kwamba, kutoweka kwa Dokta Yusha kuliongeza hofu kwa kundi la Six killers. Sasa wakawa hawafanyi kazi kwa uhuru tena kama zamani. Iliwapasa kuhamisha mahala pa kufanyia operesheni zao zile za kikatili, sasa wakawa wanaiba maiti na kwenda kuzitoa moyo huko kambini kwao, kisha kuzitelekeza porini ngome. Kubadilisha mahali pa kufanyia mauaji kukazua jambo jipya katika hospitali ya wilaya ya Kilwa, kwa maana zilikuwa zinapotea maiti kumi na tano kila jua lilipokuwa linazama. Kupotea maiti kumi na tano kila siku ndiko kukazua jambo kuu. Tanzania nzima sasa ikapata habari juu ya upotevu huo wa maiti huko Kilwa. Wananchi wa Kilwa wakawa wanaishi kwa woga na wasiwasi mkubwa sana. Hakuna aliyekuwa anajua maiti za wapendwa wao zinapotea vipi.
Wananchi wenye imani dhaifu wakahusianisha matukio hayo na imani za kishirikina. Wananchi wa Kilwa walijaribu kila njia kuzuia wizi wa maiti lakini hawakufanikiwa. Upotevu huo wa maiti ukawasogeza karibu wapelelezi mbalimbali nchini Tanzania na waandishi wengi kwenda Kilwa kufatilia sakata hilo. Kazi ilikuwa ngumu sana kwa wapelelezi hao, hii kazi ya kuiba maiti ilifanywa na watu makini, tena wakishirikiana na madaktari makini pia. Wapelelezi walipeleleza kwa siri sana lakini hawakupiga hatua yoyote. Laiti wangejua wapelelezi hao wangemtafuta Dokta Yusha ama Mwanasheria mlevi, hao ndio walikuwa wanajua kila kitu juu ya sakata hili.
Laiti wangejua wapelelezi hao wangemtafuta Dokta Yusha ama Mwanasheria mlevi, hao ndio walikuwa wanajua kila kitu juu ya sakata hili. Mmoja wa waandishi wa habari aliyekuja kuchunguza sakata hii alikuwa anaitwa Gabriel Rondo. Mwandishi wa habari mahiri toka gazeti la Chokochoko. Gabriel Rondo alikuwa Mwandishi wa habari mdadisi sana, mara nyingi akifatilia jambo hufatilia kwa undani kabisa, na huja na habari yenye kumridhisha kila msomaji wa gazeti la Chokochoko. Asubuhi moja Mwandishi wa habari Gabriel Rondo ilimkuta akiwa mlangoni kwa Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya Kilwa.
Nia na madhumuni ni kwenda kupata maono ya Mganga huyo wa wilaya juu ya kupotea maiti maiti kumi na tano kila siku katika hospitali yake. Gabriel Rondo alifika katika ofisi ile mnamo saa mbili asubuhi, lakini mganga mkuu Dokta Zaidi Kilumba hakuwa amefika. Dokta Kilumba aliwasili ofisini kwake saa sita mchana, akiwa ananuka harufu mbaya ya pombe. Alifika ofisini kwake na kukuta msururu wa mkubwa watu ukimsubiri yeye, Dokta Zaidi Kilumba aliwapita watu wale kwa dharau kama hakukuwa na watu pale, Dokta Zaidi Kilumba hakuwajari, hakuwasalimia wala kuwaangalia usoni watu wale. Alijiinamia chini na kuingia ofisini kwake akiambatana na harufu yake ya pombe. Watu pale nje walianza minong'ono,
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi