BALAA (14)
Jina: BALAA Mtunzi: Halfani Sudy SEHEMU YA KUMI NA NNE ILIPOISHIA... Alifika ofisini kwake na kukuta msururu wa mkubwa watu ukimsubiri yeye, Dokta Zaidi Kilumba aliwapita watu wale kwa dharau kama hakukuwa na watu pale, Dokta Zaidi Kilumba hakuwajari, hakuwasalimia wala kuwaangalia usoni watu wale. Alijiinamia chini na kuingia ofisini kwake akiambatana na harufu yake ya pombe. Watu pale nje walianza minong'ono, JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... minong'ono iliyotoka katika midomo ya wasemaji na kutua moja kwa moja katika masikio yote mawili ya Mwandishi wa habari Gabriel Rondo . Baada ya Dokta Zaidi Kilumba kuingia ofisini kwake, wateja waliokuwa katika foleni pale nje walianza kuingia ofisini kwa Dokta Kilumba, kulingana na foleni yao. Watu waliingia ofisini mpaka zamu ya Mwandishi wa habari, Gabriel Rondo ilifika. "Naitwa Gabriel Rondo, Mwandishi wa habari wa gazeti la Chokochoko " Gab…