Machapisho

BALAA (17)

Zephiline F Ezekiel
Jina: BALAA
Mtunzi: Halfani Sudy

SEHEMU YA KUMI NA SABA
ILIPOISHIA...
Labda Tano alishikwa na ganzi katika mguu ulipewa jeraha na Dokta Yusha, maana hakusikia kabisa maumivu ya ule mguu wake mbovu. Akiwa amelala pale chini Daniel Mwaseba aliuona vizuri sana mguu ule. Ulivyokuwa unashushwa, kwa kasi ya haraka alinyoosha mikono yake yote miwili na kuudaka mguu ule mbovu,

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
Daniel Mwaseba aliuzungusha kwa nguvu zake zote. Mguu mbovu wa Tano uliteguka aisee! Tano alianguka chini akigalagala na kulia mithili ya mtoto mdogo. Alikuwa anasikia maumivu yasiyo na mfano. Daniel Mwaseba akiwa na ghadhabu aliruka juu na kushuka chini, aliukanyaga tena mguu mbovu wa Tano palepale kwenye kifuti. Tano alilia kilugha cha kwao.... "Six killers nd'o nini?" Tano alimwangalia Daniel Mwaseba kwa hasira sana. Alijitahidi kukusanya mate ya kutosha mdomoni, ingawa kwa shida lakini aliyapata. Aliyarusha mate yale yote yaliyokuwa yamechanganyika na damu! Yalitua katikati ya paji la Daniel Mwaseba.

Mate yenye mchanganyiko wa damu mbaya! Kitendo kile cha kijeuri kilizidi kumuuzi Daniel Mwaseba. Sasa alipandwa na hasira mithili ya kifaru. Hakujiangaisha kabisa kuyafuta yale mate yenye damu ya Tano. Alirudisha kichwa chake nyuma, kwa nguvu zake zote alikipigisha kichwa chake katika kichwa cha Tano. Kilikuwa kichwa kweli! Kichwa kilichomwacha Tano akipiga kelele mithili ya mtu aliyefiwa na baba yake mzazi. Kichwa kilichomwacha Daniel Mwaseba akiwa nae katapakaa damu usoni. Damu alizozitoa toka katika sura ya Tano. Ghafla! Mlango wa kile chumba ulifunguliwa kwa nguvu! Watu watatu kila mmoja akiwa na bunduki mkononi walikuwa wanawaoneshea midomo ya bunduki zao kwa Tano wa Six Killers na mpelelezi mahiri nchini Tanzania, Daniel Mwaseba! Kasheshe! "Naitwa Alfred Duto, afisa wa jeshi la polisi, mko chini ya ulinzi" Askari mmoja alitamka huku akiwa kashikilia kitambulisho chake cha kazi imara mkononi.

Daniel Mwaseba na Tano wote walinyoosha mikono juu. kila mmoja akiuchukulia ujio wa askari wale kwa namna tofauti, wakati mpelelezi Daniel akiupokea ujio wa askari wale kwa tabasamu. Kwa sababu ujio wa Polisi wale ulikuwa ni ushindi mkubwa sana kwake. Kwakuwa yeye alikuwa ni askari pia, hivyo walikuja askari wenzake. Lakini kwa Tano lilikuwa ni pigo kubwa sana, kuingia katika mikono ya polisi ni kitu alichokuwa hataki hata kufikiria. "Haya tokeni nje haraka!" Askari mmoja aliamrisha kwa sauti ya amri. "Naitwa Daniel Mwaseba" Askari wote watatu walistuka kusikia jina hilo. Daniel alishusha mkono mmoja na kutia mfukoni, alitoka na kitambulisho chake cha kazi. Sasa Polisi wakawa makini na yule jamaa mwengine.

Huku wakitoa midomo ya bunduki zao kwa Daniel. Kumbe purukushani zao na makelele wakati wanapigana zilisikiwa na Mhudumu kule nje. Mhudumu ambaye alimpigia simu Meneja wake kumueleza juu ya hofu yake na chumba namba saba, chumba alichofikia Daniel Mwaseba. Meneja nae aliamua kutoa taarifa polisi. Sasa walikuwa Askari wanne, wakitoka nje na Mhalifu. Kutoka katika hoteli ya kitalii ya Kimbilio, hoteli aliyofikia Daniel Mwaseba, haikuwa mbali kabisa na kituo cha polisi Masoko. Ilikuwa ni pua na mdomo. Walitumia miguu tu kumfikisha Tano kituoni. Walipofika kituoni Tano aliendelea na Kiburi chake. Hakueleza kitu chochote zaidi ya kusema yeye anaitwa Tano wa Six Killers. Alipewa mateso makali sana na askari Polisi.

Mateso ambayo hayakumfanya Tano atoboe siri zake ama siri za kundi la six Killers na mpango wao haramu. Tano aliendelea kuwa bubu. Alilala kituoni siku ile, huku Daniel Mwaseba akirudi mtaani kuendelea na upelelezi wa mauaji na kupotea kwa wanafunzi. Huku akiwa na msamiati mpya kichwani mwake ambao alishindwa kuutambua. 'Six killers' Kesho yake asubuhi Tano alipelekwa mahabusu, Gereza la wilaya ya Kilwa. Alipakiwa kwenye gari la polisi akiwa kafungwa pingu mkononi. Huku bunduki mbili zikitazama kichwa chake. Gari ilioondoka kwa kasi kubwa sana huku ikipiga ving'ora. Tano alizungusha macho yake huku na huko, kutafuta nafasi ya kutoroka, na ilikuwa hivyo. Tano wa Six killers akiwa hoehae aliiona nafasi akiyoitafuta.

Tano alijilegeza kidogo ikawa laini kama mlenda kisha akaanguka kwenye bodi ya gari. Askari wote walipatwa na mshangao mkuu, waliacha kumuelekezea ile midomo hatari ya bunduki, walimsogelea huku bunduki zao zikining'inia mabegani. Lilikuwa kosa la mwaka! Tano akiwa kajilegeza vilevile alijirusha nje ya ile gari na kushuka katika barabara ya lami. Tano alifikia vibaya sana katika barabara ya lami, kumbuka gari lilikuwa linatembea kwa kasi kubwa sana. Pia Tano alikuwa amefungwa pingu mikononi. Lakini Tano hakujari hilo hata chembe. Wale Askari walibaki midomo wazi, na bunduki zao mkononi zikiwa zinawashangaa.

Hawakuwa na ujanja wa kuruka kwa kasi ile, ilikuwa ni zaidi ya hatari. Askari walipigapiga bodi ya gari ile ili kumuamrisha dereva apunguze mwendo, maskini dereva hakusikia chochote, mwendo ule ukichanganya na kelele za king'ora, ilikuwa ni kama kumpigia mbuzi gitaa. Walimuacha Mhalifu hataru sana njiani, wao wakiendelea na kasi yao ya kutisha kuelekea gerezani! Tano, kwa sasa alikuwa ametapakaa damu mwili mzima, akiwa na maumivu kila sehemu ya mwili wake, maumivu ya kupewa kichapo na Daniel Mwaseba, maumivu ya kuruka katika barabara ya wakati gari ikiwa kasi, tena na kuangukia kwenye lami. Tano alikuwa na roho ya paka! Kwa kutambaa ingawa kwa shida sana alijisogeza pembeni ya barabara, alikuwa na maumivu makali sana, kiasi kwamba alikuwa anashindwa kunyanyuka.

Nasema ilimpasa ashindwe kunyanyuka lakini Tano wa Six Killers alijitahidi kunyanyuka, maana kuendelea kukaa mahala pale ilikuwa ni hatari sana kwake. Jamaa alijitahidi kunyanyuka, aliweza, Tano alinyanyuka kwa mwendo wa kusuasua alijisogeza pembeni zaidi ya barabara. Gari ya polisi ilikuwa inaingia katika viwanja vya gereza la Kilwa. Dereva alipiga kona kwa mbwembwe nyingi huku akifunga breki kali sana. Laiti angejua kama mhalifu Tano hakuwepo kule nyuma ya gari. Gari lilisimama. Taarifa mbaya kabisa ikapenya katika masikio ya dereva. Kwamba mhalifu Tano alijirusha toka katika ile gari wakati ikiwa katika mwendo mkali.

Ilikuwa ni kitendo bila kuchelewa hata sekunde kumi, dereva alirudi kwa haraka katika usukani wa gari ya Polisi na kuligeuza gari kwa haraka pia, kurudi pale mahali ambapo alijirusha Tano. Dakika nne na sekunde thelathini tu zilitosha kuwafikisha pale, askari walishuka haraka haraka kabla gari haijasimama vizuri na kuanza kumsaka Tano. Walichakua katika nyasi zote lakini Tano hakuonekana! Askari waliishiwa nguvu, kwa jinsi Tano alivyojirusha na kufikia na mwendokasi waliyotumia kurudi pale walitegemea kumkuta Tano palepale barabarani. Hayo yalikuwa mawazo yao, lakini Tano hakuwepo kabisa pale barabarani, hata dalili tu kama kulikuwa na kiumbe.

Hayo yalikuwa mawazo yao, lakini Tano hakuwepo kabisa pale barabarani, hata dalili tu kama kulikuwa na kiumbe. Huko porini Ngome hali ilikuwa ya taharuki sana. Tangu jana yake usiku Tano alikuwa hajarejea kambini. Waliamini Tano amepotea kama alivyopotea Sita. Sasa wanapotea vipi, wanaenda wapi, hakuna aliyekuwa na majibu. Walitafuta sehemu zote walikodhani labda atakuwepo lakini Tano hawakumpata. Mwishowe walienda mahali ambako Tano aliwaambia ataenda usiku, katika baa ya Tiga Tisa. Six killers wote wanne walienda katika baa ya Tiga Tisa. Walikaa meza moja na kuanza kuchunguza mazingira ya pale baa. Hawakupata lolote la maana. Mwishowe Moja aliamua kumuita Mhudumu mmoja ili amuulizie kama alimuona jamaa yao hapo.

Kwa bahati mbaya Mhudumu aliyemuita Moja nd'o yuleyule aliyeongea na Daniel Mwaseba kabla. Nd'o yuleyule aliyefanikisha Tano kukamatwa. Mhudumu muoga sana anapokutana na wanaume kama hawa. Haikuwa kazi ngumu kwa vijana mahiri wa six killers kutambua kwamba Mhudumu yule anayajua mengi. Wakaamua nae wamchukue. Kwa bahati mbaya kabisa Mhudumu wa baa ya Tigatisa akaingia katika mikono isiyo salama. Mikono hatari ya kundi baya na katili sana kuwahi kutokea katika historia ya Kilwa, kundi la Six Killers. Mhudumu nae akapelekwa porini bila kujua ukatili wa sehemu anakopolekwa na jamaa wale. Na majaa hao makatili sasa walikaa sebuleni na kuwaza na kujadiliana nini cha kufanya baada ya matokeo mabaya sana.

Kijana mbishi, kijana mkatili, kijana sugu kabisa Tano wa six killers alikuwa katika mikoko ya pwani ya makuburi. Alikuwa amejificha katika mikoko hiyo akiwaza namna salama ya kutoka katika mikoko na kurudi kambini kwao, porini ngome. Pamoja na uvumilivu wote huo lakini Tano alikuwa anapita katika maumivu makali sana. Alikuwa na vidonda mwili mzima, vidonda ambavyo sasa vilikuwa vinapitiwa na na ladha ya chumvichumvi toka katika mikoko ya pwani. Askari walirudi kituoni, kutoa taarifa kwamba Jambazi aliyejulikana kwa jina la Tano alikuwa amewarotoka. Kwa haraka sana habari hizo mbaya zikafikishwa kwa Daniel Mwaseba huku askari wakimwaga mtaani kama njugu kumsaka Tano wa six Killers. Daniel Mwaseba alipopigiwa simu, hakujibu kitu chochote kuhusu ile simu zaidi ya kuitikia tu tena kwa sauti ndogo sana.

Mpaka saa sita usiku inaingia ilimkuta Tano pale katika mikoko, muda huo giza lilikuwa la kutisha sana, usiku ukichanganya na uwepo wa mikoko iliyoshonana. Muda huo wa saa sita ndipo Tano alishuka juu ya mkoko na kuelekea porini Ngome kwa kupitia pori kwa pori. Hakujua, Tano hakujua! Nyuma yake hatua kama kumi na saba, kulikuwa na mtu makini anamfata. Mtu ambaye alilijua lile ficho lake muda mrefu sana. Mtu huyo hakutaka kumkamata. Shida yake ilikuwa ni kutaka kujua tu uelekeo wa Tano utakuwa wapi. Yeye alikuwa na shida ya kuyafahamu makazi ya yule jamaa, aliyejiita Tano. Na sasa ndio alikuwa anafanikiwa kuuona uelekeo wa Tano, na kwa umakini mkubwa alikuwa anamfuata Tano kwa nyuma, bila Tano kuhisi jambo lolote.

Kwa bahati mbaya kabisa Mhudumu wa baa ya Tigatisa akaingia katika mikono isiyo salama. Mikono hatari ya kundi baya na katili sana kuwahi kutokea katika historia ya Kilwa, kundi la Six Killers. Mhudumu nae akapelekwa porini bila kujua ukatili wa sehemu anakopolekwa na jamaa wale. Na majaa hao makatili sasa walikaa sebuleni na kuwaza na kujadiliana nini cha kufanya baada ya matokeo mabaya sana. Kijana mbishi, kijana mkatili, kijana sugu kabisa Tano wa six killers alikuwa katika mikoko ya pwani ya makuburi. Alikuwa amejificha katika mikoko hiyo akiwaza namna salama ya kutoka katika mikoko na kurudi kambini kwao, porini ngome. Pamoja na uvumilivu wote huo lakini Tano alikuwa anapita katika maumivu makali sana.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni