
Mtunzi: Halfani Sudy
SEHEMU YA KUMI NA NANE
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Kijana mbishi, kijana mkatili, kijana sugu kabisa Tano wa six killers alikuwa katika mikoko ya pwani ya makuburi. Alikuwa amejificha katika mikoko hiyo akiwaza namna salama ya kutoka katika mikoko na kurudi kambini kwao, porini ngome. Pamoja na uvumilivu wote huo lakini Tano alikuwa anapita katika maumivu makali sana.
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
Alikuwa na vidonda mwili mzima, vidonda ambavyo sasa vilikuwa vinapitiwa na na ladha ya chumvichumvi toka katika mikoko ya pwani. Askari walirudi kituoni, kutoa taarifa kwamba Jambazi aliyejulikana kwa jina la Tano alikuwa amewarotoka. Kwa haraka sana habari hizo mbaya zikafikishwa kwa Daniel Mwaseba huku askari wakimwaga mtaani kama njugu kumsaka Tano wa six Killers. Daniel Mwaseba alipopigiwa simu, hakujibu kitu chochote kuhusu ile simu zaidi ya kuitikia tu tena kwa sauti ndogo sana. Mpaka saa sita usiku inaingia ilimkuta Tano pale katika mikoko, muda huo giza lilikuwa la kutisha sana, usiku ukichanganya na uwepo wa mikoko iliyoshonana.
Muda huo wa saa sita ndipo Tano alishuka juu ya mkoko na kuelekea porini Ngome kwa kupitia pori kwa pori. Hakujua, Tano hakujua! Nyuma yake hatua kama kumi na saba, kulikuwa na mtu makini anamfata. Mtu ambaye alilijua lile ficho lake muda mrefu sana. Mtu huyo hakutaka kumkamata. Shida yake ilikuwa ni kutaka kujua tu uelekeo wa Tano utakuwa wapi. Yeye alikuwa na shida ya kuyafahamu makazi ya yule jamaa, aliyejiita Tano. Na sasa ndio alikuwa anafanikiwa kuuona uelekeo wa Tano, na kwa umakini mkubwa alikuwa anamfuata Tano kwa nyuma, bila Tano kuhisi jambo lolote. Masaa matatu yalitosha kumfikisha jambazi Tano kambini kwao huko porini Ngome. Bila kujua kabisa kama nyuma yake kulikuwa na mtu ambaye aliyekuwa akikanyaga kila sehemu ambapo alitoa mguu wake. Mtu huyo akiyemfata Tano kwa nyuma alikuwa makini sana, asiyeruhusu kufanya makosa katika kazi yake. Mpelelezi namba moja nchini Tanzania aliyekuwa anaitwa Daniel Mwaseba.
Masaa matatu yalitosha kumfikisha jambazi Tano kambini kwao huko porini Ngome. Bila kujua kabisa kama nyuma yake kulikuwa na mtu ambaye aliyekuwa akikanyaga kila sehemu ambapo alitoa mguu wake. Mtu huyo akiyemfata Tano kwa nyuma alikuwa makini sana, asiyeruhusu kufanya makosa katika kazi yake. Mpelelezi namba moja nchini Tanzania aliyekuwa anaitwa Daniel Mwaseba. Daniel Mwaseba alitilia shaka uwezo wa mtu yule mapema sana. Aliamua kulifatilia kwa nyuma lile gari pale tu lilipotoka kituo cha polisi likiwa na Tano ndani yake.
Daniel Mwaseba alishuhudia vizuri sana jinsi Tano wa six Killers alivyojirusha wakati gari linatembea kwa kasi kubwa sana! Daniel alishangaa sana umahiri wa jambazi Tano. Kwa mwendo uliokuwa linatembea gari lile la jeshi la polisi na kwa jinsi Tano alivyojirusha angekuwa mtu mtu dhaifu kama mimi na wewe angepasuka vibaya sana. Lakini Tano hakuwa mimi na wewe, alikuwa mtu hatari zaidi ya hatari yenyewe. Pamoja na kujirusha namna ile lakini Tano hakuumia kwa kiasi hiko. Daniel akimshuhudia jinsi Tano alivyokuwa anajikokota na kujificha katikati ya mikoko. Bila kujua kama alikuwa anafuatwa na mtu nyuma yake.
Daniel Mwaseba alihakikisha hafanyi kosa lolote kama ilivyo ada yake. Na kweli hakufanya kosa. Wakati Tano wa six killers kajibana katikati ya mikoko, Daniel Mwaseba nae alijibana kwenye mikoko umbali sio mrefu sana na alipojibana Tano. Alikuwa na uwezo wa kumkamata lakini hakutaka kumkamata. Nia yake ilikuwa ni kuona uelekeo wa yule jamaa itakuwa wapi, Daniel Mwaseba alihisi Tano lazima ataenda kwenye maficho yao. Na hicho ndicho kitu ambacho Daniel Mwaseba alichokuwa anakihitaji sana. Kule kwa nje mpelelezi Daniel Mwaseba aliizunguka kwa umakini mkubwa ule ukuta mrefu uliokuwa umezunguka eneo lile.
Pamoja na kuzunguka kwake lakini Daniel Mwaseba hakuipata sehemu muafaka ya kuweza kumruhusu kuingia katika nyumba ile. Ukuta ulikuwa imara na mrefu sana, kiasi kwamba Daniel Mwaseba pamoja na ujasiri wake wote lakini hakuona namna ya kuweza kuupanda ukuta ule. Daniel Mwaseba alikaa chini na kutafakari, akaona bora arejee wakati mwengine ili aweze kuvamia kambi ile na kuumaliza kabisa mchezo unaofanywa na watu wale. Daniel Mwaseba alirejea mjini kwenda kujipanga vizuri tayari kwa kuja kuifanya shughuli mzito atakaporejea tena. Kule ndani kiongozi wa kundi la Six killers, Don Genge alikuwa anamuuliza maswali Tano, na Tano aliyajibu maswali yote kwa ufasaha na umakini mkubwa.
Kwa jinsi Tano alivyowasimulia jinsi alivyotoka katika mdomo wa mamba watu wote walibaki midomo wazi. Walimpongeza Tano kwa ushujaa wake. Pamoja na kumsifia sana Tano lakini taarifa za kuwepo kwa Daniel Mwaseba katika mji wa Kilwa Masoko zilomstua kila mmoja mle ndani. Katika watu waliokuwemo mle ndani hakuna aliyekuwa haijui habari ya Daniel Mwaseba. Walikumbuka vizuri sana jinsi alivyoangamiza na kuteketeza mpango hatari wa angamizo katika mji wa Iringa. Wahenga walisema subira yavuta heri, na kweli. Saa sita ya usiku alimshuhudia yule jamaa akitoka kwenye mikoko alipojificha. Masaa yote matatu aliyokuwa anayatumia kujiburuza kuelekea porini ngome, Daniel Mwaseba alikuwa nyuma yake.
Tano alikuwa kachoka sana, mchoko ulioambatana na maumivu kila sehemu ya mwili wake. Alikuwa anajiburuza kwa shida sana! Daniel Mwaseba alihakikisha hatoi ukelele wowote ule wa kuweza kumsitua yule jamaa. Ilikuwa ni mwendo wa kimyakimya. Porini ilikuwa giza sana, lakini kwa mara nyingine tena Dokta Yusha aliuona umahiri wa yule jamaa aliyekwenda kwa jina la Tano, pamoja na kuwa nyang'anyang'a lakini jamaa alichanja mbuga, na kufika kambini kwao. Daniel Mwaseba kwa macho yake mawili aliushuhudia ukuta mkubwa sana uliojengwa kule porini. Kimoyomoyo alitabasamu, akijua pale ndipo maficho ya wale watu wabaya. Sehemu sahihi aliyokuwa anatamani kuijua, na sasa aliijua.
Alimshuhudia yule jamaa akihangaika kubonyeza kitufe fulani pale mlango, na baada ya dakika kama tano geti lilifunguliwa. Na yule jamaa aliingia ndani ya ule ukuta kwa mwendo wake uleule wa kujiburuza, kisha geti lilifungwa tena. Daniel Mwaseba aliyashuhudia yote hayo akiwa kajibanza nyuma ya mti mmoja. Ndani ya nyumba kundi la Six killers lilikuwa katika mshangao. Walishangaa Tano kurejea tena kambini. Kila mmoja alikuwa na swali lake la kumuuliza Tano, mtu aliyerudi kimaajabu sana kambini, akiwa na vidonda kadhaa mwilini mwake, lakini hawakuweza kumuuliza chochote.
Ruhusa ya kuuliza maswali alikuwa nayo kiongozi wa kundi lile pekee, Don Genge. Huko mkoani Mtwara katika hospitali ya misheni ya Ndanda, hali za wagonjwa wa Dokta Yusha zilikuwa kidogo zinaendelea vizuri. Angalau Nasra Mpaukha, mke wa Dokta Yusha na Hasina Omary, mpambe wa Bi harusi na rafiki kipenzi wa Nasra sasa hali zao zilikuwa zinaleta matumaini. Kwa upande wa Nasra sasa alikuwa anaweza kupumua mwenyewe bila ya msaada wa mashine. Sasa alikuwa anaweza kuongea kwa kupapasia ingawa hakuwa na kumbukumbu yoyote ya mambo yaliyotokea nyuma. Hali ya Hasina ilikuwa mzuri zaidi.
Alikuwa anakula na kuongea kama kawaida na kidogo alianza kurejewa na kumbukumbu ya yaliyotokea nyuma. Kutengamaa kwa hali za watu hao wawili zilimtia faraja sana Dokta Yusha, maana aliona dhamira yake ya kwenda Kilwa, kuwakomboa watu wa Kilwa juu ya sakata lile la kutisha ilikuwa inaelekea kutimia, tena matumaini yaliongezeka siku baada ya siku. Dokta Yusha aliendelea kukaa hospitalini Ndanda, kuziangalia hali za wagonjwa wake kwa siku tatu zaidi. Siku ya nne Dokta Yusha alikuwa ndani ya basi la Nsungia akielekea Kilwa Kivinje. Aliamua kwenda kuanzia kilwa Kivinje akiamini ndipo mahali sahihi lilipoanzia suala hili na ndipo ataenda kulimaliza. Gari lilipofika Kilwa Kivinje.
Dokta Yusha alikuwa abiria wa wa tatu kushuka katika basi la Nsungia. Moja kwa moja alianza kutafuta nyumba za mahasimu wake. Saa nane mchana ilimkuta Dokta yule kijana, Dokta Yusha akigonga bila wasiwasi wowote katika mlango wa nyumba ya dokta katiri wa kike, Dokta Sharifa Juma. Dokta Yusha aligonga hodi mara tatu mlango wa Dokta Sharifa Juma, alisimama kidogo baada ya kugonga ile mara ya tatu akisikilizia ndipo alisikia kelele za miguu ya mtu ikielekea pale mlangoni ishara kuwa kuna mtu alikuwa anaenda kufungua ule mlango. Dokta Yusha alijipanga vizuri pale mlangoni, tayari kwa lolote kitakachotokea pale mlangoni.
Mlango ulifunguliwa, msichana mmoja mdogo mwenye umri kati ya miaka kumi na sita na kumi na nane ndio alienda kufungua ule mlango. "Shikamoo kaka" Yule msichana alimsalimia Dokta Yusha pale mlangoni. "Marhaba hujambo binti" Dokta Yusha aliitikia ile salamu huku macho yake yakiangalia moja kwa moja hadi ndani ya nyumba ile. "Sijambo kaka" Msichana aliitikia kwa sauti yake ya upole. "Dokta Sharifa nimemkuta?" Dokta Yusha alitupa karata yake kwa kumuulizia adui yake. Alijitahidi kuuliza kwa sauti ya kawaida kuficha hasira zake kwa Dokta huyo. "Hapana, dada hayupo" Yule msichana alijibu. "Kaenda wapi?" Dokta Yusha aliendelea kumuhoji yule dada. "Dada siku ya tatu leo hajarejea nyumbani, na simu yake haipatikani sijui hata yuko wapi?" Yule msichana alielezea kwa kirefu.
Dokta Yusha akajua mambo sasa yameiva. Kwa vyovyote Dokta Sharifa na wanaharam wenzie watakuwa sehemu fulani, wakiwa wanapanga mambo yao, na pengine kuamua kuzima simu kabisa ili kupunguza bugdha toka kwa watu. Dokta Yusha aliwaza hayo kwa haraka kichwani mwake, huku mdomoni mwake akitoa jibu. "Sawa binti" "Akija dada nimwambie alikuja nani?" Msichana yule aliyeonesha dalili ya uwerevu mkubwa aliuliza. "Mwambie alikuja Dokta makini, Dokta mwadilifu, Dokta mchapakazi, utakumbuka hilo jina?" "Ndo jina lako hilo? Nitalikumbuka" Msichana alisema huku akitabasamu.
Dokta Yusha alimuaga yule msichana mwerevu anayefanya kazi kwa Dokta katili sana na kuondoka zake. Sasa alielekea nyumbani kwa Dokta mwengine katili, Dokta Zaidi Kilumba. Huko alikutana na kijana wa kiume mlangoni. Mdogo wake na Dokta Zaidi Kilumba, naye alimpa taarifa zilezile kama alizozipata nyumbani kwa Dokta Sharifa Juma, habari za kutoonekana Dokta Zaidi Kilumba nyumbani kwake kwa siku tatu. Kengele ya hatari ikagonga kichwani kwa Dokta Yusha.
Iweje dokta Zaidi Kilumba na Dokta Sharifa Juma wote wasirejee nyumbani kwao kwa siku tatu? Kuna nini kinachoendelea. Dokta Yusha alitamani apafahamu kule katika kambi ya mateso alikopelekwa kabla, lakini hakuwa anajua kabisa njia ya kumfikisha kule. Dokta Yusha aliamua kutembelea katika nyumba za wale manesi watano waliokuwemo katika mpango huu hatari.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi