
Mtunzi: Halfani Sudy
SEHEMU YA KUMI NA TISA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Dokta Yusha alitamani apafahamu kule katika kambi ya mateso alikopelekwa kabla, lakini hakuwa anajua kabisa njia ya kumfikisha kule. Dokta Yusha aliamua kutembelea katika nyumba za wale manesi watano waliokuwemo katika mpango huu hatari.
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
Aliowaona siku ile na aliwakumbuka vizuri sana. Ingawa kwa shida lakini alizipata nyumba zao kwa kuulizia kwa watu, nako ujumbe ulikuwa uleule. Wahusika wote wa mauaji yale ya kikatili walitoweka majumbani mwao kwa takribani siku tatu. Dokta Yusha aliamua kwenda Kilwa Masoko alihisi labda huko atapata kitu cha
kumsaidia kujua chochote juu ya sakata hili hatari. Siku hiyo usiku ulivyoingia ndio Daniel Mwaseba alikuwa anarejea tena kule porini, Ngome. Kuona jinsi ya kulisambaratisha kundi hatari la Six Killers. Mchana wa siku ile alienda katika kituo cha polisi Masoko na kupewa baadhi ya vitu akivyovihitaji, ikiwemo na pikipiki kwa ajili ya kumfikisha kule porini. Sasa Daniel Mwaseba akiwa katika chumba chake katika hoteli ya Kimbilio, alivaa suruali nyeusi aina ya jeans pamoja na T-shirt nyeusi yenye matirio ya mpira iliyombana vizuri katika mwili wake. Chini alivaa raba nyeusi vyepesi maalum kwa ajili ya mapambano.
Upande wa kulia na wa kushoto kiunoni mwake alikuwa na bastola, moja kila upande. Huku mgongoni akiwa na begi dogo jeusi alimoweka kamba pamoja na zana zingine kwa ajili ya kwenda kukamilisha kazi yake hii hatari. Nyuma ya pikipiki lake aina ya Kawasaki ambalo lilikuwa linamsubiri kwa nje aliweka chuma kikubwa na kizito maarufu kama nanga pamoja na kama ngumu ya mwani. Saa sita ya usiku aliwasha pikipiki yake kwa mwendo wa taratibu na kuelekea porini ngome. Alipofika karibu na ile nyumba Daniel Mwaseba aliipaki pikipiki yake pembeni mbali kidogo na lile eneo la kambi ya kundi la Six Killers. Akihofia kelele za pikipiki yake kuwastua watu waliokuwepo ndani ya kambi ile hatari. Daniel Mwaseba aliifungua ile nanga nyuma ya pikipiki yake.
Aliibeba ile nanga hadi pembezoni mwa ukuta mrefu wa kambi ile. Daniel Mwaseba akafikiria namna sahihi ya kuingia mle ndani kwa kutumia ile nanga, lakini aliikosa, alichokuwa anafikiria kuja kukifanya na ile nanga ilikuwa sivyo. Daniel Mwaseba alipiga mahesabu yake vibaya. Akaiacha ile nanga pale chini. Akaamua kupiga hatua za kimyakimya kwenda katika geti la mlango ule. Alihisi labda hapo nd'o patakuwa sehemu sahihi patapomuwezesha kuingia ndani ya kambi ile hatari. Alichunguza kwa makini kama dakika kumi pale getini ili kupata namna ya kuingia mle ndani, lakini bado hakupata sehemu sahihi ya kuingia mle ndani.
Six Killers walikuwa wamejipanga vizuri sana kiulinzi na usalama. Daniel Mwaseba aliamua kurejea tena upande wa kushoto alikoiacha ile nanga yake. Alifika hadi pale alipoiacha ile nanga, akaipita tu kama hajaiona na kuelekea mbele zaidi. Alitembea hafi akafika nusu ili aumalize ule ukuta. Aliangalia pembeni, akauona mti mrefu pembezoni zaidi ya ule ukuta. Akili za Daniel Mwaseba zikafanya kazi kwa kasi ya haraka. Mithili ya nyani aliupanda ule mti hadi juu. Kwa kutumia taa zao zenye mwanga hafifu sasa alishuhudia ramani nzima ya ile kambi. Kwa kutumia macho yake Daniel alipima umbali toka pale kwenye mti alikokuwepo hadi kwenye ule ukuta. Ulikuwa umbali mkubwa, lakini aliona inawezekana. Daniel Mwaseba alipitisha uamuzi wa kujirusha toka kule mtini ili adondokee mle ndani.
Kwa kutumia macho yake Daniel alipima umbali toka pale kwenye mti alikokuwepo hadi kwenye ule ukuta. Ulikuwa umbali mkubwa, lakini aliona inawezekana. Daniel Mwaseba alipitisha uamuzi wa kujirusha toka kule mtini ili adondokee mle ndani. Haikuwa kazi rahisi kama unavyoweza kufikiria. Ilikuwa kazi ngumu sana inayohitaji mtu wa kufanya hivyo awe na roho ya kijasiri, roho ya kikomando, roho ya paka! Ambayo bila shaka Daniel Mwaseba alikuwa na roho ngumu zaidi ya hizo. Daniel Mwaseba alijirusha bwana toka kule mtini. Alielea hewani mithili ya samaki mkizi. Alipofika ndani ya ile kambi, Daniel Mwaseba alipata maumivu ya mguu kutokana na umbali ule mrefu aliojirusha.
Daniel alisimama kivivu, alijinyoosha kidogo viungo vyake ili kujiweka sawa. Kabla hajafikiria chochote cha kufanya alisikia sauti ya ukelele wa miguu kuelekea pale alipokuwa. Ishara kwamba kuna mtu alikuwa anaelekea pale alipokuwa. Daniel Mwaseba alijibana ukutani akisaidiwa kwa kiasi kikubwa na giza la usiku. Huku akizishukuru taa za mle ndani kwa kutoa mwanga hafifu. Akatulia kidogo, akaangaza huku na huko Alikiona! Daniel Mwaseba alikiona Kivuli cha mtu kikielekea pale alipoangukia awali, akajua bila shaka alikuwa amesikia kishindo chake kile cha kuchumpa. Daniel Mwaseba akasimama imara, akijua muda muafaka wa kupambana umefika. Yule jamaa, ambaye alikuwa Mbili wa Six Killers alisimama pale alipoangukia awali Daniel Mwaseba, huku akiwa kampa kisogo Daniel.
Daniel Mwaseba akaona ile ndio nafasi pekee ya kuitumia. Alimsogelea Mbili kwa mwendo wa taratibu sana, mwendo wa kunyata, hakuruhusu kelele yoyote katika msogeo wake, alimkaribia sana Mbili. Mbili alikuwa kasimama vilevile. Daniel Mwaseba alikunja ngumi, akaurudisha nyuma mkono wake, mkono ule ambao alikuwa amekunja ngumi aliuleta mbele kwa nguvu sana, usawa wa uti wa mgongo wa Mbili wa Six Killers. Daniel Mwaseba alivyotegemea haikuwa hivyo. Ule mkono uliokunjwa ngumi ulikosa wa kumpiga. Mbili pale aliposimama, ingawa alimpa kisogo Daniel Mwaseba lakini alikuwa anahisi kila kitu kilichokuwa kinatokea nyuma yake. Kumbuka vijana hawa walikuwa ni nusu makomandoo, makatili na wanaoweza kucheza na hisia.
Ingawa Daniel Mwaseba hakutoa ukelele wowote ule wa kuweza kumstua mtu hadi anafika pale, lakini Mbili wa Six Killers alikuwa anasikia makelele makubwa sana, ndio alikuwa anapigiwa makelele hisiani. Na ile ngumi ya nguvu toka kwa Daniel Mwaseba kwenda katika uti wake wa mgongo alikuwa ameshaihisi tangu inakunjwa hadi wakati inarushwa. Kazi ya Mbili ilikuwa ndogo sana, kuruka mbele kwa haraka kwa mtindo wa sambasoti na alipotua chini walikuwa wanaangaliana na Daniel Mwaseba uso kwa uso! Balaa! Daniel Mwaseba alistaajabu sana umahiri mkubwa uliooneshwa na yule jamaa. Lakini alishangaa kwa sekunde i mbili ilipotimia sekunde ya tatu naye akajipanga vyema, akajua anapambana na mtu asiye wa kawaida.
Daniel Mwaseba alijirusha juu huku mguu wake wa kulia ukitangulia mbele kuelekea katika kifua cha yule jamaa. Mbili sasa alikuwa amejipanga vizuri, alirudi nyuma kidogo na kubonyea kwa chini, Daniel alipitiliza jumla na kudondoka vibaya sana baada ya teke lake kukosa wa kumpiga. Daniel alinyanyuka kwa kusuasua huku yule jamaa akiwa anamcheka kwa kebehi na dharau. Daniel Mwaseba alijipanga tena, safari hii akiwa makini zaidi alishachoka dharau za yule jamaa. Lakini kwa bahati mbaya kabisa hakufanikiwa kufanya alichotaka kukifanya! Ghafla! Taa zenye mwanga mkali ziliwashwa na uwanja mzima ulikuwa na nuru mithili ya mchana! Balaa Baada ule mwanga mkali wa taa. Ulioleta nuru mahali pote pale, vikafata vicheko vya karaha toka mahali ambako Daniel Mwaseba hakuwa anapajua, yeye alisikia sauti tu.
Lakini Mbili wa Six Killers alipatambua vizuri sana mahali ambako vikipotokea vicheko hivyo. Wakati Daniel Mwaseba akishangaashangaa kutafuta mahali sahihi vikipotoka vicheko hivyo mara mlango mkubwa wa nyumba iliyokuwa mbele yake ulifunguliwa. Walitoka watu watatu walioshiba. Miili imara iliyojengeka vizuri kimazoezi. Vifua wazi huku wakiwa wamevaa pensi za kijeshi zilizo katika mtindo wa timberland, na T-shirt nyeusi za mpira zilizowabana vyema. Jamaa walimsogelea Daniel Mwaseba kwa mwendo wa taratibu huku Daniel nae akijihadhari kwa kusogea nyuma, kinyumenyume. Kwa kasi ya haraka Daniel Mwaseba alichomoa bastola yake iliyokuwa upande wa kulia wa kiuno chake. Akawa anawaelekezea wale jamaa kwa zamu, mara kamuelekezea yule jamaa akiyepambana nae kabla, mara akiwaelekezea wale majamaa watu waliokuwa wanamfata. Wale majamaa hawakujari, walikuwa
wanamsogelea tu Daniel Mwaseba bila uwoga wowote ule. Daniel alirudi nyuma mpaka aliufukia ukuta, akauegemea ukuta huku bastola yake akiwa kaielekeza mbele. Bila kusita wale majamaa watatu walikuwa bado wanamsogelea, bila kusema neno lolote lile. Ilikuwa kama hawaioni ile bastola aliyoishika Daniel Mwaseba. Au labda walikuwa wanaona Daniel Mwaseba kashika kijiti tu kidogo. Hali ilikuwa ya hatari sasa! Jamaa walisogea hadi wakafika pale ukutani, alipokuwa Daniel Mwaseba. Daniel hakutaka kupiga risasi alijua madhara ya kurusha risasi kwa watu ambao asiowajua wamejipanga vipi. Maana kujiamini kwao ilimaanisha wamejipanga vizuri kwa hali ile. Ilibidi asubiri aone watu wale wana nia gani huku akitafuta mpenyo wa kujitoa katika kisanga kile kibaya. "Karibu sana kwenye nyumba ya kifo mpelelezi mahiri nchini Tanzania, Daniel Mwaseba!" Jamaa mmoja kati ya wale watu watatu waliokuwa wanatoka kule katika mlango wa ile nyumba ndogo alisema kwa nyodo na dharau kubwa sana.
Daniel Mwaseba hakujibu kitu chochote alikaa kimya huku akitafuta mbinu ya kutoka salama mahali pale, alitafuta kwa haraka namna ya kujiokoa sehemu ile ya hatari, lakini hakuipata! Ghafla jamaa wale, wote watatu kwa pamoja waliruka juu na huku wakitanguliza mguu wa kulia mbele. Yalikuwa mateke matatu kwa mpigo! Yaliyorushwa kwa ufundi mkubwa sana. Mateke matatu yenye uzito tofauti toka kwa watu watatu tofauti yalitua katika kifua cha mtu mmoja, Daniel Mwaseba. Nguvu ya mateke yale yalimsukuma kwa nguvu Daniel Mwaseba katika ukuta na alijibamiza vibaya sana ukutani! Alisota katika ule ukuta na kudondoka chini taratibu. Kabla hajainuka wale majamaa watatu walisogea kwa kasi pale alipokuwa amedondokea Daniel Mwaseba.
Jamaa aliyekuwa amesimama upande wa kulia alirusha teke lengine kwa mguu wake wa kulia, na yule aliyekuwa amesimama upande wa kushoto nae alirusha teke kwa mguu wake wa kushoto, wakati yule wa kati alikuwa amesimama tu akiangalia ujuzi wa wale wenzake. Mashavu yote mawili ya Daniel Mwaseba yalikutana na shurba. Mateke yote mawili yale yalitua katika mashavu ya Daniel Mwaseba. Damu ziliruka toka katika mdomo wa Daniel Mwaseba. Daniel sasa aliona hakuna tofauti, kufa na kuishi vyote ni sawa, akiwa amelegea kidogo kutokana na mapigo ya wale jamaa aliinyanyua bastola yake tayari kwa kufyatua. Alimuelekeza yule mtu aliyesimama katikati ya wenzake, hakuwa na mzaha sasa Daniel, macho yake yalionesha hivyo.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi