BALAA (19)
Jina: BALAA Mtunzi: Halfani Sudy SEHEMU YA KUMI NA TISA ILIPOISHIA... Dokta Yusha alitamani apafahamu kule katika kambi ya mateso alikopelekwa kabla, lakini hakuwa anajua kabisa njia ya kumfikisha kule. Dokta Yusha aliamua kutembelea katika nyumba za wale manesi watano waliokuwemo katika mpango huu hatari. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Aliowaona siku ile na aliwakumbuka vizuri sana. Ingawa kwa shida lakini alizipata nyumba zao kwa kuulizia kwa watu, nako ujumbe ulikuwa uleule. Wahusika wote wa mauaji yale ya kikatili walitoweka majumbani mwao kwa takribani siku tatu. Dokta Yusha aliamua kwenda Kilwa Masoko alihisi labda huko atapata kitu cha kumsaidia kujua chochote juu ya sakata hili hatari. Siku hiyo usiku ulivyoingia ndio Daniel Mwaseba alikuwa anarejea tena kule porini, Ngome. Kuona jinsi ya kulisambaratisha kundi hatari la Six Killers. Mchana wa siku ile alienda katika kituo cha polisi Masoko na…