BALAA (1)
Jina: BALAA Mtunzi: Halfani Sudy SEHEMU YA KWANZA KILWA KIVINJE , mwaka 1989. Ilikuwa tarehe kumi na tano, mwezi wa nne, mwaka elfu moja mia tisa themanini na tisa. Ilikuwa usiku wa manane, usiku wenye kiza kinene, usiku ulioandamana na mvua kubwa sana, na radi iliyotoa sauti kali na za kutisha sana pamoja na miale yenye mwanga wa kuogopesha. Usiku huo ulikuwa ni usiku muhimu sana, kwa Don Genge pamoja na kundi lake hatari sana. Usiku huo wa tarehe 15 mwezi wa 4 mwaka 1989 katika chumba cha kuhifadhia maiti , katika hospitali ya wilaya ya Kilwa , maarufu kama Kinyonga , iliyopo katika mji wa Kilwa Kivinje, mkoa wa Lindi , kulikuwa na mkutano wa siri. Don Genge akishirikiana na madaktari mahiri wa hospitali ya Kinyonga, pamoja na manesi wenye roho nyeusi, roho mbaya kabisa, roho zisizokuwa na chembe ya huruma hata kidogo, roho zinazojari pesa na kusahau utu, walikuwa wanaendelea na kikao chao cha Siri, kilichofanyika katika chumba cha siri, kikiwahusisha watu wanaojua kutunza siri. Katika kikao hi…