BALAA (2)

Zephiline F Ezekiel
BALAA (2)
Jina: BALAA Mtunzi: Halfani Sudy SEHEMU YA PILI ILIPOISHIA... Dr Yusha akatulia kwa sekunde kadhaa, ndipo aliposikia, kumbe mshereshaji wa sherehe alikuwa amemwambia akakate keki iliyokuwa mbele ili akamlishe mkewe, Nasra , wakati yeye alikuwa busy na simu. "Ndugu bwana harusi tunaomba uje ukate keki na kwenda kumlisha mkeo mpendwa " Mshereshaji alikuwa anayarudia kwa mara ya tano maneno hayo. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Wakati Dr Yusha akiwa mbali kwa mawazo, ya kumfikiria mgonjwa. Dr Yusha alikuwa anawaza, akakate keki ama aende Kivinje kumsaidia mgonjwa. Alikuwa anafikiria kwa kina, kumlisha mkewe mpendwa Nasra ile keki tamu aende kuokoa uhai wa mgonjwa. Nasra, mwanamke aliyekuwa anampenda kuliko kitu chochote hapa duniani alikuwa analia. Hakuelewa kabisa mumewe kakumbwa na nini. Dr Yusha alinyanyua mguu wake wa kulia taratibu na kuelekea kwenye meza iliyowekwa keki, ghafla simu yake iliit…