Machapisho

BALAA (22)

Zephiline F Ezekiel
Jina: BALAA
Mtunzi: Halfani Sudy

SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Hali ilikuwa tete mle ndani kwa upande wa Dokta Kilumba. Vijana wale wawili makini walikuwa wamembana Dokta Kilumba kisawasawa. Mwanasheria mlevi nae alitoka pale mlangoni na kusogea pale walipokuwa Dokta Yusha na Dokta Kilumba. Siku hiyo Mwanasheria alikuwa hajatia hata tone moja la pombe,

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
lakini mwendo wake ulikuwa wa kilevi. Sauti yake ilikuwa ya kilevi. Ama hakika Mwanasheria mlevi alikuwa ameathiriwa sana na pombe, pombe ilikuwa imeweka kambi ya kudumu katika mishipa yake ya damu. Mwanasheria alikuwa akikanyaga mguu mmoja hapa anakanyaga mguu mwengine kule, alikuwa anayumba ndani ya chumba, alikuwa anakwenda mtindo wa zigzag, lakini Mwanasheria alifika alipopakusudia. Pale walipokuwa wale mahasimu wawili, Dokta Yusha na Dokta Kilumba.

Mwanasheria alikuwa akikanyaga mguu mmoja hapa anakanyaga mguu mwengine kule, alikuwa anayumba ndani ya chumba, alikuwa anakwenda mtindo wa zigzag, lakini Mwanasheria alifika alipopakusudia. Pale walipokuwa wale mahasimu wawili, Dokta Yusha na Dokta Kilumba. "Dokta Kilumba, daktari mkuu wa hospitali ya Kinyonga. Daktari msomi uliyekabidhiwa dhima kubwa katika wilaya hii. Dhima ya kuokoa uhai wa wagonjwa. Daktari makini sana, uliyepata mafunzo yako ya udaktari huko katika jiji la Mumbai, India. Daktari mzalendo, uliyekataa kufanya kazi mjini, na kuamua kuja huku wilayani, porini eti kuja kusaidia wananchi maskini wa huku kama ulivyodai mbele ya jopo la madaktari bingwa.

Unakumbuka ulikataa kufanya kazi Muhimbili? Ulikataa kufanya kazi katika hospitali ya Taifa, hospitali iliyopo jijini Dar es salaam, unakumbuka Dokta? Ulikataa dokta, inamaana ulikuwa na mpango huu kabla ndomana uliamua kuja huku kujificha ili ufanye kwa amani ufarauni wako? Una roho mbaya sana Dokta Kilumba, Zaidi John Kilumba sindo jina lako, nakufahamu vizuri Dokta. Si ulisoma shule ya msingi Kigoma wewe? Au nikwambie mwaka uliomaliza? Jua nakufahamu vizuri sana kabla hujajifahamu. But to make story short, Dokta Kilumba maisha yako yapo mikononi mwangu, ni bahati mbaya sana kwako kwakuwa maisha yako yapo mikononi mwa mlevi, mlevi niliyekubuhu, mlevi niliyopitia mengi sana katika maisha yangu, kuishi na kifo kwangu ni sawa tu, kwa hiari yako na hii hasa kama bado unatamani kuishi naomba ujibu swali langu kwa ufasaha bila kunidanganya....." Mwanasheria mlevi kwa sauti ya kilevi aliweka nukta na kumeza mate, huku akimwangalia Dokta Kilumba kwa umakini mkubwa. Kiukweli Mwanasheria mlevi aliongea maneno yaliyowashangaza wote mle ndani.

*****

Kule kambini porini Ngome, hali ya mpelelezi Daniel Mwaseba ilikuwa mbaya sana. Wale majamaa walikuwa walikuwa makatili kweli, walikuwa wamemchakaza Daniel Mwaseba vibaya sana. Walimwacha pale chini akiwa nyang'anyang'a, hatamaniki. Tano toka kundi lile la Six killers, jambazi sugu kabisa alisogea pale alipolala Daniel Mwaseba. Tano alimnyanyua Daniel kwa hasira toka pale chini na kumuweka begani, baada ya kumuweka begani toka akaona bega siyo sehemu sahihi, Tano akagairi, akamtoa begani Daniel na kumnyanyua juu, ilikuwa mithili ya mtu kalibeba pipa tupu. Daniel Mwaseba akiwa hoi bin taaban kule juu alifumbua macho yake, Daniel Mwaseba alifikiria harakaharaka, alitoa na kujumlisha akiwa hewani, baada ya kugawanya na kuzidisha akajua inampasa kufanya kitu kuokoa maisha yake.

Tano, alimwachia Daniel taratibu, huku akiutega mguu wake ule mzima ili Daniel Mwaseba afikie katika goti la mguu ule, nia yake kuu ni kumvunja kiuno. Na kweli Daniel Mwaseba alikuwa anashuka kule juu kuelekea katika lile goti zima la Tano. Daniel Mwaseba aligari akiwa hewani. Aliruka sarakasi huku akiachia teke lililotua katika kidevu cha Tano. Ilikuwa Balaa! Lilikuwa pigo la ajabu lililomshangaza kila mmoja mle ndani. Hakuna aliyeamini uwezo ule wa ajabu aliouonesha Daniel Mwaseba. Pigo lile la ajabu liliondoka na meno mengine mawili ya Tano. Tano alikuwa amepoteza meno manne sasa. Huku Daniel Mwaseba akitua chini akiwa kasimama imara. Daniel Mwaseba alikunja ngumi huku aliwaangalia watu wale kwa zamu na umakini mkubwa sana.

Sasa Daniel alikuwa tayari kwa lolote! Daniel mwaseba alizidisha umakini zaidi maana alijua yuko sehemu hatari sana, tena mbele ya watu hatari sana. Watu ambao kuuwa ni kitu kidogo sana kwao, hawajari, hawaogopi. Mbili wa Six killers naye kwa umakini mkubwa alisogea pale aliposimama Daniel Mwaseba. Mbili alikuwa makini, alikuwa ashazisikia habari kuhusu Daniel Mwaseba. Kwahiyo alikuwa makini kuzizima mbinu zote za Daniel Mwaseba. Mbili alimsogelea Daniel huku akijifanya kutabasamu. Wakati uleule Tano wa Six killers naye alikuwa anaamka pale chini, akiwa na ghadhabu pasi na mfano. Hasira za kufanywa namna ile tena mbele ya bosi wake, Don Genge. Tano naye alijizoazoa kwa taabu na kumsogelea Daniel Mwaseba.

Ilikuwa kushoto Mbili kulia Tano, mbele ya mpelelezi makini, Daniel Mwaseba. Patamu hapo. Ghafla! Mbili wa Six killers alifanya kitu cha ajabu sana. Alidanda chini kwa nguvu. Mdando uliomfanya aruke juu na kuanza kujivingirisha mithili ya feni huku akiachia mapigo mawili kwa nguvu yaitwayo kificho. "Kificho ni pigo asili yake ni Thailand. Pigo ambalo mpigaji anapiga kwa siri hata ukiwa makini kiasi gani kumwangalia huwezi kujua katumia kiungo gani cha mwili kupiga, pigo la kificho likimgusa mpigwaji ni kifo moja kwa moja" Kwa bahati nzuri Daniel Mwaseba alikuwa anaujua vizuri sana mtindo ule wa kificho. Mwenyewe alishawahi kuutimia mara kadhaa mtindo ule wa kificho. Kumbuka katika simulizi iitwayo mpango wa siri. Siku zote, pigo la kificho huzuiwa kwa kificho. Daniel Mwaseba alifanya hivyo.

Alizuia mapigo yale ya kificho kwa kificho. Kati ya watu waliokuwepo pale hakuna aliyeamini uwezo ule wa ajabu wa Daniel Mwaseba. Mara zote pigo la kificho huondoka na roho ya mpigwaji. Lakini cha kushangaza Daniel Mwaseba alikuwa bado anapumua baada ya pigo lile la kificho toka kwa Mbili wa Six killers. Bosi wa Six killers, Don Genge alikuwa anayaangalia yote hayo kwa umakini mkubwa sana, huku akitabasamu. Aliuhusudu sana uwezo uliokuwa unaoneshwa na vijana wake. Mbili alivyotua chini alijipanga imara, huku akimkuta Daniel Mwaseba akiwa imara zaidi yake. Wanaume wawili walikuwa tayari kwa kazi! Mmoja kutetea kazi haramu, mwengine kupinga kazi haramu.

Mbili alirusha teke la nguvu kwa mguu wake wa kulia, teke lililokuwa linaenda katika sura ya Daniel Mwaseba, lakini Daniel aliliona. Alifanya mambo mawili kwa kasi ya haraka sana. Daniel alibonyea kwa chini kidogo huku akiufyatua ule mguu wa kushoto wa Mbili uliobaki chini. Kwa mara ya kwanza tangu waanze kupambana Daniel Mwaseba alikuwa amemuweza Mbili. Jamaa alidondoka chini vibaya sana. Ilikuwa mithili ya gunia la viazi limerushwa toka kwenye fuso. Daniel Mwaseba hakutaka kabisa kushangaa, aliruka juu kiasi na kutua kwa nguvu tena kwa miguu yake yote miwili katika tumbo la Mbili wa six killers. Mbili aliipatapata! Mkanyago ule ulimwingia barabara Mbili. Alitema majimaji mekundu mdomoni bila kupenda, Ilikuwa ni damu!.

Daniel Mwaseba hakuzubaa, aliruka tena juu huku goti lake la mguu wa kulia likielekea shingoni kwa Mbili. Hili sasa lilikuwa pigo la kifo! Lakini cha ajabu goti lile la Daniel Mwaseba halikufika katika shingo ya Mbili. Ndio halikufika kabisa! Tano wa six killers aliingilia kati kumuokoa jamaa yake, maana bila hivyo, Daniel Mwaseba alikuwa ameshageuka mbogo! Tano aliruka juu nae na kumvaa Daniel Mwaseba hukohuko angani. Katika watu wote walikuwa mahali pale, Daniel Mwaseba hakuna mtu aliyekuwa hampendi kama Tano wa Six killers. Tano alikuwa sugu, Tano alikuwa jeuri, na kwa bahati mbaya kabisa ni Tano wa Six killers ndiye aliyemfata Daniel Mwaseba kule angani. Walipotua tu chini Tano hakujiuliza mara mbili, alimuwahi kwa kumbinya Daniel Mwaseba katika koromeo.

Alimbinya hasa! Daniel alisikia maumivu makali sana, alitoa mkoromo usioeleweka, lakini yule jamaa aliendelea kumbinya. Akiongeza nguvu kila mshale wa saa wa sekunde ulivyokuwa unasogea kuelekea kulia. Balaa! Daniel Mwaseba alianza kuona watu wakiwa wamevaa mavazi meupe wakieleaelea hewani, kisha walitoweka ghafla. Mara likaja giza kubwa sana, kitu kimoja tu kikapita katika akili ya Daniel Mwaseba kwamba alikuwa nd'o anaelekea kufa. Baada ya kama dakika moja ya giza lile la ajabu, Daniel hakuelewa tena kilichokuwa kinaendelea duniani. Daniel Mwaseba nae alitoka duniani na kulifata lile giza la kutisha. Daniel Mwaseba aliwafata wale malaika weupe wakioelea hewani. Kule upande.... katika nyumba ya kulala wageni ya Mjaka hali ilikuwa ngumu sana kwa Dokta Kilumba.

Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi walikuwa wamembana vizuri sana daktari yule Mwanaharam. Pamoja na upole wake wote lakini cha ajabu Dokta Yusha sasa aligeuka mbogo. Jasho lilikuwa linamtoka huku akimnyanyasa daktari mwenzake. Tena alikuwa Bosi wake, kumbuka Dokta Kilumba alikuwa ndiye daktari mkuu wa wilaya ya Kilwa. Pamoja na hasira zake zote Dokta Yusha lakini mara kwa mara hakusita kuzishangaa mbinu za mateso akizotumia Mwanasheria mlevi. Mwanasheria alikuwa anatoa mateso ya hali ya juu kwa Dokta Kilumba, tena kwa mbinu zinazotumiwa na majasusi wa kimataifa.

Dokta Kilumba alijitahidi sana kuvumilia mateso ya watu wale wawili.... Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi lengo lao kuu la kumtesa lilikuwa ni Dokta Kilumba awatajie mahali kambi ya watu wale hatari ilipo, na Dokta Kilumba alikuwa anaonesha utukutu. Hakutaka kabisa kuwatajia. Dokta Yusha akahisi yule jamaa labda amekula kiapo cha kutotoa siri. "Hata kama amekula kiapo atasema leo" Dokta Yusha alijisemea kimoyomoyo. Dokta Yusha alijisachi mfukoni na kutoa mashine ya kukatia kucha. Aliishusha suruali ya Dokta Kilumba mpaka magotini. Mwanasheria mlevi alikuwa makini akiangalia kitu alichotaka kufanya Dokta Yusha.

Dokta Yusha aliichukua ile mashine ya kukatia kucha na kuanza kunyofoa vipande vidogovidogo kutoka katika paja la dokta Kilumba. Alikuwa ananyofoa na kuweka sakafuni vile vipande. Balaa! Maumivu makali aliyokuwa anayapata Dokta Kilumba yalimfanya alie kama mtoto mdogo, aliona paja na mwili wake wote kwa ujumla unawaka moto! Bila kupenda huku akipitia katika mateso makali Dokta Kilumba aliwatajia Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi mahali kambi ya Six killers ilipo. Baada ya kutajiwa hawakumuacha Dokta Kilumba pale. Walitoka nae kama rafiki. Mhudumu wa nyumba ile ya kulala wageni hakuelewa chochote kilichokuwa kinaendelea, hakujua kabisa kama mteja wake alikuwa ametekwa.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni