Machapisho

BALAA (24)

Zephiline F Ezekiel
Jina: BALAA
Mtunzi: Halfani Sudy

SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE
ILIPOISHIA...
Bila kupenda huku akipitia katika mateso makali Dokta Kilumba aliwatajia Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi mahali kambi ya Six killers ilipo. Baada ya kutajiwa hawakumuacha Dokta Kilumba pale. Walitoka nae kama rafiki. Mhudumu wa nyumba ile ya kulala wageni hakuelewa chochote kilichokuwa kinaendelea, hakujua kabisa kama mteja wake alikuwa ametekwa.

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
Walitoka nae na kwenda nae hadi katika nyumba ya kulala wageni alikopanga Dokta Yusha na kumfungia kwa ndani katika chumba chake katika nyumba ile ya wageni aliyopanga. Usiku uleule safari ya kuelekea porini ngome ilianza, kambini kwa kundi hatari la Six killers. Pamoja na kupoteapotea sana kule porini lakini wazalendo hawa wawili wenye nia ya dhati ya kuokoa raia wema walifika katika eneo ambako kulikuwa na kambi ya kundi hatari la Six killers. Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi walitumia saa zaidi ya mbili wakizitumia wakiwa nje wakitafuta namna ya kuingia mle katika kambi ile hatari.

Lakini hawakupata namna yoyote ya kuingia kambini kwa kambi ile hatari. Hadi jua la asubuhi linachomoza Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi walibaki wakiwa nje, bado wakihaha kutafuta njia ya kuwawezesha kujipenyeza mle kambini. Mle ndani ya kambi Daniel Mwaseba alikuwa katika hali ngumu sana. Ilikuwa ni hali mbaya zaidi kuwahi kukutana nayo mpelelezi huyu mahiri nchini Tanzania. Baada ya ule mbinyo wa nguvu shingoni, mbinyo aliopewa na jambazi katili, Tano wa Six killers Daniel Mwaseba alipoteza fahamu. Sasa mwili wake usio na pumzi ulikuwa katika chumba cha mateso cha watu wale makatili. Chumba kilekile alichowahi kuingizwa Dokta Yusha baada ya kutekwa kule hospitali Kivinje.

Naam..... Chumba cha kifo kama walivyokuwa wanakiita wenyewe Six killers. Mwili wa mpelelezi Daniel Mwaseba ukiwa haujitambui ulilazwa katika sakafu ukisubiri muda wa kuja kutolewa uhai tu. Tangu saa tisa usiku mwili ule uliowekwa katika chumba kile cha kifo. Masaa matatu baadae Daniel Mwaseba alifumbua macho taratibu. Ni kudra za Mwenyezi Mungu tu zilimusha. Na kitu cha kwanza kukiona japo kwa shida katika chumba kile cha kifo kilikuwa ni kiti, kiti cha kifo! Kiti hatari sana kisichofaa kukaliwa na binadamu. Daniel Mwaseba alijinyanyua taratibu pale chini, akiwa bado yuko makini na kile kiti cha moto, kiti cha kifo! Daniel Mwaseba alikuwa anakiangalia kiti cha kifo huku akitabasamu. Kwa mwendo wa taratibu alianza kukisogelea kile kiti cha kifo! Daniel Mwaseba alikitambua kile kiti cha kifo. Naam...alikitambua! Daniel Mwaseba alikuwa anazijua vizuri sana habari za kile kiti cha kifo. Ni yeye ndiye aliyetumwa na waziri mkuu wa Jamhuri ya

Muungano wa Tanzania kukileta kile kiti nchini, toka katika Jamhuri ya watu wa China. Alikumbuka vizuri kuwa alimuuliza Waziri mkuu kuhusu matumizi ya kiti kile hatari, na alikumbuka kuwa jibu la Waziri mkuu lilikuwa fupi tu.. 'Ni kwa sababu za kiusalama' Daniel Mwaseba alienda China kwa shingo upande. Kwa kuwa hakuridhika kabisa na jibu alilopewa na Waziri mkuu wakati huo. Alikuwa anajua vizuri uwezo na maajabu wa kiti kile. Ni kiti hatari kuliko hatari yenyewe. Pamoja na kuwa na muonekano wa kiti kwa sasa lakini kilikuwa na uwezo wa kubadirishwa na kuwa silaha mbalimbali hatari. Kiti kilikuwa na uwezo wa kuwa Bomu kubwa hatari la maangamizi na kuleta athari kubwa sana sehemu litakaporushwa ama kutegwa.

Kiti pia kilikuwa kinaweza kubadirika na kuwa bunduki kubwa za kivita. Uwezo hatari wa kiti kile nd'o sababu iliyomfanya Daniel Mwaseba aende China kukifata kiti kile kwa shingo upande. Sababu kuu ya mashaka ya Daniel ilikuwa.....Wakati huo nchi haikuwa na uhaba wa silaha katika maghala yake...na wala hakukuwa na tishio la usalama kwa nchi. Sasa kwanini nchi inunue gharama ghali na hatari namna ile? Pamoja na mashaka yake lakini Daniel Mwaseba alienda China, hakutaka kupinga kabisa agizo la Waziri mkuu. Alienda China salama na alirudi Tanzania salama. Na ni yeye mwenyewe ndiye aliyemkabidhi kiti kile Waziri mkuu tena nyumbani kwake. Utaratibu uliotumika kuleta kiti kile na kukabidhi uliendelea kuongeza mashaka kichwani mwa mpelelezi Daniel Mwaseba. 

Na ni yeye mwenyewe ndiye aliyemkabidhi kiti kile Waziri mkuu tena nyumbani kwake. Utaratibu uliotumika kuleta kiti kile na kukabidhi uliendelea kuongeza mashaka kichwani mwa mpelelezi Daniel Mwaseba. Ashaenda kufata ama kuongoza msafara wa kwenda kuchukua silaha mara nyingi, na mara zote hukabidhi kwa Mkuu wa majeshi na wanajeshi wengine wenye vyeo vya juu huku wakishuhudiwa na Amiri jeshi mkuu. Kwa ujumla utaratibu uliotumika kuleta kiti kile ulimshangaza sana Daniel. Lakini mshangao na wasiwasi wa Daniel Mwaseba leo hii ulileta jibu, kiti kile hatari sana alikikuta ndani ya kambi hatari ya Six killers.

Kimefikaje? Maswali mengi sana yalipita katika kichwa cha mpelelezi Daniel Mwaseba. Lakini maswali yote hakuwa na majibu yake kabisa, pamoja na kutopata majibu ya maswali yake lakini Daniel hakuacha kujiuliza maswali ingawa alijua hakukuwa na wa kumjibu . Lakini alijiuliza..... "Je kiti hiki kimekuja kwa bahati mbaya au makusudi katika kambi ya watu hawa hatari?" Daniel Mwaseba alijiuliza kimoyomoyo huku akikiangalia kile kiti. Bahati mbaya kwa maana kundi lile hatari labda walikiiba kiti kile toka mikononi kwa Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Justus Bitesigile, au Waziri mkuu alikuwa na dhamira tangu mwanzoni, dhamira ya kuwaletea kiti kile kundi hatari la Six Killers.

Kwa dhamira hii wanayoifanya watu hawa. Daniel Mwaseba akajua umakini mkubwa zaidi unahitajika katika kutatua mkasa huu mzito! Mkasa wenye sura ya usaliti, mkasa wenye sura ya usiri mkubwa sana. Mkasa wenye nia mbaya kwa nchi ya Tanzania. Hisia kuwa kuna viongozi wakubwa toka serikalini pia wanahusika katika mkasa huu mzito zikatamalaki katika kichwa cha Daniel Mwaseba. Uwepo wa kiti kile mahali pale ulidhihirisha hilo. "Wakubwa, kwa dhamira ipi sasa? Iweje viongozi wa nchi wauwe wananchi wao?, kosa la wananchi ni lipi? Wananchi ndio waliowachagua hao viongozi, kwa hiyo moja kwa moja viongozi wana dhima ya kuwalinda wananchi, kuwahudumia wananchi, Kuhakikisha wananchi wanapata huduma zote za kijamii" Daniel Mwaseba aliendelea kujiuliza mwenyewe na kujielezea mwenyewe.

Tena sasa sio kimoyomoyo tena, alikuwa anaongea kwa sauti ndogondogo...ya kunong'ona. "Sasa kwa mfano wananchi wote wakiuwawa na kundi hatari la Six Killers, tena kuuwawa kikatili na kwa makusudi watawaongoza kina nani hao viongozi waliopo katika mpango huu?" Mawazo pamoja na maswali yasiyokuwa na majibu ya Daniel Mwaseba yalikatishwa na makelele ya kitasa cha mlango, makelele ambayo ilikuwa ni ishara tosha kuwa kuna mtu alikuwa anafungua ule mlango kwa nje na kutaka kuingia ndani. Kwa kasi ya ajabu Daniel Mwaseba alijirusha na kurejea mahali palepale alipolazwa awali. Akalala kwa mtindo uleule kama waliomlaza awali. Daniel Mwaseba akazimia tena! Kelele zile za mlango zilienda sambamba na mlango kufunguka. Mle ndani ya chumba hatari cha mateso aliingia Komando Mbili wa Six Killers. Mbili akiwa kanuna kwa hasira.

Bila kujulikana hata sababu ya Mbili kununa namna ile. Mbili alikuwa kapania kwenda kumuonesha Daniel Mwaseba kuwa yeye ni nani?. Na kwanini alipewa namba Mbili katika kundi lile hatari. Lakini kwa bahati mbaya kabisa alimkuta Daniel Mwaseba hajazinduka bado toka usingizini, usingizi wa kuzimia. Mbili wa Six Killers alimsogelea Daniel Mwaseba pale chini huku akitabasamu. Sasa Mbili aliacha kununa. Alipofika pale mahali ambapo alipolala Daniel Mwaseba, Mbili alijisachi mfukoni na kutoa sindano ndogo ya kushonea nguo. Nia yake kuu ni kutaka kuiingiza ile sindano katika mwili wa Daniel Mwaseba ili aone na kuthibitisha kama Daniel Mwaseba alikuwa amezimia kweli ama ulikuwa ni mchezo tu . Mbili wa Six killers alijisachi mfukoni, alitoa kisu kirefu na kikali mfukoni na kuchana suruali ya Daniel Mwaseba ile sehemu ya paja. Paja la Daniel Mwaseba sasa lilikuwa wazi, likiangaliwa na mtu hatari sana! Laiti lingejua paja lile kinachokuja kukutana nacho, bora lingebaki ndani hukohuko.

Mbili alitoa sindano iliyokuwa imeviringishwa katika kipande cha gazeti. Ilikuwa sindano ndogo nyembamba ya kushonea nguo, lakini Mbili aliishika ile sindano kibabe na kuanza kuizamisha taratibu katika paja la Daniel Mwaseba. Balaa! Sindano ilianza kuingia taratibu katika nyama laini za paja za Daniel Mwaseba. Mwendo ule wa taratibu wa kuingia sindano ile ulienda sambamba na maumivu. Daniel Mwaseba alianza kupata maumivu taratibu....sindano ilipofika robo na maumivu sasa yakashamiri. Kumbuka Daniel Mwaseba alikuwa hajazimia kweli lakini ilimpasa kuvumilia maumivu yale makali, Daniel Mwaseba ilimpasa kutulia tuli kama maji ya mtungini.

Mtikisiko wowote toka kwa Daniel Mwaseba ulikaribisha jambo baya sana..naam mtikisiko wowote ulikaribisha kifo! Ilikuwa ngumu sana kuvumilia maumivu yale makali ya sindano. kwa mtu wa kawaida kama mimi na wewe maumivu yale yalikuwa hayavumiliki, tusingethubutu hata chembe. Lakini Daniel Mwaseba hakuwa mtu wa kawaida kama mimi na wewe. Mafunzo mbalimbali aliyoyapata Daniel Mwaseba yalimtoa katika ubinadamu kidogo na kuanza kumpeleka taratibu katika unyama! Amini usiamini Daniel Mwaseba aliyavumilia maumivu yale.

Hakutikisika wala kuonesha ishara yoyote ile kwamba alikuwa hajazimia. Sindano ilipofika nusu, Mbili wa Six killer akaanza kuichezesha ile sindano ikiwa ndani ya paja. Balaa! Maumivu yakazidi maradufu. Kama kuna binadamu sugu duniani basi Daniel Mwaseba alikuwa ndio mwalimu wake. Pamoja na mtikisiko ule wa sindano, mtikisiko uliokuja na maumivu makali zaidi lakini Daniel Mwaseba alitulia, ilikuwa kama amefariki vile. Utulivu ule wa Daniel ukamfanya Mbili aamini kwamba Daniel Mwaseba alikuwa bado kazimia,

akaichomoa ile sindano kwa haraka sasa na kuamua kuondoka katika chumba kile cha mateso....chumba cha kifo!. Hilo ndio lilikuwa kosa la kiufundi ambalo Mbili wa Six killers atalijutia milele. Kosa la kiufundi na kwa bahati mbaya zaidi alilifanya mbele ya fundi. Kwa mkupuo mmoja Daniel Mwaseba alifungua macho yake yote mawili. Alivuta pumzi kwa haraka na kunyanyuka taratibu. Daniel alitembea kwa mwendo wa kimyakimya lakini wa haraka akimuwahi mbili pale mlangoni. Alimshika Mbili shingoni na kumrudisha Mbili ndani kwa nguvu. Sasa mkao ulibadirika....Daniel Mwaseba akakaa ule upande ulikokuwa mlango huku Mbili akiwa kwa ndani. Wote wakiwa wamejipanga tayari kwa mapambano. Mbili alikuwa na silaha ya kisu tu ambayo ilikuwa imetulia kiunoni,

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni