BALAA (24)
Jina: BALAA Mtunzi: Halfani Sudy SEHEMU YA ISHIRINI NA NNE ILIPOISHIA... Bila kupenda huku akipitia katika mateso makali Dokta Kilumba aliwatajia Dokta Yusha na Mwanasheria mlevi mahali kambi ya Six killers ilipo. Baada ya kutajiwa hawakumuacha Dokta Kilumba pale. Walitoka nae kama rafiki. Mhudumu wa nyumba ile ya kulala wageni hakuelewa chochote kilichokuwa kinaendelea, hakujua kabisa kama mteja wake alikuwa ametekwa. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Walitoka nae na kwenda nae hadi katika nyumba ya kulala wageni alikopanga Dokta Yusha na kumfungia kwa ndani katika chumba chake katika nyumba ile ya wageni aliyopanga. Usiku uleule safari ya kuelekea porini ngome ilianza, kambini kwa kundi hatari la Six killers. Pamoja na kupoteapotea sana kule porini lakini wazalendo hawa wawili wenye nia ya dhati ya kuokoa raia wema walifika katika eneo ambako kulikuwa na kambi ya kundi hatari la Six killers. Dokta Yus…