
Mtunzi: Halfani Sudy
SEHEMU YA ISHIRINI NA SITA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Kufanikiwa huko kwa Inspekta Jasmine kulifanya azidi kutegemewa na nchi, kutegemewa na jeshi la Polisi. Inspekta Jasmine alitegemewa pia na raia wema. Baada ya wiki kadhaa za kuwatafuta wahalifu pamoja na watu na wanafunzi waliopotea katika mazingira ya kutatanisha kugonga mwamba.
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
Inspekta Jasmine ndiye aliyepewa jukumu na Mkuu wa jeshi la Polisi nchini Tanzania ili kwenda Kilwa kupeleleza juu ya upotevu wa watu hao. Inspekta Jasmine sasa alikuwa na siku ya pili ndani ya Kilwa lakini upelelezi wake ulikuwa haujamfikisha kabisa karibu na adui. Ilikuwa siku ya tatu sasa tangu inspekta Jasmine Wahabu awasili Kilwa ili kwenda kutatua utata juu ya kupotea kimaajabu kwa watu ndani ya Kilwa, tena katika hali isiyoeleweka hadi sasa. Siku hiyo ya tatu asubuhi na mapema Inspekta Jasmine ilimkuta akiwa amelala kitandani, katika nyumba ya kulala wageni aliyofikia. Ghafla alisikia sauti ya wimbo wa Daz P, simu yake ya mkononi ilikuwa inaita. Inspekta Jasmine alitupa shuka yake nyeupe pembeni na kuifata simu yake ambayo aliyokuwa anaichaji.
Inspekta Jasmine alitupa shuka yake nyeupe pembeni na kuifata simu yake ambayo aliyokuwa anaichaji. 'Afande Dismas' inspekta Jasmine alisema kwa sauti ndogo. Inspekta Jasmine alikuwa amepigiwa simu na askari polisi aitwaye Dismas. Alibonyeza kitufe cha kijani cha kupokelea simu na kuiweka sikioni ili kusikiliza. Simu kutoka kwa Afande Dismas ilileta kwa inspekta Jasmine taarifa juu ya Dokta aliyekutwa amefungwa kamba katika nyumba ya kulala wageni ya Mikumi. Ilikuwa asubuhi, Mhudumu alimkuta Dokta Kilumba akiwa kafungwa mle chumbani alipokuwa anaenda kufanya usafi wa kile chumba. Mhudumu aliamua kumtaarifu Bosi wake kisha kupiga simu Polisi. Baada ya muda mfupi afande Dismas akiwa na askari wengine sita waliwasili pale. Na ndipo waliamua kumtaarifu inspekta Jasmine juu ya tukio lile.
Tokea kule nyumba ya kulala wageni, Inspekta Jasmine alivaa nguo za kiraia haraka, alivaa suruali aina ya jeans na tshirt nyeusi na kuelekea eneo la tukio. Baada ya uchunguzi wa kiaskari mle chumbani walimchukua Dokta Kilumba na kumpeleka hospitali. Nia ni kuangalia athari aliyoipata Dokta Kilumba, huku askari Polisi wakiongozwa na inspekta Jasmine wakimsubiri kwa hamu apate nafuu kwa ajili ya mahojiano maalum ili awaeleze kitu kilichotokea mpaka ikatokea akafungwa namna ile. Baada ya kumuacha Dokta Kilumba pale hospitali na kuacha askari kadhaa kwa sababu za ulinzi na usalama. Inspekta Jasmine alitoka hospitali na kuelekea kituo cha Polisi. Mahali ilipokuwepo ofisi yake kwa kipindi chote atakachokuwa Kilwa kwa ajili ya operesheni hii.
Alipoweka kitako tu katika kiti chake, simu yake ya mkononi iliita tena. Safari hii jina lililosomeka katika kioo cha simu yake lilikuwa Songelael.... "Hallo" upande uliopiga ile simu ndio ulioanza kuita. "Nambie Songe" inspekta Jasmine alijibu ile simu huku akiwa makini. "Sasa nimegundua kila kitu Inspekta kuhusu huu mkasa" Songelael aliongea kwa sauti ndogo simuni. Sauti iliyoonesha hakuwa sehemu ya kawaida. "Eeeh umegundua nini Songe" inspekta Jasmine aliuliza kwa shauku kubwa ya kutaka kujua hiko kitu alichokigundua Songelael. " Tusiongee sana Inspekta....njoo katika pori la Ngome sasahivi, ukiwa unakaribia kufika nipigie ili nikupe maelekezo, njoo na askari wengi inspekta " Songelael aliongea kwa kirefu simuni.
Muda huohuo baada ya ile simu toka kwa Songelael gari tano za Polisi zikiwa na Polisi zaidi ya arobaini zilikuwa njiani kuelekea porini Ngome. Gari za polisi zilitembezwa kwa kasi sana huku zikiwa na Askari waliojipanga kivita, na silaha mzitomzito, walikuwa tayari kwa lolote, walikuwa na uhakika na wanachoenda kukifanya baada ya kuhakikishiwa na askari imara wa kike, inspekta Jasmine, kuwa wanakoenda ndio kwenye jibu la wahalifu wote wanaoisumbua Kilwa. Inspekta Jasmine mwenyewe alikuwa juu ya pikipiki kubwa aina ya Kawasaki, naye akielekea porini Ngome kwenda kuumaliza mchezo. Kule ndani ya kambi sasa, Mpelelezi Daniel Mwaseba walikuwa wanatazamana macho kwa macho na Moja wa toka kundi la Six killers.
Kukutana ghafla na Mateka wao akiwa huru kulimfanya Moja asite kidogo, alibabaika kwakuwa hakujua Daniel katokaje katika chumba cha kifo, pia alibabaika kwa kuwa hakujua amfate yupi? amfate yule mtu aliyekuwa kule juu ya ukuta wa kambi yao ama aanze kupambana na huyu aliyepo mbele yake, Daniel Mwaseba. Kusitasita kwa Moja ilikuwa faida kubwa sana kwa Daniel Mwaseba. Baada moja alipata wazo la kutoa bastola yake iliyokuwa kotini, aliamua kuanza kummaliza Daniel Mwaseba kwa risasi, lakini alikuwa amechelewa sana........ Daniel aliruka sarakasi kwa kasi toka pale alipokuwa amesimama na kwenda kumvaa Moja kwa nguvu. Bastola ya Moja ilirudi tena ndani ya koti bila kupenda.
Kule juu ya ukuta alikokuwa Dokta Yusha, alikuwa anashuhudia kila kitu. Sasa Dokta Yusha alikuwa anatafuta namna ya kudumbukia ndani kutokea kule juu ya ukuta. Baada ya kuvamiwa kwa nguvu na Daniel Mwaseba, Moja aliyumba kidogo kisha akasimama imara tayari kwa kupambana na Daniel Mwaseba. Ilhali sasa wote wakiwa mikono mitupu. Kabla hawajaanza hata kurushiana ngumi, Tatu wa Six Killers alitoka nje ya ile nyumba ya bluu, akiwa na bastola mkononi. Tayari kwa kuua! Balaa! Tatu wa Six Killers alivyotoka tu nje aliona mambo mawili kwa mpigo. Kwanza Komando Tatu alimwona Dokta Yusha akiwa anaelea hewani akiingia mle ndani ya kambi yao, Dokta Yusha aliamua kujirusha toka kule ukutani na wakati huohuo aliwaona Moja na Daniel Mwaseba wakiwa wanatazamana kwa chuki wakiwa tayari kwa kupambana.
Bila kutegemea Tatu wa Six Killers nae akapatwa na mfadhaiko mkubwa, mfadhaiko kama alioupata Komando Moja wa Six Killers alivyokutana na hali hii. Daniel Mwaseba nae alimwona Tatu pale mlangoni. Akili yake ilifanya kazi harakaharaka. Kwa muda ule aliona Tatu ni hatari zaidi ya Moja, kwa kuwa Tatu wa Six Killers alikuwa na silaha mkononi. Mpelelezi Daniel Mwaseba alitoka kwa kasi kubwa sana na kufanya kama anamvaa Moja lakini alipitiliza, moja kwa moja alienda kumvaa Tatu pale mlangoni kwa msukumo mkubwa. Msukumo ulioleta faida kubwa sana. Ughafla na nguvu ya msukumo ule uliomwacha Tatu wa Six Killers akiwa kalala chali ardhini bila bastola mkononi. Sasa Daniel Mwaseba ilimpasa kupambana na watu wawili hatari sana. Moja na Tatu wote toka kundi hatari la Six Killers. Moja wa Six Killers alikuwa amefura kwa hasira.
Sasa alikuwa anamfata Daniel Mwaseba kwa ghadhabu, lakini kwa bahati mbaya kabisa hakumfikia Daniel, akiwa katikati katika safari yake ya kumfata Daniel Mwaseba alikutana na MTU! Alikutana na Dokta kijana, Dokta makini, Dokta shujaa, Dokta msomi, Dokta Shupavu, Dokta Mzalendo......Moja alikutana na Dokta Yusha! Tena Dokta Yusha akiwa imara kupambana na jambazi namba moja toka kundi hatari la Six Killers. Waligawana bila kutarajia, yaani ilitokea tu...sasa ilikuwa kila mtu na wake, Tatu wa Six killers na Daniel Mwaseba, Moja wa Six Killers na Dokta Yusha. Tatu wa Six Killers alivyotoka tu nje aliona mambo mawili kwa mpigo. Kwanza Komando Tatu alimwona Dokta Yusha akiwa anaelea hewani akiingia mle ndani ya kambi yao, Dokta Yusha aliamua kujirusha toka kule ukutani na wakati huohuo aliwaona Moja na Daniel Mwaseba wakiwa wanatazamana kwa chuki wakiwa tayari kwa kupambana.
Bila kutegemea Tatu wa Six Killers nae akapatwa na mfadhaiko mkubwa, mfadhaiko kama alioupata Komando Moja wa Six Killers alivyokutana na hali hii. Daniel Mwaseba nae alimwona Tatu pale mlangoni. Akili yake ilifanya kazi harakaharaka. Kwa muda ule aliona Tatu ni hatari zaidi ya Moja, kwa kuwa Tatu wa Six Killers alikuwa na silaha mkononi. Mpelelezi Daniel Mwaseba alitoka kwa kasi kubwa sana na kufanya kama anamvaa Moja lakini alipitiliza, moja kwa moja alienda kumvaa Tatu pale mlangoni kwa msukumo mkubwa.
Msukumo ulioleta faida kubwa sana. Ughafla na nguvu ya msukumo ule uliomwacha Tatu wa Six Killers akiwa kalala chali ardhini bila bastola mkononi. Sasa Daniel Mwaseba ilimpasa kupambana na watu wawili hatari sana. Moja na Tatu wote toka kundi hatari la Six Killers. Moja wa Six Killers alikuwa amefura kwa hasira. Sasa alikuwa anamfata Daniel Mwaseba kwa ghadhabu, lakini kwa bahati mbaya kabisa hakumfikia Daniel, akiwa katikati katika safari yake ya kumfata Daniel Mwaseba alikutana na mtu! Alikutana na Dokta kijana, Dokta makini, Dokta shujaa, Dokta msomi, Dokta Shupavu, Dokta Mzalendo......Moja alikutana na Dokta Yusha! Tena Dokta Yusha akiwa imara kupambana na
jambazi namba moja toka kundi hatari la Six Killers. Waligawana bila kutarajia, yaani ilitokea tu...sasa ilikuwa kila mtu na wake, Tatu wa Six killers na Daniel Mwaseba, Moja wa Six Killers na Dokta Yusha. Kule nje ya kambi ile hatari ya Six killers askari lukuki wa jeshi la Polisi walikuwa wameshakamilisha zoezi la kuizunguka ile kambi pande zote. Lilikuwa zoezi rahisi sana kwa askari Polisi tofauti kabisa na walivyotegemea, urahisi huo ulitokana na umakini wa Six Killers ulikuwa umepungua kutokana na upinzani wa watu wawili mle ndani, upinzani toka kwa Dokta Yusha na Mpelelezi Daniel Mwaseba.
Askari Polisi walikuwa wanaongozwa na yule jamaa aliyempigia simu inspekta Jasmine, aliyejulikana kwa jina la Songelael Ntenga. Jamaa makini aliyewapigia simu askari Polisi na kuwaeleza uwepo wa watu hatari mahala pale. Kule ndani kabisa ya ile nyumba ya bluu. Walikuwa wamebaki watu wawili tu, komando Nne wa Six Killers na mkuu wa kundi hili hatari, Don Genge. Walikuwa wapo sebuleni wakiangalia runinga, bila kujua wala kuhisi kwamba walikuwa katika hatari kubwa sana. Walikuwa wamezungukwa na askari Polisi kwa nje, walikuwa wamevamiwa na Daniel Mwaseba na Dokta Yusha kwa ndani.
Walikuwa wamezungukwa na askari Polisi kwa nje, walikuwa wamevamiwa na Daniel Mwaseba na Dokta Yusha kwa ndani. Wao walikuwa hawana wasiwasi wowote ule, wakijua kuwa hali ya usalama tayari imedhibitiwa vizuri, na vijana wao wawili, Moja na Tatu wa Six Killers, laiti wangejua. Pale nje mapambano yalianza......Tatu wa Six Killers alimfata kwa kasi Daniel Mwaseba huku akitanguliza kichwa chake mbele, lengo lake kuu ni kwenda kumzoa Daniel Mwaseba kwa kutumia kichwa chake kilichokomaa kwa shuruba na mazoezi. Daniel Mwaseba alikuwa aneshatambua tayari nia ya Tatu wa Six Killers, labda pengine kabla ya yeye kufikiria kufanya hivyo. Kumbuka siku zote Daniel Mwaseba alikuwa anaendeshwa na hisia, na mara zote hisia zake zilikuwa sahihi,
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi