BALAA (5)

Zephiline F Ezekiel
BALAA (5)
Jina: BALAA Mtunzi: Halfani Sudy SEHEMU YA TANO ILIPOISHIA... Waliisukuma machela ile kuelekea pale alipokuwa Dokta Sharifa, ili Dokta afanye kazi ile ya kikatili ! Kazi ya kuutoa moyo mwili ule, mwili wa mkwe wa Dokta Yusha . Mwili wa mama Mpaukha ukawekwa katika kile kitanda maalum kwa kazi hii ya kikatili! Dokta Sharifa alinyanyua mkono wake wa kulia ulioshika kisu juu, JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... akakielekeza kile kisu katika upande wa kushoto katika kifua laini cha marehemu mama Mpaukha, akichana taratibu. Kilikuwa ni kitendo cha kikatili sana, lakini daktari yule wa kike alikuwa anakifanya bila wasiwasi wowote. Alikizungusha kile kile kisu kwa mtindo wa duara, kisu maalum kilichokuwa kimezama vizuri katika nyama za kifua cha mama yule. Alipoona imetosha aliingiza mkono wake wa kulia, aliokuwa amevaa gloves, alichezesha mkono wake kama dakika moja katika shimo baya alilolijenga pale kifuani, na ku…