
Mtunzi: Halfani Sudy
SEHEMU YA TANO
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Waliisukuma machela ile kuelekea pale alipokuwa Dokta Sharifa, ili Dokta afanye kazi ile ya kikatili !
Kazi ya kuutoa moyo mwili ule, mwili wa mkwe wa Dokta Yusha.
Mwili wa mama Mpaukha ukawekwa katika kile kitanda maalum kwa kazi hii ya kikatili!
Dokta Sharifa alinyanyua mkono wake wa kulia ulioshika kisu juu,
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
akakielekeza kile kisu katika upande wa kushoto katika kifua laini cha marehemu mama Mpaukha, akichana taratibu.
Kilikuwa ni kitendo cha kikatili sana, lakini daktari yule wa kike alikuwa anakifanya bila wasiwasi wowote. Alikizungusha kile kile kisu kwa mtindo wa duara, kisu maalum kilichokuwa kimezama vizuri katika nyama za kifua cha mama yule. Alipoona imetosha aliingiza mkono wake wa kulia, aliokuwa amevaa gloves, alichezesha mkono wake kama dakika moja katika shimo baya alilolijenga pale kifuani, na kutoka na moyo uliozungukwa na damu!
Aliuweka pembeni kwenye sahani ya chuma moyo ule, na kuanza kuushona mwili ule, mwili usiokuwa na moyo kwa sasa.
Kule wodini 'story' zilinoga kati ya Dokta Yusha na Dokta Kilumba. Walikuwa wanasimuliana mambo mbalimbali kuhusu fani yao ya utabibu. Bila kujua mambo ya siri yaliyokuwa wanaendelea katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Mara, mjomba wake Nasra aliingia wodini.
"Samahani Dokta, inabidi tukautoe mwili wa marehemu ili tukaufanyie maandalizi"
"Sawa, ngoja tumpigie mtu wa chumba cha kuhifadhia maiti" Dokta Kilumba alidakia ilihal hakuambiwa yeye.
Alimpigia Dokta Tamaa, na Dokta Tamaa alimjibu kwamba mambo yako vizuri wakauchukue tu mwili mpendwa wao.
Dokta Yusha akiongozana na ndugu mwengine walienda kuuchukua mwili ule usiokuwa na moyo kwa sasa na kwenda nao Kilwa Masoko kwa ajili ya maandilizi ili wauzike.
Siku ile ya kwanza kundi la Don Genge kwa kishirikiana na madaktari wale wenye roho mbaya kabisa walifanikisha Mpango wao ule wa kinyama!
Siku ya pili Asubuhi, ndio ilikuwa siku ya kuuosha mwili ule tayari kwa kwenda kuuzika. Mshono waliukuta katika kifua cha mama Mpaukha ulimshangaza kila mtu aliyekuwa mle chumbani wakati wanauosha mwili ule…
Wakati mwili unaoshwa, kizaaza kikaibuka!
Mwili wa mama Mpaukha ulikuwa na mshono mkubwa sana ambao ulikuwa haujapona bado.
Mshono uliowaacha midomo wazi waoshaji. Pamoja na mshangao wao lakini waoshaji wale walihisi labda jeraha lile ni mojawapo ya madhara aliyoyapata mama yule katika ajari ile mbaya!
Wakina mama wale Waliamua kukaa kimya na kuendelea na kazi yao ya uoshaji kama kawaida.
Mwili wa mama Mpaukha ulioshwa na kwenda kuzikwa katika makaburi ya Sanga bila uwepo wa mwanae mpendwa, Nasra, bila uwepo wa mumewe kipenzi, Mzee Mpaukha .
Mama Kindumba, alikuwa mlevi maarufu wa kike katika mji wa Kilwa Masoko. Kutokana na kupenda sana kunywa pombe za kienyeji alikuwa na marafiki wengi sana walevi, miongoni mwa marafiki ni Mwanasheria.
Mama kindumba alikuwa anakaa jirani sana na familia ya Mzee Mpaukha. Ujirani huo ndio uliosababisha na yeye apate fursa ya kwenda kuuosha mwili wa mama Mpaukha. Na Mama kindumba ni miongoni mwa watu waliostushwa sana na ule mshono wa mama Mpaukha ulikuwepo pale kifuani.
Baada ya kumzika mama Mpaukha, jioni ya siku ile mama kindumba ilimkuta kilabuni akipata pombe za kienyeji kama kawaida yake. Kikao kilikuwa kimependeza ingawa mwenyekiti wa kikao hiko alikuwa hajawasiri bado.
Baada ya muda mfupi Mwenyekiti aliwasiri huku akiimba wimbo wa bendi ya msondo ngoma. Alikuwa Mwanasheria.
"Eeeeeeh nilikuwa nakusubiri kwa hamu Mwana" mama kindumba aliongea kwa nguvu baada ya kumuona Mwanasheria.
"Kuna nini tena mama kindumba maana nawe huishiwi michapo"
"Ni kuhusu ile ajari yenu" mama kindumba alisema huku anacheka.
"Umeanza kuharibu sasa" sauti ya Mwanasheria ilipoa kidogo.
"Kumbe yule maza alipata bonge la jeraha kifuani. Alichomwa na chuma nini pale"
"Mama gani tena?" Mwanasheria alihoji.
"Si jirani yangu tuliomzika leo kule Sanga"
"Acha zako mama, ushalewa nini, yule mama hakuumia sehemu yoyote. Alikufa bila jeraha"
"We si ulilewa Mwanasheria utakuwa na kumbukumbu kweli, maza alikuwa na jeraha kubwa sana kifuani"
"Hamna kitu kama hicho mama"
Ulizuka mbishano mkubwa sana kati ya mama Kindumba na Mwanasheria. Walevi wengine walibaki kuwa wasikilizaji tu.
"Tusiandikie mate, ngoja nimpigie Dokta Yusha tumuulize, halafu naweka sauti ya nje kabisa" Baada ya mzozo mkubwa Mwanasheria alishauri.
"Simu itakayozua kizaazaa kipya" tusubiri hiyo kesho tuone!"
Mwanasheria akatoa simu yake. Akabofyabofya muda mfupi kuitafuta namba ya Dokta Yusha, aliiona na kuipiga.
Wakati simu ile inapigwa, Dokta Yusha alikuwa wodini. Akiwahudumia wagonjwa mbalimbali, wakiwemo mkewe Nasra na na rafiki wa Nasra, Hasina. Mzee Mpaukha na Musa hali zao sasa zilikuwa vizuri sana.
Akiwa amekaa pembeni ya kitanda cha mkewe simu yake iliita. Kuangalia kioo cha simu yake kilisomeka Mwanasheria, alitabasamu. Alitoka nje na tabasamu lake, alikumbuka vizuri sana vituko vya Mwanasheria. Alitoka nje ya geti ili akaongee na Mwanasheria.
"Hallo"
"Dokta tuna ubishi hapa" Mwanasheria alianza kuongea bila hata salamu.
"Ubishi gani tena?"
"Eti katika ile ajari marehemu alikuwa na jeraha lolote?"
"Hapana, alifariki kwa mstuko tu"
"Aliumia kifuani doktaaaa" sauti ya mama kindumba ilisikika katika ile simu kwa sauti kubwa.
"Hapana, hakuumia!"
"Tafuta mtu yeyote aliyekuwepo wakati wa kuosha maiti atakwambia" Mama kindumba alisema.
Na simu ili katika. Bila shaka kwa kuisha salio ama chaji.
Dokta Yusha alichanganyikiwa sana.
Ingawa taarifa ile ilitoka kwa walevi lakini Dokta Yusha aliipa uzito unaostahili. Alipanga kuufatilia ukweli wa taarifa ile na kuujua ukweli wa taarifa hiyo ya kushangaza.
Tano wa kundi la Six killers bado alikuwa anafatilia nyendo za Dokta Yusha. Na nia yao ya kutaka kumuuwa Dokta Yusha bado ilikuwa palepale. Tano alikuwa anapata ugumu sana kwa kuwa Dokta Yusha alikuwa anakaa wodini muda wote. Wodi yenye wagonjwa muda wote, na kufanya kazi ya kumuua iwe ngumu sana.
Wakati Dokta Yusha akiongea na simu ile, Tano alikuwa hatua chache nyuma yake. Alisikia kila kitu alichoongea Dokta Yusha na Mwanasheria….alilishika kichwani jina la Mwanasheria.
"Mwanasheria anahitaji kuuwawa!" Alilipitisha katika kichwa chake.
Kule kilabuni ubishi bado uliendelea. Huku Mwanasheria akiwa amepata nguvu na kuelekea kushinda. Ubishi sasa ulipata washiriki zaidi, walevi walianza kuchangia mada, huku walevi wengi wakimuunga mkono Mwanasheria.
Tano aliona mambo yao sasa yameanza kuingiwa na vijidudu vibaya. Na jukumu lake lilikuwa ni kuviondosha vijidudu vyote. Sasa naye Mwanasheria akaingia katika orodha ya kifo!
Baada ya kuongea na simu ile toka kwa Mwanasheria, Dokta Yusha alikuwa na mawazo mengi sana. Kwa uyakinifu mkubwa aliipima ile taarifa ya Mwanasheria. Akajua kuna kitu. Alikaa pale kitandani huku akiingalia bandeji kubwa aliyefungwa mkewe kichwani. Kichwa cha Nasra kiliathirika sana. Huku kukiwa na wasiwasi kama Nasra akiamka atarejewa na kumbukumbu zake.
Dokta Yusha alichukua simu yake na kuitafuta namba ya Shangazi yake Nasra. Alijua kwa vyovyote lazima alikuwepo wakati maiti ya mama Mpaukha inaoshwa. Aliiona namba na kuipiga huku akiwa anatoka nje ya wodi.
"Hallo Shangazi"
"Habari Dokta?"
"Safi kwema Shangazi"
"Tupo tu hivyohivyo"
"Kuna kitu nataka nikuulize Dokta"
"Kitu gani hiko Dokta"
"Ulikuwepo kati ya watu waliomuosha marehemu leo?"
"Ndio nilikuwepo"
"Eti marehemu alikuwa na jeraha lolote?"
"Tena kubwa sana kifuani, aisee bila shaka ndio litakuwa limesababisha kifo chake lile"
"Sehemu gani lilikuwepo"
"Juu ya kifua, sehemu unapokaa moyo!"
Mwili wa Dokta Yusha ulipigwa ganzi. Ni yeye ndiye aliyepima mapigo ya moyo ya mama Mpaukha, mara tu walipoingia katika chumba cha matibabu kabla ya mwili ule kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Alikumbuka aliweka kifaa cha kupima mapigo ya moyo sehemu ileile unapokaa moyo. Hapakuwa hata na mchubuko. Iweje leo aambiwe kuna jeraha kubwa sana?
"Halo Dokta….Halloo…unanisikia?"
Shangazi wa Nasra alikuwa anaongea peke yake simuni. Ingawa Dokta Yusha aliweka simu sikioni lakini alikuwa mbali sana kimawazo, alikuwa hasikii chochote.
Usiku uleule Tano alienda Kilwa Masoko. Kummaliza Mwanasheria. Alijua kumuacha hai Mwanasheria basi habari juu ya kidonda kilichoibuka ghafla katika kifua cha mama Mpaukha itaendelea kusambaa. Ilikuwa ni lazima kumuuwa Mwanasheria ili kumziba mdomo milele !
Usiku wa saa nne usiku ulimkuta Mwanasheria akinywa bia katika baa ya Tiga Tisa. Alikunywa bia nyingi sana. Tangu saa kumi na mbili jioni alikuwa hapo akipata ulabu.
Meza ya tatu toka pale alipokaa Mwanasheria kulikuwa na mgeni. Mgeni aliyewasiri pale majira ya saa tatu usiku. Mgeni huyo alikuwa makini kwa kila alichokuwa anakifanya Mwanasheria. Mgeni huyo hakuwa mwengine ila ni Tano wa Six Killers. Alikuwa anamsubiri mwanasheria anyanyuke ili akamfanye alichotaka kwenda kumfanya.
Saa tano usiku Mwanasheria alinyanyuka pale kwenye kiti. Tayari kuelekea nyumbani kwake. Alisogea taratibu kwenye gari yake, alipanda na kuliwasha. Safari kwenda nyumbani kwake ilianza. Tano naye alitoka pale Tiga Tisa. Alichukua pikipiki yake na kulifuata gari la Mwanasheria kwa nyuma.
Mwanasheria alikuwa amelewa hasa. Alipoteza kabisa umakini na hakutambua kabisa kama alikuwa anafuatwa. Alifika nyumbani kwake na kuingia ndani. Kutokana na ulevi Mwanasheria alijikuta amelala katika sofa pale sebuleni.
Tano alipaki pikipiki yake kwa nje. Alifika hadi mlangoni katika nyumba ile ya Mwanasheria. Kwa bahati mbaya nyumba ile haikuwa na fensi.
Kwa kutumia funguo malaya alifungua mlango wa sebule wa Mwanasheria. Ilikuwa ni kazi ndogo sana, kazi iliyodumu kwa dakika tatu. Alifungua mlango na kumkuta Mwanasheria amelala pale sebuleni kama mzoga. Alichomoa kisu chake mkononi. Kwa mwendo wa kunyata akawa anamsogelea pale sofani.
Akamtikisa kidogo, Mwanasheria hakuamka, alikuwa amelewa sana pombe. Alimtikisa tena. Nia ya Tano ni kumuamsha Mwanasheria ili kumjua mtu wa pili aliyedakia ile simu wakati yeye anaongea na Dokta Yusha. Lakini Mwanasheria hakuamka.
Tano aliamua kuua tu, akijipa moyo atamjua tu huyo mtu. Alirudisha nyuma ule mkono uliishika kisu, kwa nguvu aliungiza katika tumbo la Mwanasheria, akatoa akaingiza tena. Alirudia mara nne.Mwanasheria akakata roho akiwa amelewa.
Tano alitoka nje huku akiwa na furaha tele. Bila kujua kama alimuua mtu asiye sahihi. Yeye alimuua Mwanasheria wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa,
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi