Machapisho

BALAA (8)

Zephiline F Ezekiel
BALAA (8)
Jina: BALAA Mtunzi: Halfani Sudy SEHEMU YA NANE ILIPOISHIA... Daktari hakuamini kabisa madhara yaliyotokea mle wodini. Alijishika kichwa huku akipiga kelele za kuomba msaada. Ndani ya dakika chache manesi na baadhi ya watu waliokuja pale hospitali walijaa katika wodi ile. Kila mmoja alistaajabu kilichotokea mle ndani, ilikuwa ni balaa ! Nesi mmoja alipiga simu kituo cha Polisi kuwataarifu juu ya mauaji yale. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Askari waliwasili baada ya muda mfupi sana, na kushuhudia unyama mkubwa waliofanyiwa askari wenzao. Huku Mwanasheria mlevi akiwa ni shuhuda pekee aliyeshuhudia kila kitu. Nusu saa baadae, kundi hatari la Six Killers walikutana tena na bosi wao. Ilikuwa ni furaha kubwa sana kwao, kuitekeleza kazi ile ya masaa mawili kwa nusu saa tu. "Hongereni sana vijana wangu, mmefanya kazi kwa haraka sana, ila sina uhakika kama mmeifanya kwa umakini ninaouhitaji" Don Geng…