BALAA (9)
Jina: BALAA Mtunzi: Halfani Sudy SEHEMU YA TISA ILIPOISHIA... Waulikuta mlango wa chumba cha kuhifadhia maiti upo wazi. Waliingia ndani. Hali aliyoikuta Dokta Yusha mle ndani ilimstua sana! Aliona maiti zimelazwa bila mpangilio mle ndani, tena sakafuni. Maiti zenye majeraha ya kutisha sana, ambayo ni ngumu kutazamwa na macho ya kawaida. Aliangalia watu aliowakuta mle ndani, JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... wote wakiwa makini na shughuli zao za kinyama, walikuwa hawamwangalii kabisa yeye. Macho ya Dokta Yusha yalitua kwa Dokta Sharifa , daktari wa kike alikuwa makini bila wasiwasi wowote, akiishughulikia maiti iliyolazwa juu ya meza mbele yake. Macho ya Dokta Yusha yalitua kwa Dokta Sharifa, daktari wa kike alikuwa makini bila wasiwasi wowote, akiishughulikia maiti iliyolazwa juu ya meza mbele yake. Dokta Yusha aliitazama kwa makini ile maiti akitaka kujua Dokta Sharifa alikuwa anaifanyia kitu gani. Bila …