HATI FEKI (2)

Zephiline F Ezekiel
Jina: HATI FEKI

SEHEMU YA PILI
ILIPOISHIA...
Hakuna taarifa za kukamatwa kwa wahusika japo polisi walikuwa wakiendelea na uchunguzi. Alitaka kumuuliza John kaka yake kama alikuwa akijua lolote linaloendelea kuhusiana na vifo hivyo.

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
Hakujua wazo alilokuwa nalo John kwani alihisi John lazma atakuwa na la kufanya na yeye angetoa ushirikiano.

“Kaka, unampango gani baada ya haya yote,” Antony alimuuliza John siku mbili baada ya kumaliza mazishi.

“Dah, bado…ila nawasubiri hao polisi wakamilishe uchunguzi wao.

Wakati huo John alikuwa akifikiria namna ya kumpata Aminata. John na Antony walianza kufatilia mali za baba yao ili wazirithi. Walizunguka kote na kuongea na watu waliokuwa wameachiwa na kujua maendeleo ya biashara hizo. Walifanikiwa kwenye mali nyingi isipokuwa mgodi wa baba yao.

Utata ukaanza kugubika kwenye suala la umiliki. Baada ya kifo cha baba yake mgodi ulisimama kufanya kazi. Hakuna kilichoendeshwa na wafanyakazi wote walitawanyika wasijue la kufanya.

Hata wachimbaji hawakuelewa. Tukio lililowashangaza wachimbaji wote. Baadhi ya watu walifika na kuwaamuru wasitishe uchimbaji wa madini hadi watakapoambiwa. Iliwashangaza sana. Wachimbaji wote walijua kwamba mwisho wao wa kufanya kazi umefika.

"Mgodi umeuzwa, hahitajiki mtu hapa…..ondokeni,” mmoja wa viongozi wa juu wa kundi la Mosses Ndula, Mbashala aliwapa taarifa. Hali hiyo ilileta sintofahamu huku baadhi ya wachimbaji wakilalamikia.

“Mbona tusipewe taarifa mapema, mnakuja kutuambia wakati tuko kazini, Mzee Amigolas hawezi kutufanyia hivyo, hata watoto wake hawana roho mbaya hivyo, na kama angekuwa anauza mgodi kweli angetufahamisha mapema na kujua hatma yetu, nyie mnakuja tu mnatuambia mgodi umeuzwa…. nendeni, sisi tuende wapi?" Mmoja ya wachimbaji aliyejulikana kama Mbago, ambaye alikuwa ndiye kiongozi wa wa wachimbaji ambaye anamjua sana bosi wake, Mzee Amigolas na watoto wake alikuwa akipingana na watu waliotumwa na Mosses Ndula.

"Tuonyesheni basi vielelezo siyo mnatuambia tu kwa mdomo, kama ni uongo je? Siku zote karatasi za uthibitisho zinatangulia….tutajuaje kama nyie ni matapeli." Mbago aliwataka watoe vielelezo ili wapate uhakika wa kile walichoambiwa.

"Hizo nakala za maelezo hatujaja nazo, ila ukweli ndiyo huo. Mgodi umeuzwa na mnatakiwa mfuate utaratibu uliowekwa. Hakuna chenu hapa. Kuanzia sasa hakuna atakayewalipa,” Hakuna aliyemwelewa. Walianza vurugu. Mbashala na wenzake waliwanyooshea bastola wachimbaji lakini hawakurudi nyuma wala kutetereka.

Baada ya kuona wanazidi kusogea. Mlinzi wa Mbasha alifyatua risasi moja hewani. Hata hivyo wale wachimbaji walizidi kiusogea huku wakiokota mawe makubwa.

“Aaagh…mama n’kufaa,” mmoja wa wachimbaji alipiga kelele baada ya risasi nyingine kufyatuliwa na kumpata ya begani. Sasa waliamua kurusha mawe.

“Nani kakuambia upige risasi.” Mbashala alimfokea Yule mlinzi huku wakiingia haraka kwenye gari na kuondoka. Waliwarushia mawe na kufanikiwa kuharibu kioo cha gari lao.

Baada ya kufanikiwa kuwafukuza. Mbago aliwaita wenzake wote na kujikusanya kwa ajili ya kikao ambacho kngewasaidia kujua hatima yao katika machimbo hayo.

“Jamani sikilizeni, naomba tuzungumzie hili jambo," Mbago aliwatuliza wachimbaji ili azungumze nao. Wachimbaji wote walitii na kukaa chini huku wengine wakiwa wamesimama kumsikiliza kiongozi wao. Yule aliyepigwa aliopelekwa hospitali na kuendelea na matibabu.

“Hili jambo sidhani kama tunakubaliana nalo wote, au siyo jamani?"

"Ndiyoo!Ndiyooo!" Wachimbaji walijibu kwa sauti za kelele kuashiria kuafikiana na kiongozi wao.

“Mwenzetu kapigwa risasi. Inaonyesha hawa watu wanataka kutuingilia kwa nguvu bila kufuata sharia. Wote tunaona kwamba hakuna ndugu au motto yeyote wa mzee wetu Amigolas aliyefika kutueleza. Hata hao wasaidizi wake hawajaja. Iweje wachukue tu mgodi. Lazima tujue.”

“Ndiooo! Ndiooo!” wote walishangilia kauli aliyoitoa Mbago.

Sasa, mi nadhani si jambo zito sana. Mi n’taenda hukohuko nyumbani kwa bosi n’kajue moja. Kama kuna kazi au hakuna. Sisi tumeajiriwa na kama mgodi umeuzwa walipaswa watuambie. Kwani watoto wa Mzee Amigolas si wapo. Mi nafahamiana na John, mtoto wa marehemu. Nitaenda kwao kuongea naye. Hata yeye anaweza kutusaidia. Kesho nitakwenda kujua moja."

“Ndiooo!” Haki haitapotea. Tujue mojaaa,” wachimbaji walishangilia baada ya kusikia kauli ya kiongozi wao.

“Nitaongozana na Masud na Baraka,” Mbago aliwateua wachimbaji wawili ambao angeongozana nao hadi nyumbani kwa Mzee Amigolas.

“Tukamjulieni hali mwenzetu aliyepigwa risasi.”

Polisi walikuwa wameshafika katika eneo hilo. Walihakikisha hali ya usalama inarudi. Mbago alikuwa ameshatoa taarifa polisi juu ya watu waliokuja kuuvamia mgodi na kuwafukuza kazi kwa nguvu. Polisi waliwapa taarifa juu ya mgodi ule. Mosses Ndula alikuwa polisi pamoja na wakili wake. Walikuwa wamepeleka hati ya kuonyesha kwamba kauziwa mgodi na Mzee Amigolas kabla ya kufariki na kwamba umiliki wake ungeanza baada ya miezi sita.

****

John alikuwa njiani akielekea kituo cha polisi cha kati. Hakuwa na taarifa zozote kuhusiana na yaliyotokea Mererani baina ya wachimbaji na watu wa Mosses Ndula. Kichwani kwake alikuwa akifikiria juu ya Aminata. Alitaka kujua ni vipi atampata Aminata.

Aminata Peter, ni mwanamke aliyesomea masuala ya upelelezi na kuwa moja wa wapelelezi wakuu wa jeshi la polisi. Taaluma yake ilimfanya ajuane na watu wengi ikiwapo kugundua njama mbalimbali za watuhumiwa.

Kama ilivyokuwa kwa John na Antony, Aminata alipata pigo kama lililowapata baada ya baba yake pamoja na mama na ndugu zake kufariki baada yua kuuliwa na majambazi wakati wakiwa njiani. Tukio hilo lilitokea baada ya kuwekewa mawe makubwa barabarani na hivyo kushindwa kupita na kuvamiwa.

Baada ya kufanikiwa kuwazuia kupita. Majambazi hao walipora vitu vyao vyote pamoja na kuwafyatulia risasi na kuwaua wote.

Wakati wa tukio hilo la kusikitisha Aminata alikuwa yuko shuleni. Shule ya bweni na hivyo hakuweza kusafiri pamoja na familia yao. Alilia sana kuwapoteza ndugu zake. Upelelezi ulikuwa ukifanyika lakini matokeo hayakumridhisha Aminata ambaye alikuwa na shauku kubwa sana ya kutaka kuwajua wauaji.

Baada ya kumaliza kidato cha sita, Aminata alijiapiza kufa na kupona hadi ajue mtandao wa wauaji wale. Ikiwezekana autokomeze kabisa. Hakumwambia mtu mwingine yeyote juu ya mpango wake huo. Alianza msako wake taratibu.

Alipenda kutoka mida ya usiku ili akakutane na baadhi ya vijana na kuzoeana. Alijua lazima watakuwa baadhi wanaufahamu huo mtandao.

Kwa mara ya kwanza Aminata anaingia ndani ya himaya ya Mosses Ndula. Anakutana na sura za watu wajuao kazi. Sura za kila aina ya wahuni. Haogopi.

Anakutana na kijana mmoja ambaye alikuwa anavuta sigara mlangoni. Anamwangalia sana kisha anapita. Yule kijana anamfuata.

“We nani?” anamuuliza Aminata.

“Mambo kaka angu, mi naitwa Stellah. Nimeshawahi kukuona mahali mjini karibu na Posta.

“Inawezekana,” yule kijana aliwaza huku akionyesha kuvutiwa na Aminata. Aminata alikuwa ni mzuri sana na hivyo kila aliyemwangalia alimtamani.

“Unataka nini huku?” alihoji yule kijana.

“Nadhani nitakuwa nimepotea njia. Samahani sijui huku ni wapi. Naomba unisindikize niweze kutoka huku. Samahani lakini kaka yangu.

“Aah, niko kazini hapa…lakini nitakusindikiza uweze tu kutoka hapa.” yule kijana alikuwa ndiye mlinzi wa mlangoni katika ngome ya Mosses ndula iliyokuwa eneo la Kambi wa Fisi. Huko ndiko Mosse alijua kwamba hasingeweza mtu yeyote kujua kinachoendelea.

“Asante kaka yangu,”aminata alimshukuru yule kaka na kisha alimuuliza jina lake.

“Naitwa Dula,” alisema yule kijana.

“Sasa Dula, nitakutafuta siku nyingine basi. Nimependa ulivyonisindikiza. Napenda tuwe marafiki zaidi.

“Aaah, siamini,” Dula aliwaza huku akitabasamu kwa kutokuamini kama ni yeye. Hakujali kwamba ameacha mlango peke yake na kama atatafutwa na mkuu wake ambaye alikuwa ndani. Alimwacha Aminata akiondoka na kumwachia namba za simu ili wawasiliane.

Dula alirudi haraka. Alifika mlangoni na kwa bahati nzuri hakuna aliyefika hapo tangu atoke na Aminata. Aliendelea kusimama hapo hadi Mosses alipotoka na kuchukua gari lake na kuondoka pamoja na wapambe wake.

Aminata alifika nyumbani. Ilikuwa ni usiku wa saa tano. Hakuogopa kutembea mwenyewe. Baada ya kuondoka mitaa ya Kambi ya Fisi. Alichukua teksi iliyompekleka hadi nyumbani kwake Sakina. Alijilaza juu ya kitanda na kuanza kutafakari juu ya kumwingia Dula ili aweze kumwambia kuhusiana na Mosses pamoja na kundi lao wote.

*****

Asubuhi alimpigia simu Dula na kumtaarifu kwamba wakutane Café la Azziz.

“Unapajua hapo.”

“Ndiyo, lakini ni sehemu hatari sana kwetu sisi hasa ukizingatia na jinsi tunavyojulikana mjini.”

“Unamaanisha nini Dula? Acha woga, we ni mwanamume. Njoo mjini bana. Huko kwenu mbali.”

“Ok poa bibie. Nakuja hapo.” “kumwacha mtoto mzuri kama yule…ni sawa na kuokota dhahabu alafu kuitupa ukiwa na akili zako timamu, waccha niende. Nitamdanganya bosi,” aliwaza Dula huku akitafuta kijana mwenye bodaboda ili aweze kumfikisha aliko Aminata.

Dula alichukua usafiri wa bodaboda hadi alipokuwa Aminata. Kutoka eneo la Kambi ya Fisi hadi Café la Azziz haikumchukua zaidi ya nusu saa. Alimkuta Aminata akimsubiri.

“Dula nikuombe kitu,” Aminata alimwambia Dula mara baada tu ya Dula kushuka katuika bodaboda.

“Nini tena bibie?” alihoji Dula.

“Samahani lakini, sipendi harufu ya sigara.”

“Aaah, hilo tu bibie? ok nikiwa na wewe sitovuta hadi niondoke.”

“Ntashukuru sana.”

“Vipi bibie, za tokea jana?”

“Nzuri tu Dula.”

Dula alikuwa akimwangalia sana Aminata ambaye alikuwa akiendelea kunywa soda yake taratibu. Aliupenda uzuri wake. Alijiona mwenye bahati hasa baada ya kumwona Aminata akiomba msaada na kutaka kuwa marafiki. Hakujua lengo hasa la Aminata hadi kufanya hivyo.

Aminata aliutumia mwanya huo kuwajua vizuri. Alifurahia ushirikiano na Dula. Kila alipomhitaji Dula alikuwa akifika mara moja. Wakati mwingine alimfuata yeye ili Dula asijue lengo lake. Hata baadhi ya rafiki wa Dula walianza kumjua Aminata.

Wakiwa katika ukumbi wa starehe wa Triple A. Aminata alitaka kujaribu bahati yake kwa kumuuliza mengi kuhusiana na kundi lao. Kwa kipindi kifupi cha kujuana na Dula aliweza kuonana na wengi katika kikundi hicho akiwemo Mosses ambaye baada ya Dula kumtambulisha alionekana kumtamani sana Aminata.

“Unakaribisha sana shemeji. Wakati wowote.”

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni