HATI FEKI (5)

Zephiline F Ezekiel
Jina: HATI FEKI

SEHEMU YA TANO
ILIPOISHIA...
Alijuana na viongozi wengi na hata baadhi ya kesi zake zilizimwa kimya kimya kwani waliamini yeye ndo angeweza kuwafanikishia biashara zao haramu.

Alipata kujiamini sana. Ni suala moja tu ambalo aliliwaza sana.

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
Kumiliki mgodi. Mgodi uliokuwa ukitema madini kila kukicha. Mgodi wa mzee Amigolas. Na sasa hati anayo. Kicheko kiilimtoka kila alipofikiria kazi yake ilikuwa rahisi sana hasa baada ya kumtumia wakili wake na kufanikisha kubadilisha hati ya umiliki kwa madai ya kwamba mzee Amigolas alisaini wiki moja kabla hajafa baada ya kuuziana.

Alijiamini kwa kuwa hati sasa iko mikononi mwake. Alijua ikitokea kesi yoyote basi angeonyesha hati hiyo kama kithibitisho. Alicheka. Alimkuwa haishi kumpigia wakili wake simu na kumpa shukrani tena na tena.

Alikumbuka vitisho alivyovitoa kwa mzee Amigolas na familia yake.

“Watoto wadogo sana wale…. Kazi tunajua sisi,” aliwaza na kucheka kwa kicheko cha ushindi. Sigara yake na glass ya wine vilikuwa mkononi vikisindikiza furaha yake. Pafu moja moja lilimkosha na kujiskia fahari.

Siku hiyo kabla ya kumuua mzee Amigolas, alitoa hati ambayo alimpa mzee Amigolas aisaini. Mzee Amigolas alishangaa na kushtuka.

Alikumbuka hati yake ilikuwa ndani ya nyumba yake, iweje Mosses yuko nayo. Alibaki akimwangalia Mosses. Alijua hati yake imechukuliwa. Aliona sehemu alizosaini kabla zikiwa tupu. Alijua kuna mchezo umechezwa. Alijua tayari kadhulumiwa.

“Shika kalamu hii hapa,” Mosses alimkabidhi mzee Amigolas kalamu huku akimnyooshea bastola. Mzee Mosses alikuwa akitetemeka sana. Alijua atakufa. Alimwomba Mosses asimuue.

“Kusaini nasaini. Tafadhali usiniue. Umeshawaua mke wangu na watoto. Naomba uniache. Tafadhali naomba usiniue,” mzee Mosses alimaliza kusaini ile hati na Mosses aliichukuwa na kuiweka mfukoni.

“Mzee mpumbavu wewe, nikikuacha nitawezaje kuchukua hii mali? Lazima ufe.”

“Tafadhaaa….” Kabla hajamalizia kusema alichotaka kusema Mosses alimfyatulia risasi Mzee Amigolas na kumuua. Damu iliruka na kuchafua kila mahali. Kisha Mosse na watu wake walitoka na kukimbia.

*****

Bodi inayosimamia mgodi ambayo iliwekwa na Mzee Amigolas hawakujua kinachoendelea. Hawakuwa na taarifa juu ya kuuzwa kwa mgodi hali iliyowachanganya wote. Wakiwa wanajitayarisha kuelekea nyumbani kwa Mzee Amigolas, walivamiwa na kundi la walinzi wa Mosses Ndula na kuuliwa.

Habari zilifika kila mahali ikiwa ni pamoja na John na Antony waliokuwa wakijitayarisha kwa ajili ya kuanza kumsaka na kumjua aliyefanya mauaji nyumbani kwao.

“Bodi nzima ilikuwa ikija huku John na wote walivamiwa na kuuliwa na majambazi,” Antony alimweleza John ambaye alikuwa amemwegemea Aminata asijue la kufanya.

“Mi nadhani kazi ianze, la sivyo hata sisi tutakuwa hatarini. Ni afadhali tuwe katika mapambano kuliko kuwasubiri waanze kutusaka sisi. Antony hakikisha unaidhibiti hiyo hati isipotee ikiwezekana uipeleke sehemu salama zaidi.”

“Sawa mimi nitafanya hivyo. Nitaipeleka Nairobi kwa mtu ninayemwamini na kumkabidhi hadi itakapohitajika.” Wote walikubaliana na kuamua kuanza kazi.

Kazi ambayo walikuwa wamejipanga vilivyo.

******

Uzuri wa Aminata ulimchanganya sana John. Hakujua kwamba hata kwa upande wa Aminata alikuwa na swali na jibu sahihi kwamba inawezekana kama ikitokea wakiwa wapenzi. Walijikuta wakitoka kwa ajili ya mipango yao.

Hiyo ilikuwa ni baada ya Antony kwenda Nairobi na hivyo katika kumsubiria waliamua kutumia muda huo kujuana na kuanza uhusiano wa kimapenzi.

Walikuwa pamoja kila wakati. Walijikuta wakiingia kwenye penzi zito ndani ya wiki moja tu ambayo Antony aliitumia akiwa Nairobi.

“John, tupo kwenye kipindi kigumu sana lakini siwezi kuuzuia moyo wangu juu yako,” sauti nyororo ya Aminata ilitooka ikiwa imelainishwa na juice baridi ambayo walikuwa wakiburudika ndani ya jumba kubwa na marehemu Mzee Amigolas.

“Hata mi nakupenda sana Aminata, unansaidia sana. Namwomba Mungu tufanikiwe kwenye haya mapambano ili tuendelee kuwa pamoja,” John alisema huku akizishika nywele za Aminata ambaye nay eye alimruhusu John afanye analolitaka. Hali hiyo iliendelea huku mazungumzo nayo yakiendelea.

“Ni wazi hadi sasa tumeshashinda.”

“Ki vipi unasema hivyo mpenzi?” john alikuwa ameshaanza kumpapasa kifuani Aminata na kuyashika vizuri matiti yake yaliyokuwa yamesimama imara. Aminata hakuwa na la kusema. Alizungusha mikono yake nyuma ya mwili wa John na kuanza kumpapasa.

“Nina uhakika na kile nkisemacho John. Kama nlivyokuambia….hee! nini hiko John?” ulikuwa ni mshindo mkubwa wa risasi ambao ulimwangusha chini mlinzi wa nyumba ya Mzee Amigolas. Kwa mara nyingine tena nyumba ya Mzee Amigolas inavamiwa na walinzi wa Mosses Ndula.

“Nimewaona,” John alikuwa akichungulia kwa nje kuona ni kina nani. Walikuwa vijana watatu waliokuwa wamevalia kofia nyeusi za kufunika uso ili wasionekane. Haraka John na Aminata walijihami na kutoa bastola zao na kuzishika kikamilifu.

Penzi liliwekwa pembeni na sasa ukawa ni mpambano kati yao na walinzi wa Mosses. Waliwajibu kwa risasi na kufanikiwa kumpiga mmoja na kudondoka chini. Risasi mfululizo ziliwafanya walinzi wa Mosses Ndula washindwe kuifikia nyumba ya Mzee Amigolas na kujikuta wakirudi nyuma na kutoka nje. Waliwasha gari lao na kukimbia.

*****

“John, wanaondoka,” Aminata alisema huku akiichukua nguo yake na kuvaa. John alichukua haraka funguo za gari ili kuwawahi.

“Tusiwaruhusu wakaondoka John. Tuwafuatilie hadi mwisho wao ikiwezekana tuwamalize wote.” Aminata alisema huku akiufungua mlango na kutoka.

“Sidhani kama watafika mbali. Kwa sababu watakuwa wameelekezwa, hapa wataishia njiani. Hafiki mtu.”

John na Aminata walitoka nje na kuchukua gari na kuanza kuwafukuza. John alihimili usukani vilivyo na kukanyaga mafuta hadi alipowaona. Hawakutumia mwendo mrefu sana wakawa wamewakaribia kabisa. Waliwaona wakikata kona na hivyo waliongeza mwendo na kuikaribia kona huku John akiwa amezima taa za gari ili wasiwaone.

“John usiwakaribie kwanza, watakimbia zaidi. Twende taratibu ili wasijue.”

“Hawatakatiza.”

Kila njia waliopita waliwafuata nyuma. Wakiwa Barabara ya Uhuru. Gari la walinzi wa Mosses Ndula lilikatiza na kuibukia Barabara ya Fire ambayo ilikuwa haina magari. walijua wamewapoteza na hivyo kupunguza mwendo. Hapo wakanza kutupiana lawama baada ya kushindwa kuvamia nyumbani kwa John.

“Risasi imetuharibia kaka,” mmoja wao alianza kulalamika baada ya kuona kwamba mlio wa risasi uliwashtua John na Aminata.

“Kwa nini usingefunga kizuizi sauti isitoke?”

“Dah, askari yule tayari alikuwa ameshanielekezea mdomo wa bunduki aliyokuwa nayo. Hivyo sikuwa na muda wa kuitoa na ukikumbuka lengo letu ilikuwa ni kumteka na kumfunga kamba ndo tuingie kimyakimya.” Yule jamaa alijitetea huku akijilaumu mwenyewe.

Jasho lilikuwa likiwatoka kwani walikimbiza gari sana kuhofia watu kuwakamata baada ya kusikika kwa mlio wa risasi. Sasa walikuwa wakiendesha kawaida baada ya kuona hali ni shwari na hakuna aliyewaona baada ya kukimbiza gari na kuiacha barabara ya Kijenge na kuibukia barabara ya Uhuru na kuingia barabara ya Fire.

Zaidi ya mwendo wa kilomita moja wakawa wanajadiliana na kulaumiana juu ya kitendo kile. Wote wakwa wamenyamaza kimya bada y mmoja wao kuwatishia bastola na kuwaamuru wote wanyamaze.

“Nimesema yaishe. Mnafanya ujinga alafu mnalaumiana. Tutarudi siku nyingine kama leo0 imeshindikana. Nisikie mtu analalamika. Tutamwambia bosi kwamba mambo mabaya. Hawakuwa wamelala na hivyo tulishindwa kulifikia geti.

“lakini akiuliza kwa nini askari amekufa baada ya kusikia taar4ifa. We unadhani itakuaje.”

“Aaaaaah, na we tumia akili. Walipotuhisi sisi askari mmoja alitoka akaanza kurusha risasi ndo tukamuua. Ili mradi sisi wote tuko salama na hawakutujua. Kwa hiyo tusiogopeni. Bosi atatuelewa.”

Ghafla walishangaa kuona gari mbele yao. Aminata na John walifika na haraka. Waliingia kwa mbele yao na kuwazuia wasiweze kukimbia. John alisimamisha gari na Aminata akatoa kichwa dirishani na kuanza kuwarushia risasi ambazo zote zilikuwa zikililenga gari. Aliendelea kuwarushia risasi. Risasi mfululizo zilifyatuliwa na Aminata huku John akiendelea kuwazuia wasiweze kupita.

Wale watu walisikia sauti ya ving’ora vya polisi na hivyo waliona ni hatari zaidi. Waliongeza mwendo kurudisha gari nyuma ili wakimbie lakini risasi moja iliyofyetuliwa na Aminata ilimjeruhi dereva na kusababisha ashindwe kuhimili usukani na gari lao kupindukia ndani ya mtaro wa maji machafu.

Hakuna aliyeweza kutoka kwani walifunga ilango. Mpaka walipoweza kufungua milango ili watoke, polisi walikuwa tayari wameshafika. Ilikuwa ni rahisi kwa John na Aminata kuwaweka chini ya ulinzi. Watu wengi walijazana kushuhudia watu hao wakikamatwa.

Polisi nao walifika mara moja lakini walishindwa kuwachukua wakiwa hai kwani Aminata na John waliwamaliza palepale. Aminata aliwatambua watu wale. Mmoja wao alishangaa kumwona Aminata kabla ya kupigwa risasi.

Askari waliwashangaa John na Aminata. Waliwatambua baada ya Aminata kuwaamrisha wawachukue maiti wale. P[olisi walitii amri ya Aminata. John alishangaa tukio lile la amri iliyotolewa na Aminata. Alitabasamu baada ya kuona akitolewa heshima na wale polisi.

“Mkuu tumekuelewa,” alitania John huku akiingia kwenye gari na kumfungulia Aminata mlango.

“Mwone kwanza.” Alijibu Aminata.

“Mapambano sasa yameanza. Tusirudi nyumbani.” John alisema huku akiwasha gari tayari kuwafuata wengine eneo la Kambi ya Fisi.

“Hapana mpenzi, tukamcheki kwanza mlinzi imekuaje, atakuwa amefariki au yu hai.” Aminata alimsihi John warudi kwanza nyumbani kwa ajili ya kucheki hali ya mlinzi ambaye alikuwa amelala chini baada ya kupigwa risasi ya kifuani.

Walifika na kukuta umati wa watu wakiwa wameuzunguka mwili wa marehemu. Ulikuwa umefunikwa na polisi walikuwa wameshafika baada ya majirani kupiga simu na kutoa taarifa juu ya mauaji na baadaye magari mawili kutoka kwa kasi yakifukuzana. John alisikitika sana.

Walifanya mipango na kuhakikisha askari wao anazikwa ndipo waendelee na mapambano. Alijua lazima wale watu wameshapata taarifa kuhusiana na kufa kwa watu wao wengine na hivyo mara tu baada ya mazishi ya yule askari, John na Aminata waliamua kuendelea kuwafatilia wale watu wa Mosses.

“John, tuwawahi kabla hawajatuwahi, kwa sasa hawajui tulipo. Tumeanza na hao watatu. Tuhakikishe tunawamaliza wote,” Aminata alisema baada ya kuona mambo yamekwisha tulia.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni