HATI FEKI (5)

Zephiline F Ezekiel
HATI FEKI (5)
Jina: HATI FEKI Mtunzi: Hassan S. Kajia SEHEMU YA TANO ILIPOISHIA... Alijuana na viongozi wengi na hata baadhi ya kesi zake zilizimwa kimya kimya kwani waliamini yeye ndo angeweza kuwafanikishia biashara zao haramu. Alipata kujiamini sana. Ni suala moja tu ambalo aliliwaza sana. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Kumiliki mgodi. Mgodi uliokuwa ukitema madini kila kukicha. Mgodi wa mzee Amigolas . Na sasa hati anayo. Kicheko kiilimtoka kila alipofikiria kazi yake ilikuwa rahisi sana hasa baada ya kumtumia wakili wake na kufanikisha kubadilisha hati ya umiliki kwa madai ya kwamba mzee Amigolas alisaini wiki moja kabla hajafa baada ya kuuziana. Alijiamini kwa kuwa hati sasa iko mikononi mwake. Alijua ikitokea kesi yoyote basi angeonyesha hati hiyo kama kithibitisho. Alicheka. Alimkuwa haishi kumpigia wakili wake simu na kumpa shukrani tena na tena. Alikumbuka vitisho alivyovitoa kwa mzee Amigolas na familia yak…