
Mtunzi: Hassan S. Kajia
SEHEMU YA SABA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
USALAMA katika ngome ya Mosses uliwatisha kidogo kina John. Walifika na gari karibu na uzio wa mgodi ule na kuangalia kwa mbali kidogo shughuli zilizokuw zikiendelea kule ndani.
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
Mosses Ndula alifanikiwa kuweka ulinzi mkali. Si polisi wala mtu yeyote aliyeruhusiwa kuingia mle ndani. Hata viongozi nwa serikali na wateja wake wa madini waliofika pale walikaguliwa ipasavyo kuhakikisha hawaingii wala kutoka na chochote. Hakuamini mtu yeyote kwani alijua alifanyalo.
Hata Mosses Ndula alikuwa akitoka kwa msafara wa gari tano hadi sita zikiwa zimebeba walinzi wake pamoja na wasaidizi wake. Gari zote zilikuwa nyeusi zenye vioo vyeusi ambapo ilikuwa ni nadra sana kwa mtu wa nje kuchungulia ndani. Pia mtu asingejua ni gari gani alilopanda Mosses Ndula kwani magari yote yalifanana.
Hakupenda kujulikana japo alijulikana kwa taarifa zake tu kama mmiliki. Hakuna aliyemfahamu kwa sura. Alikuwa si mtu wa kukaa eneo moja. Aliwatumia zaidi wasaidizi wake. Ni katika dili kubwa tu ndipo yeye angetokea na kujihusisha nazo. Dili alizocheza na watu wakubwa ambazo zilihitaji awepo.
Ni mara chache sana John na Aminata waliweza kuuona msafara huo ukipita wakati wa jioni. Hawakuweza kufanya chochote. Francis aliwaelezea juu ya mambo yanayoendelea.
“Mkiona hivyo, mjue mida hii wanaenda sehemu. Na leo ni wiki endi wanaenda hoteli za kifahari na kumbi za starehe. Mosses alipenda sana kustarehe. Alifanya hivyo pasipo kujulikana.
“Huu ndo mwanya wa kuingia ndani na kuwashambulia watakaobakia huko. Tuanzeni leoleo hakuna kusubiria tena,” Aminata alisema huku akiyaangalia yale magari ya Mosses yaliyokuwa kwenye msafara.
Francis alikuwa ni kijana na hivyo alijua mambo mengi yaliyoendelea kwani tangu kuingia kwao alishuhudia ikiwa ni pamoja na kipindi walipoondolewa na kukaa bila kazi. Alikubali kushirikiana nao katika kazi.
“Kwa kweli nna hamu ya kurudi kazini, nitasaidiana na nyie nihakikishe tunawaondoa hawa jamaa,” Francis aliwaambia John na Aminata.
“Safi sana Francis. Na tunakuahidi makubwa endapo tutafanikisha huu mpango,” John alimwambia Francis ambaye alionekana kufurahia dili hilo.
“Uwe makini lakini kwa sababu wanatumia silaha kali sana,” Aminata alimsihi Francis aliyejitolea kuwasaidia kuukomboa mgodi. Aliomba silaha ambayo itamsaidia.
“Hutaweza kutumia silaha wewe, nadhani utafuata tu maelekezo. Pia muda wa kukufundisha hakuna,” Aminata alimwambia Francis.
“Naweza dada angu. Nilishapitiaga jeshi.”
“Acha utani,” John ambaye alikuwa akitazama eneo la uzio wa mgodi, alisema huku akionyesha kwamba hataki utani.
“Kweli John. Naweza na nakuhakikishia nilimaliza mafunzo sema taabu za kule zilinishinda. Ila niko fiti sana.”
John na Aminata walionyesha kupuuzia. John aliwasiliana na Antony ambaye alikuwa ameshawasili mjini Mererani. Alitaka kwenda hadi walipo.
“Tayari tupo karibu na uzio. Na wameondoka hivyo tunataka kuingia.”
“Basi nakuja hapo hapo mlipo tujue tutaingiaje.”
Baada ya dakika kumi na tano, Alifika hadi walipokuwepo John na Aminata. Walikuwa pembeni ya hoteli ya kawaida ambayo ilikuwa ikitazamana kwa mbali kidogo na lango la kuingilia mgodini. Tayari walikuwa wametimia akiwa ameongezeka Francis ambaye alitambulishwa kwa Antony.
"Karibu Antony,” alisema Aminata ambaye alikuwa akimwangalia Antony aliyekuwa ameshika bastola yake huku akiisafisha kwa kitambaa. Kutokana na baridi iliyokjuwepo mjini Mererani, wote walikuwa wamevalia makoti ya kuwakinga nayo.
“Kazi inaanza sasa. Kama tulivyosema, Antony atabakia nje kwanza afu mi na John tutaingia pamoja na Francis. Francis atafika langoni na kuwahadaa kwa kuzungumza na askari kisha mi na John tutakata nyaya na kuingia ndani kisha wakimkatalia Francis kuingia atarudi na kutufata sehemu tuliyoingilia. Sawa?”
“Nimewaza jambo,” Antony alisema.
“Jambo gani tena?” Aminata aliuliza huku akiona kwamba kuna jambo linguine litaingilia uamuzi wao.
“Yule jamaa aliyekuja home kutueleza kuhusu mgodi kuuzwa na aliyewajulisha kuwa jamaa wameanza kazi. Kwani si anafanya nay eye huku?”
“Dah… kweli. Aminata,” aliita John aliyetaka kumweleza jambo Aminata.
“Sema.”
“Kwa nini hatukuwaza jambo kama hilo. Ingewezekana angetusaidia katika kujua kinachoendelea huko ndani ikiwa ni kuwaeleza na wenzake juu ya mpango wetu ili wawe tayari na tuingiapo waweze kutusaidia.”
“Kweli, sasa kwa sasa tunaingia au?”
“Subiri niwasiliane naye kama anapatikana tuweze kufanya naye hii ishu,” John alisema huku akitoa simu yake na kutafuta jina la Mbago. Alimpigia simu.
Simu ya Mmbago iliita bila ya kupokewa. John alipiga tena na tena. Simu haikupokewa.
“Ok, tusichoshane, nimepiga sana hapokei. Sijui kwamba ndo hawaruhusiwi simu huko?”
“Kweli, ndo mlikuwa mnampigia mtu wa huko ndani?”
“Ndiyo, inamaana hawaruhusiwi mawasiliano.”
“Ndiyo hawaruhusiwi. Wanaacha simu zao ndo waingie. Pengine hakuzima yeye ila wanazima na kuingia wakitoka ndo wanazichukua. Na mara nyingi hutoka saa tano usiku,” Francis aliwaelezea kuhusu t5aratibu za mgodi ule. Yeye alifahamu kwani wapo rafiki zake ambao huwa anawatafuta na hawapati.
Hivyo hugundua ya kwamba watakuwa wamezuiliwa simu. Ni hadi pale alipowauliza ndipo walipomwambia ya kwamba hawawezi kutumia simu hadi pale wanapotoka nje ya mgodi.
“Sasa basi, haina haja ya kupoteza muda wale jamaa wakarudi tukashindwa kazi yetu.”
“Ndiyo, tusichelewe basi. Tuanzeni mara moja kabla hawajarudi.”
Mosses Ndula na walinzi wake walikuwa wametoka. Huo ulikuwa ni mwanya kwa kina John kuutumia kuingia ndani na kuwasubiria huko.
******
Alikuwa ni Francis wa kwanza kutoka na kuelekea moja kwa moja hadi katika lango kuu la kuingilia mgodini. Alifika na kubonyeza kengele ambapo alifunguliwa na walinzi. Aliruhusiwa aingia ndani hadi sehemu ya mapokezi na kuanza kuhojiwa. Hakuonyesha wasiwasi wowote zaidi ya kuangalia kwa makini sehemu ambayo John na Aminata walikuwa wakipitia bila kuonwa na askari.
Wakati huo John na Aminata walikuwa wameshatoka na kwenda moja kwa moja hadi kwenye uzio wakiwa wamesheheni kila aina ya silaha waliyoona itawafaa kwa mapambano. Francis hakwenda na silaha.
“Umefuata nini hapa na unatoka wapi?”
“Natokea mjini, nimesikia kuna kampuni mpya ya uchimbaji madini imeanzishwa hivyo nimekuja kuomba kazi ya kuchimba,” Francis alianza kuelezea huku akitazama kama John na Aminata wanaendelea kutafuta njia ya kuingilia.
“Kazi hapa hakuna, wachimbaji wapo wengi, na kwa nini unakuja jioni yote hii karibia usiku unaingia? Ondoka haraka hapa. Uje kesho asubuhi,” mmoja wa wale askari alimfokea Francis ambaye taratibu alianza kurudi nyuma kuelekea mlango ulipo ili atoke aende zake.
Francis hakuonyesha woga. Aliwaona kina John wakiwa wanaingia na yeye aliamua kutoka kiustaarabu ili wale askari wasije wakashtukiwa.
John na Aminata walikuwa wamejificha nyuma ya gari kubwa la mizigo. Hakuna aliyewaona. Walishika silaha zao kikamilifu na kuanza kuelekea mahala nyumba zao zilipo.
Waliwakuta askari wawili nje. Waliwafyatulia risasi. Walitumia bastola zao walizokuwa wamefunga viwambo ili sauti isisikike. Kisha waliingia kwenye zile nyumba na kuanza kuwashambulia askari waliokuwemo ndani.
Walitoka na kuelekea katika nyumba nyingine wakifanya hivyohivyo. Askari wa lango la kuingilia hawakujua kilichoendelea kwani walikuwa wakiua bila ya watu kuwaona. Sasa walifikia eneo la machimbo. Waliwakuta askari wane wakiwa wanawaamrisha wachimbaji wakae chini.
Mmoja wa wachimbaji wale alikuwa Mbago ambaye aliwaona kina John na Aminata. Aminata na John waliwavizi wale askari kwa nyuma na kuwapiga risasi na kuwaua.
Baadhi ya askari waliona tukio lile na hivyo walikimbilia eneo lile ili kuwashambulia kina John. Mbago na wenzake walikuwa wameshachukua zile bunduki ambazo zilikuwa zikitumiwa na wale askari na kuanza kuwashambulia wale askari waliokuwa wakija.
John na Aminata walitoka na kuwaacha pale wakiwamaliza.
“Asibaki hata mmoja….ueni wote,” Aminata alisema kwa sauti kuwaambia wale wachimbaji baada ya kuona sasa mapambano yameanza. Nao walifanya hivyo kwani walichoka na dhuluma na mateso ya askari wale. Nia yao ilikuwa kuwamaliza na pia kumshikilia mkuu wao Mosses Ndula.
*****
Risasi mfululizo zilirushwa na kina John na Aminata kabla ya kuondoka. Walikuwa wakiwazuia wale askari wa Mosses kuwafikia kabla wale wachimbaji hawajasogea na kukaa sawa.
Mbago na wachimbaji wenzake waliendelea kuwamiminia risasi wale askari wa Mosses ambao waliongezeka. Risasi zilirindima kiasi cha kuwafanya wakazi wa Mererani kukimbiakimbia wakihofia maisha yao.
Aminata na John walikuwa wakiwafuata askari wa lango kuu. Walikuwa wote wameshauliwa. Hawakuona mtu yeyote zaidi ya milio ya risasi iliyosikika kutoka kwa wachimbaji waliokuwa wakiwashambulia askari wa Mosses.
“Twendeni huku,” Antony ambaye alikuwa na Francis alitoka katika moja ya ofisi zilizokuwa karibu na lango kuu na kuwashtua kina John na Aminata ambao walikuwa amesimama kwa kujihami wakiangaza huku na kule kuangalia kama kuna adui anakuja.
Antony aliwaelekeza John na Aminata wawafuate walikokua wanakwenda baada ya kuona taa za magari zikiwa zinakuja kuelekea lango kuu.
“Tumeshawamaliza. Nimeona magari yanakuja kule. Njooni huku,” Antony alisema huku akizunguka nyuma ya gari kubwa la kubebea mchanga. Walisimama yeye pamoja na Francis huku kina Aminata John wakisimama ghafla.
“Hapana, tusikae wote upande mmoja. Nyie nendeni na sisi twende huku,” Aminata aliamua kuwagawa na yeye na John walirudi kule ziliko ofisi za Mosses na kuwaacha Antony na Francis wakaenda kujificha nyuma ya magari huku wakiwasubiri Mosses na wenzake warudi. Hakutaka kumwachia John.
Antony alimwangalia na kutabasamu. Aminata naye alitabasamu kama vile kila mmoja alielewa jambo. John hakuwa na la kusema. Alibaki akiangaza huku na kule. Aliyaona magari na hivyo alimshika mkono Aminata na kwenda kujificha kabla hawajaonwa.
Magari yalikuwa yamerudi yote. Hawakuona mtu katika lango kuu zaidi ya miili ya wafu ambao ilikuwa imetapakaa damu. Askari waliokuwa wameongozana na Mosses waliteremka haraka kwenye gari na kuanza kuangalia huku na huko. Hawakuona lolote zaidi ya miili ya askari wenzao.
Ghafla John aliwatokea na kuwamiminia risasi ambazo ziliwashtua Mosses na wenzake.
“Wafuateni,” alifoka Mosses akiwaamuru askari waliobaki wawafuate wenzao.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi