JAMANI DADA MARTHA... LOOO! (10)

Zephiline F Ezekiel
JAMANI DADA MARTHA... LOOO! (10)
Jina: JAMANI DADA MARTHA... LOOO! Mtunzi: 2jiachie SEHEMU YA KUMI ILIPOISHIA... Mara, gari jeusi lilifika na kupaki getini kwa Roi , wakashuka wanaume wawili, wakiwa wamevaa suti nyeusi. Wakatembea kuelekea pale dukani. Wakasalimia wote kisha mmoja wao akauliza... JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... “Jamani tuna shida na Edo...anaishi kwenye nyumba hii,” alisema akionesha kidole nyumba ya Roi... “Sisi hatujamwona...kwenye simu vipi?” alidakia mzee huyo... “Simu yake inaita tu hapokei,” alisema mmoja wa wanaume hao huku wakirudi ndani ya gari na kuondoka zao... “Sasa hawa jamaa wanasema anaitwa Edo...mimi najua anaitwa Ismaili...wewe unasema unamjua kwa jina la Roi...huyu muuza duka anasema anaitwa Evender. Huyu kijana si kawaida,” alisema mzee huyo akionekana kushangaa, akamwangalia Martha ... “Kwani wewe binti, unamfahamu kivipi?” mzee huyo alimuuliza Martha huku akimshika mkono na kwenda naye kando... “Mimi ni…