JAMANI DADA MARTHA... LOOO! (4)

Zephiline F Ezekiel
Mtunzi: 2jiachie

SEHEMU YA NNE
ILIPOISHIA...
“Mmm....mmmm...”

“Mm...mmmm...waaaa...”

Walichukua kama dakika tatu nzima wapo ndani ya denda motomoto huku wakisikika kwa sauti za kuhemka.

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI

ENDELEA...
Miguu yao chini ilitembea sawasawa na kila mmoja na uwezo wake wa kuhimili sakafu.

Ilitembea kama iliyokuwa ikiamrishwa na sauti moja. Ilikuwa kulia...kulia yote, kushoto...kushoto yote! Wakati mwingine mbele...mbele yote pia...

“Baby,” aliita Martha baada ya kujichomoa kwenye denda na Roi...

“Yes darling...”

“Chumbani ni noma, wale wapangaji wenzangu wamekaa nje ya dirisha langu la chumbani...”

“Kwa hiyo itakuaje sista..?”

“Bwana! Kwanza mi sitaki uniite sista...mimi ni baby wako...”

“Sawa sweet...sasa itakuaje?”

“Si hata hapa sebuleni panatosha au?”

“Wewe tu! Unaona panatosha kweli?”

“Panatosha darling,” alisema Martha kwa sauti iliyokwishazidiwa nguvu na joto la mahaba.

Tayari Martha alishalishika lile gauni lake la kulalia ambalo lilimchora umbo lake lote na akalichojoa kwa juu kichwani, akalitupia kule mbali...

“Mmh!” aliguna moyoni Roi kwani kwa mara ya kwanza alimwona vizuri mrembo huyo alivyoumbwa tofauti na siku ya kwanza.

Martha kwa kuwa hakuwa na vazi jingine ndani ya gauni hilo kwa hiyo hakuwa na kibarua kingine cha kuchojoa, akamshika Roi, akamfungua vifungo viwili vya t-shirt aliyovaa, akamnyoosha mikono, akamchojoa nguo hiyo, akammalizia na singlendi!

Akiwa amebakiza vazi la chini tu, Roi alijitegemea mwenyewe kujichojoa, akamaliza na kubaki saresare maua na mwenyeji wake, Martha.

Martha alikimbilia mlangoni kwanza ili kujiridhisha kwamba, umefungwa. Sasa wakati anakwenda, macho ya Roi ambayo yalikuwa kwake, yalikuwa cherekochereko kwa namna wowowo lilivyokuwa likivaibreti kwa papara kama siyo pupa!

“Mbengenyu...mbengenyu...mbengenyu...duu!” alisema moyoni Roi akifuatilia wowowo hilo lilivyokuwa likisumbuliwa na mmiliki wake.

Martha alirudi na kufikia kwenye mwili wa Roi, wakaenda wote hadi chini kwenye sofa kubwa! Puuu!

Kazi ilianza palepale, kila mmoja alikuwa moto kimahaba akimtaka mwenzake. Ni Martha ndiye aliyeonesha kumtaka zaidi Roi kwani alikuwa moto zaidi ya ule wa kifuu!

Kwa vile kila mmoja alijua wanatakiwa kutosikika nje kwa hiyo walicheza kwa ububububu ili sauti isitoke kwenda nje...

“Mm...mmmm...”

“Mm...mmmm...”

Ilikuwa ni miguno tu! Lakini yenye kutoa kielelezo tosha kwamba wapo uwanjani wanajiandaa kwa mechi ya kikubwa!

***

Kule nje, wale wapangaji walikuwa wakizungumza kwa sauti ya chini ili kutoa nafasi kwa sauti za chumbani kwa Martha kuwafikia kama wangekuwa wameingia na kuanza kulisakata kabumbu!

“Itakuwa kaka yake kweli si unaona wako sebuleni...”

“Itakuwa kweli. Lakini wakiingia chumbani tu, ujue ni geresha, hakuna cha ukaka pale,” walizungumza wale wapangaji.

Penzi ni kikohozi kulificha huliwezi, ni kweli kabisa! Licha ya mechi kuihamishia kwenye uwanja wa sebuleni lakini ile wanapuliza kipyenga tu, Martha alianza vuvuzela la mahaba.

“Nyie...nyie kumbe wapo sebuleni kweli lakini si mtu na kaka yake, hebu sikieni,” waliambiana pale nje.

Sauti ya Martha ilisema na kutafsiri kila jambo lililokuwa likiendelea...

“Ooo...”

“Mmm,” aliguna Roi. Hamasa ya mapenzi kwake ilikuwa kubwa sana kiasi kwamba, kila nukta ilikuwa ya furaha kwake.

Kilio cha Martha kilifika nje vizuri sana, wapangaji wenzake wakajisogeza hadi kwenye dirisha la sebuleni na kukaa hapo huku wakijikemea kuwa kimya!

“Ndiyo kaka yake huyu?” mpangaji mmoja aliwaambia wenzake kwa sauti ya chini.

Ilifika mahali, wapangaji hao walitamani kuangalia mechi laivu hivyo wakaanza kuinua vichwa na kusogelea dirishani kabisa lakini pazia lilikuwa madhubuti kutotoa nafasi kuangalia ndani.

Mpangaji mmoja, anaitwa mama Mbega, yeye aliangaza huku na kule na kuona kipande cha mti, akakiokota na kuanza kukipitisha kwenye nyavu, sehemu iliyotoboka. Lengo lake lilikuwa ni kuweka pazia pembeni ili apate nafasi ya kuona mechi inavyoendelea ndani.

“Mh! Jamani tutaonaje sasa ndani?” alisema mama Mbega kwani alishindwa kupenyeza mti kwa kukosa sehemu iliyotoboka.Kelele za Martha ziliwapagawisha wote pale nje. Sasa walikuwa wakihema mihemo kama vile wao ndiyo wako ndani kwenye tukio.

Walishindwa kujizuia mpaka wakaanza kujinyonganyonga huku na kule kwa sababu ya kukumbwa na joto la mahaba ya sauti ya Martha.Martha alisikika kabisa akitangaza nia na kuwafanya wale wa nje kuzidi kuwa moto zaidi...

“Jamani Martha...kwa nini anatufanyia hivi lakini?” wapangaji waliulizana wao kwa wao tena kwa sauti, sema tu Martha na Roi hawakuisikia kwa sababu walikuwa kwenye eneo la mpira wa piga nikupige.

Walipomaliza, wale wapangaji nao wakakimbia. Kila mmoja aliingia ndani kwake na kujilaza kitandani huku wakiugulia maumivu ya joto la mahaba.

“Sweet,” Martha alimwita Roi...

“Niambie.”

“Daa! Afadhali sasa, maana loo...ilikuwa hatari sana,” alisema Martha huku akichekacheka...

“Kwa hiyo sasa umeridhika?”

“Sana tu.”

Wakati Martha anamsindikiza Roi, wale wapangaji walijua, wakatoka kwa mkupuo nje mpaka Martha mwenyewe akashangaa sana...

“Kuna nini kwani? Mbona kama wameibuka kwa mpigo?” alijiuliza Martha lakini hakutoa sauti yake kuwauliza.

“Jamani kaka yangu anaondoka sasa.”

“Oo! Karibu sana kaka.”

“Asanteni sana, siku nyingine.”

“Haya, wasalimie huko, siku nyingine uje hata kama dada yako Martha atakuwa hayupo,” alisema mama Mbega huku akicheka kicheko cha kejeli kama vile moyoni alikuwa akisema...

”Kaka gani wewe Martha, tumesikia kila kitu sisi.”

***

Ulikuwa usiku wa mawazo kwa Martha. Licha ya kwamba alikata kiu yake lakini Martha alijikuta akiumizwa na dhamira mbaya kuhusu Roi...

“Hivi tungebaki kuwa kaka na dada nini kingetokea? Kwanza undugu ungedumu zaidi. Kwa hii hatua tuliyofikia uhusiano wetu utakatika ghafla siku si nyingi,” alisema moyoni Martha akiwa amelala kuangalia juu.

“Ni lazima nichukue uamuzi mgumu. Nimwambie ukweli kwamba tusitishe uhusiano wetu ili ukaka na udada uendelee.”

Alichukua simu, akamtumia meseji Roi...

“Upo?”

Baada ya dakika kumi, Roi alijibu...

“Nipo darling, niambie.”

“Nina jambo linanisumbua, naweza kuchati na wewe kama hutajali?”

“Unaweza baby...”

“Oke. Nimekaa, nimewaza sana. Licha ya kwamba umenikata kiu yangu lakini muda mwingi dhamira inaniambia kwamba tunatakiwa kuendelea kuwa kaka na dada kama makubaliano yetu ya siku ya kwanza kabisa.”

“Mh!” aliguna Roi na ndiyo ikawa jibu lake kwa Martha...

“Usigune Roi, nasema kutoka moyoni mwangu.”

“Mmmh!” Roi alizidisha kuguna, Martha akakasirika na kukaa kimya.

Roi alipoona Martha ametulia, akajua amekasirika, akamtumia meseji...

“Naweza kukupigia?”

“Yes! Unaweza.”

Roi alipiga simu, Martha akapokea haraka sana...

“Halooo...”

“Sista...”

“Yes braza.”

“Umewaza nini tena jamani?”

“Mh! Bro, nimewaza mengi. Mimi nimefikia uamuzi huohuo. Lazima tuendelee kuwa kaka na dada ili uhusiano wetu uendelee kudumu zaidi na zaidi,” alisema Martha...

“Mh! Nikwambie kitu Martha..?”

“Niambie bro...”

“Hata mimi sasa nimeamua kuwa kuanzia sasa hivi tuwe ndugu, tena wa damu moja! Mimi ni kaka yako, wewe ni dada yangu.”

“Loo! Jamani napiga vigelegele, umenifurahisha sana kaka yangu,” alisema Martha.

“Hata mimi dada nimefurahi sana. Unajua tulikuwa tunafanya makosa makubwa sana. Watu tumekubaliana kuwa kaka na dada sasa hizi tamaa nyingine za kutoka wapi?” aliuliza Roi...

“Ndiyo hapo sasa bro,” alishadadia Martha.

Baadaye waliagana wakakubaliana kuwasiliana asubuhi inayofuata ili kujuliana hali.

***

Martha alilala kwa amani na furaha. Alihisi ameutua mzigo mkubwa sana. Ilipofika saa kumi na moja alfajiri, Martha alipigiwa simu na shangazi yake kuwa, mumewe huyo shangazi amefariki dunia.

“Ha! Shangazi kweli? Mbona sijajua kama alikuwa anaumwa?” aliuliza Martha akianza kulia.

“Kafa ghafla Martha.”

Martha alikata simu, akatoka kitandani na kutungua nguo za kuvaa ili kwenda kwa shangazi yake.

Lakini wakati anatoka akampigia simu Roi...

“Kaka, mume wa shangazi yangu kafa ghafla jamani...eeee..ooo,” alilia.

“Wapi?”

“Nyumbani kwake Magomeni.”

“We uko wapi sasa sista?”

“Mimi ndiyo nakwenda huko.”

“Uko wapi?”

“Nipo hapa kituoni Kimara.”

“Nakuja hapohapo kituoni sista.”

Roi alikurupuka, akatoka mbio hadi kwenye gari, akaendesha hadi kituoni Kimara. Akamchukua Martha kwenye gari hadi Magomeni msibani.

Nyumba yote ililipuka kwa vilio, majirani walijaa nao wakilia sambamba na familia ya marehemu. Martha alifikia kulia akiwa ameishiwa nguvu.

Ilibidi Roi ajumuike na wanaume wengine waliokaa nje ili kuona hali inakwendaje.

Kulipokucha, Martha ndiyo akamkumbuka Roi kwamba hawakuagana baada ya kuachana...

“Ooo! My God! Bro atakuwa ameondoka bila kujua nini kinaendelea!” alisema moyoni Martha, akampigia simu huku akiwaza...

“Sikumfanyia fea hata kidogo. Mtu akupe lifti hadi msibani halafu unamwacha bila kumshukuru.”

Simu ilipokelewa, Martha akashtuka kusikia kelele...

“Bro, upo wapi?”

“Nipo hapa nje sista.”

“Haa! Nakuja.”

Martha alitoka mbio hata waombolezaji wengine wakamshangaa. Alimkuta Roi amekaa kwa kujikunyata akitetemeka baridi.

“Ooh! Pole baby,” Martha alijikuta akisema hivyo.

Alimsimamisha Roi, akamvutia pembeni...

“Nisamehe sana sweet, nilichanganyikiwa. Sikujua kama upo nje, mawazo yangu umeshaondoka,” alisema Martha.

“Nilishindwa kuondoka sista,” alisema Roi kwa sauti ya upole huku akimpa pole Martha kwa msiba...

“Asante sana baby. Sijajua mazishi itakuaje? Lakini kikao kitakaa baadaye kwenye saa nne asubuhi,” alisema Martha.

Roi aliaga, akaondoka huku Martha akimsindikiza kwa macho yaliyojaa huruma...

“Maskini. Yaani amekubali kuacha usingizi wake kwa sababu ya msiba wangu. Huenda Roi si kaka yangu,” alisema moyoni Martha.

***

Baada tu ya kikao cha familia cha kujadili namna ya mazishi ya mume wa shangazi yake Martha, Roi akapiga simu kama alijua vile...

“Kaka...”

“Ee dada! Vipi kuhusu utaratibu?”

“Tunazika kesho saa kumi jioni, Kinondoni.”

“Ooh! Nakutumia shilingi laki moja na nusu kama mchango wangu.”

“Da! Nitashukuru sana kaka yangu.”

“Poa...poa! halafu kesho nitakuja kwenye mazishi.”

“Sawa kaka, sawa.”

***

Ulikuwa mchana wenye mawazo kwa Martha...akiwa ametulia tuli huku wachache wakiendelea kulia, aliwaza...

“Hivi kweli yule ni kaka yangu au mume wangu? Ina maana anaweza kunijali kiasi hiki kweli?”

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni