JAMANI DADA MARTHA... LOOO! (6)

Zephiline F Ezekiel
Mtunzi: 2jiachie

SEHEMU YA SITA
ILIPOISHIA...
“Tuachane na udada na ukaka kabisa, tubaki kuwa wapenzi, huenda siku moja tutakuwa mke na mume...”

“Naunga mkono baby, sitaki tena ukaka kutoka kwako...”

“Na mimi sitaki tena udada kutoka kwako.”

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
Martha alianza kupandisha ‘mashetani’ yake ya mahaba. Alitoa mlio wa kumtoa simba kwenye msitu mkubwa huku akisema anachotaka kukifanya. Akapokelewa kwa maneno matamu na Roi.

Walitulia kidogo kuvuta kasi na Martha kujiweka fiti, wakaanza tena lakini safari hii walibadili mapozi, wakaenda na pozi la muunga mboga jikoni, Roi hakufika mbali akatangaza nia.

Sasa walikuwa wamelala wote wakiangalia juu...

“Baby,” aliita Roi...

“Niambie sweet wa mimi!”

“Unajua nakupenda sana, si kama dada lakini bali kama mpenzi wangu.”

“Hata mimi si kama kaka sasa ila kama my baby.”

“Mbali na mwanaume uliyezaa naye ambaye uliniambia alikuacha, una mchumba? Maana hatukuwahi kuliongelea hili hata siku moja.”

“Ni kweli hatujawahi kuliongea hili hata siku moja mimi na wewe, nina mwanaume lakini si mchumba wangu.”

Roi alishtuka, akainuka na kukaa kitandani...

“Vipi tena baby wangu?”

“Nimeshtuka, una mtu?”

“Yes!”

“Ina maana siku ile mpaka nakuja kwako usiku ukasema una kiu, kumbe una mtu?”

“Ninaye sweet lakini alisafiri siku zile, alikuwa Zambia lakini amerudi, yupo mjini kwa sasa.”

“Anaishi wapi?”

“Anaishi wapi kivipi?”

“Huyo jamaa yako anaishi wapi hapa jijini Dar es Salaam?”

Kwangu.”

Roi alitoka kitandani, akasimama akihema kwa kasi...

“Martha acha mambo ya utani bwana.”

“Sina utani, anaishi na mimi pale.”

“Mh! Kumbe una mume Martha?”

“Ndiyo Roi. Ndiyo maana uliponiuliza nina mchumba nikakwambia sina kwa sababu nina mume. Sikutaka kukwambia siku za kwanza kwa sababu zangu binafsi.”

“Sababu kama zipi?”

“Nazijua mwenyewe, iko siku nitakwambia.”

“Kama ni hivyo Martha please tuendelee kuwa kaka na dada kuanzia sasa hivi tunavyoongea, mimi si mpenzi wako tena na wala wewe si mpenzi wangu tena.”

“Noo! Roi noo! Mimi bado nakuhitaji wewe kama mpenzi wangu. Ukaka na udada ulishakufa, we unajua.”

“Martha…” aliita Roi.

“Abee…”

“Katika vitu sivitaki katika maisha yangu ni kutembea na mke wa mtu. Sitaki wala sipendi na sitamani. Kwangu mke wa mtu ni sumu kama sumu nyinginezo. Yaani wewe saa hizi ninapokuangalia nakuona kama ile sumu ya kuulia panya,” alisema Roi akiwa amekunja sura.

“He! Hayo yote yanatokana na nini mpenzi wangu jamani?”

“We unajua. Kumbe una mume wako halafu unatembea na mimi! We ni msaliti.”

Martha alimlalia mapajani Roi na kuanza kulia tena kile kilio cha kwikwi.

“Unalia nini sasa?” aliuliza Roi mikono ikiwa juu kwa maana kwamba hakuwa anataka kumshika Martha.

“Baby,” aliita Martha kwa sauti tamu sana…

“Nini?”

“Kuna kitu nilitaka kujifunza kwako.”

“Kipi?”

“Niliamua kukudanganya ili nione kama utakubali kuendelea kuwa na mimi au la! Inaonekana wewe ni mwanaume mwaminifu, usiyetaka kuchanganya. Nimefurahi sana,” alisema Martha…

“Martha we mwongo. Unajifanya ulikuwa unanidanganya kwa vile nimekuonesha msimamo wangu siyo? We si mkweli.”

“Baby, unataka nifanyeje ili uamini?”

“Mimi sijui ufanyeje! Wewe ndiyo unajua ufanyeje!”

“Twende ukalale kwangu leo,” alisema Martha huku akimwangalia Roi kwa kutokea chini.

Sasa Roi alishalegeza masharti. Alimshika mwilini Martha huku akimpapasapapasa sehemu mbalimbali. Mara kifuani, mara tumboni, mara kwenye nido.

“Pengine mumeo kasafiri.”

“Utawauliza wale wanawake.”

“Ah! Si utawaambia hata kwa simu kwamba nikiwauliza wajibu nini!”

“Basi twende kwako nikalale huko.”

“Sitaki. Si utamdanganya mumeo kwamba umekwenda kumsalimia shangazi yako.”

“Jamani baby! Sasa nifanyeje ili uamini nilikuwa nakudanganya?”

“Mimi sijui Martha.”

“Haya! Sikia, basi twende kwako, chukua nguo, twende kwangu. Ukae pale hata kwa siku kadhaa hivi.”

“Sawa. Twende.”

Roi na Martha waliondoka mpaka nyumbani kwa Roi. Ilikuwa mara ya kwanza, Martha kuingia kwenye nyumba hiyo, akapongeza kwa jinsi ilivyo.

Roi alibeba nguo za kubadili kwa siku tano, aliamini ndani ya siku hizo. Atajua ukweli kwa kuchunguza mambo kadhaa.

Walianza safari hadi nyumbani kwa Martha…

“Hilo duka lina mlinzi baby, kwa hiyo gari laza hapahapa nje,” alisema Martha. Mbele ya nyumba anayoishi kuna barabara, ng’ambo yake kuna duka.

Ilikuwa ni dalili ya kwanza kwa Roi kuthibitisha kwamba, kweli Martha hana mume…

“Angekuwa ana mume, asingetaka gari lilale jirani hivi,” alisema moyoni huku akifunga milango.

Nje ya nyumba, walikaa wale wapangaji wenzake, Martha. Walipomwona Roi walimchangamkia sana…

“Karibu kaka…mzima wewe? Za siku jamani?”

“Njema…njema…njema sana,” Roi aliwaitikia wote kwa kuunganisha maneno.

Walipoingia ndani, nyuma maneno yakaanza…

“Jamani, mbona kaja na begi? Ndiyo kahamia nini?”

“Inawezekana. Lakini jamani twende mbele na kurudi nyuma, Martha si mwanamke machepele,” alisema mmoja wa wapangaji hao.

“Ni kweli. Ila aliwahi kuwa na kizee kimoja hivi, sijakiona muda, nadhani walizinguana,” alisema mwingine.

Wapangaji hao walimchambua Martha mpaka wakafika kwa Roi, kwamba kwa nini anamtambulisha kama kaka yake wakati ni mpenzi wake?

“Kile kizee alikitambulisha kuwa ni mpenzi wake, sasa huyu kijana mwenzake kwa nini anasema ni kaka yake?” aliuliza mpangaji mmoja.

“Ukiona hivyo ujue ni mume wa mtu. Kile kizee si kilifiwaga na mke, ndiyo maana alikiweka wazi,” alisema mpangaji mwingine. Mpangaji wa tatu akatahadharisha kuwa, Martha anatoka baada ya kusikia kutembea kwake…

“Anakuja jamani… anakuja! Nyamazeni.”

Martha alitoka na Roi, wakasimama…

“Jamani! Huyu bro wangu atakuwa hapa kwangu kwa siku kadhaa. Kwa hiyo msishangae mkimwona anaingia na kutoka,” alisema Martha kwa sauti ya kujiamini sana kisha akamshika mkono Roi na kurudi naye ndani huku wale wapangaji wakisema…

“Sawa, karibu bro. Hakuna shida.”

Nyuma, walianza tena wale wapangaji…

“Jamani…Martha si ana chumba kimoja tu?”

“Ndiyo.”

“Sasa kaka yake atamlaza wapi?”

“Si anatuvunga tu.”

“Sasa mimi nitamkomesha,” alisema mpangaji mmoja.

“Utamkomeshaje?”

“Nitachukua namba yake ya simu halafu nitaanza kujigonga kwake.”

***

Ulikuwa ni usiku wa kwanza kwa Martha na Roi kulala pamoja wakiwa wamefuta ukaka na udada wao.

Martha ndiye aliyekuwa mchokozi pale kitandani. Alimshikashika Roi kwa kuanzia kichwani, akaja kifuani, akampa kidole chake kwenye kinywa, Roi akakipokea, akamlalia kifuani huku akianza kuhema kwa staili ya mahaba.

Mara, mlango mkubwa wa kuingilia sebuleni uligongwa…

“Mh! Martha! Si jamaa yako huyo kweli?”

Ilipita kama dakika tatu hakuna aliyekuwa akizungumza zaidi ya kuendelea kushikana kiaina. Kilichosikika ni kuhema kwa mama Anna ambaye sasa alionekana kama tayari amechaji.

Roi alimsimamisha, akamshika mkono na kuondoka naye…

“Tunakwenda wapi sasa?” aliuliza mama Anna.

“Wewe twende tu, wala usiogope,” alisema Roi, tayari akili yake ilikwishahama kabisa, kwa kumwangalia tu, ingekufanya ujue tayari penzi lilimchukua.

JIACHIE MWENYEWE SASA…

Safari yao ilikwenda mpaka kwenye gari la Roi, mama Anna akapanda upande wa abiria, Roi akakalia usukani na kuanza mwendo mpaka nyumbani kwa Roi.

“Karibu sana, hapa ndiyo nyumbani kwangu,” alisema Roi na kumshangaza sana mama Anna…

“He! Kumbe! Nyumba nzuri sana.

Sasa kwa nini unakuja kuishi kule ambako Martha amejibana?”

“Haitakuwa kila siku. Lakini tukubaliane jambo moja. Nimekuleta hapa, iwe siri yako wewe, sawa?” alisema Roi akiwa amesimama na mama Anna sebuleni.

“Yaani elewa mimi ni msiri sana kama nilivyokwambia, kwa hiyo wala usiwe na wasiwasi wowote ule.”

Roi alimpeleka chumbani mama Anna…

“Hiki ndiyo chumba changu ninacholala,” Roi aliendelea kutambulisha…

“Jamani! Umebakiza kuwa na mwanamke tu! Hivi, utaoa lini wewe mwanaume?”

“Nitaoa karibuni.”

“Ndiyo Martha sasa?”

“Hata Martha wewe kwani pia si Martha?” alisema Roi huku akicheka kuashiria kwamba, alikuwa kwenye utani.

Moyoni mama Anna alinuia jambo moja. Kwamba, watakapopanda kitandani kuanza mechi, aoneshe ufundi wote, chenga kwa wingi, danadana kwa sana ili ikibidi yeye sasa, amkamate kimapenzi Roi na kumpiku wajina wake, Martha…

“Jamani, mimi bahati hiyo nitaipata kweli?” alisema mama Anna akiwa na yake moyoni.

Ni Roi ndiye aliyemuanza mama Anna mle chumbani. Alimshika, akamvutia kwake, wakakaa wote kitandani. Alikaa Roi, mama Anna akaja juu yake. Alimkalia Roi...

“Teh! Teh! Lakini mi mwenzako naona aibu,” alisema mama Anna huku akiuma kidole chake.

“Aibu ya nini bwana wewe? Kwanza lazima ujue mimi naweza kuwa mumeo. Sasa mumeo utamuoneaje aibu?” alisema Roi, lakini moyoni alisema…

“Ungekuwa una aibu ungeanza wewe kunitongoza? Acha mambo yako wewe.”

Roi, ili kumtoa mwanamke huyo hiyo aibu, alimshika shingo, akamgeuzia kwake, akaomba denda, akapewa. Wakapeana, wakazama kwenye mahaba mazito.

Alichofanya mama Anna, wakati wapo katikati ya denda, alipeleka mkono kwenye kifua cha Roi na kuanza kumfungua vifungo vya shati, kimoja baada ya kingine mpaka mwisho.

Akalitoa shati pembeni, akalitupa kwenye kiti. Akahamia kwenye singilendi, akaivua mpaka usawa wa midomo, akatoa ulimi na kuivua singilendi kisha akarudisha ulimi tena.

Alipoitupa singilendi, Roi alikuwa tumbo wazi, akajua mambo yameisha, kumbe mama Anna alikuwa bado. Wakiwa ndani ya denda, akapeleka mkono kwenye suruali, akashika sehemu ya kufungia usalama wa suruali na kupafungua, akaishusha suruali huku denda likiwa palepale.

Ilifika mahali, mama Anna akatumia miguu kuimalizia suruali kwa chini, ikatoka kwenye miguu ya Roi, akabaki na boksa.

Kwa Roi, aliyokuwa akifanyiwa na mama Anna yalikuwa mageni kwake. Hakuwahi kuyaona popote, hata kwa Martha mpenzi wake. Yaani denda liwepo mdomoni huku anavuliwa nguo? Kwake ilikuwa elimu mpyaa!

Mama Anna akapeleka mkono kwenye boksa, akaivuta, ikavutika. Akaitoa na mkono mpaka usawa wa magoti, akaisindikiza chini kwa miguu na kuimalizia, ikatoka na kuangukia kwenye kapeti.

Sasa Roi alikuwa kama alivyozaliwa huku mama Anna naye akianza kujiondoa vazi moja baada ya jingine mpaka wakawa saresare.Waliingia uwanjani huku mama Anna akipania ushindi wa kishindo. Roi yeye alitegemea kuyaona mengi zaidi. Na kweli.

Mama Anna alijilaza kuangalia miguuni kwa Roi mpaka Roi akashangaa. Alishangaa kwa sababu alihisi mwanamke huyo hakuwa tayari kwa mchezo zaidi ya kupandishana joto la mahaba tu.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni