JAMANI DADA MARTHA... LOOO! (12)
Jina: JAMANI DADA MARTHA... LOOO! Mtunzi: 2jiachie SEHEMU YA KUMI NA MBILI ILIPOISHIA... Waliingia ndani watatu, wale wapangaji wawili na Martha . Mama Anna aliwakaribisha kwa mbwembwe akijifanya mama mwenye nyumba huku Roi akionekana kukosa amani... JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Karibuni jamani...karibuni sana,” alikaribisha mama Anna kwa sauti ya ‘mimi ndiye mmiliki halali wa mwanaume huyu’, yaani Roi sasa. “Tunashukuru sana,” waliitikia wale wapangaji wawili kasoro Martha ambaye yeye alifikia kuweka begi chini kisha akamwambia Roi... “Ungeangalia kama nguo zako zote zipo maana nimehakikisha siachi nguo yako hata moja.” “Naamini zote zipo bila hata ya kuhakikisha,” alisema Roi kwa sauti iliyojaa dharau, mkono mmoja ulipita kiunoni kwa mama Anna huku mkono mwingine ukishughulika na rimoti ya televisheni. Bila kukaa, Martha akageuza kutoka lakini kabla hajafika mlangoni, ikasikika hodi... “Hodi,” hodi hiyo…