MWAJUMA UTAMU (3)
Jina: MWAJUMA UTAMU Mtunzi: Juma Hiza SEHEMU YA TATU ILIPOISHIA... Kimuonekano alikuwa ni kijana mtanashati, kiukweli nilitokea kumpenda kwa moyo wangu wote. Kipindi nipo katika mahusiano naye nilisahau shida na matatizo yote niliyokutana nayo katika maisha yangu, JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... sikutaka kukumbuka kitu chochote kilichotokea nyuma. Oscar alinipenda sana, ahadi zake za kunioa ndizo zilizonifanya nikazidi kumuamini mara dufu, bila kujali nikamkabidhi mwili wangu ambao aliutumia autakavyo. Maisha yalibadilika kwa kiasi fulani, nilikuwa nikiishi maisha yenye furaha, Oscar aliendelea kunijali, alinipa matunzo pamoja na mapenzi moto moto. Kiukweli wazo la kurudi nyumbani kichwani mwangu halikuwepo kabisa kwa wakati huo, niliona ni jambo gumu mno kurudi katika maisha ya kimasikini niliyozaliwa katika familia yetu. Nilikuwa nikiishi maisha ya furaha yaliyogubikwa na amani tele, sasa kwanini nikumb…