MWAJUMA UTAMU (7)
Jina: MWAJUMA UTAMU Mtunzi: Juma Hiza SEHEMU YA SABA ILIPOISHIA... “Usiuzungumzie moyo wangu Suzie, nimeshakwambia kuwa simpendi Martin mbona hunielewi na sioni sababu ya kuolewa naye.” JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... “Mwajuma unajua unaichezea bahati, wasichana wengi wanaitafuta bahati hiyo wanaikosa halafu wewe unaipata lakini unaichezea.” “Suzie hivi hakuna stori zingine za kuzungumza?” “Utakuja kuijutia bahati hii unayoichezea.” “Sidhani kama kuna siku nitakuja kuijutia, kwanza hilo haliwezi kutokea halafu nimekumbuka baadae ninatakiwa nikameet na Damian.” “Who is Damian?” (Damian ndiyo nani?) “Mpenzi wangu, mume wangu mtarajiwa,” nilimjibu. Suzie alibaki akinishangaa baada ya kumwambia nilikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine aliyejulikana kwa jina la Damian. Hii ilionyesha picha ya umalaya, yaani sikutulia na mwanaume mmoja, maisha yangu yalikuwa ni ya kudangadanga leo nilikuwa kwa m…