
Mtunzi: Hassan S. Kajia
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
“Chanzo cha yote haya ni huyu mpumbavu mwenzako….wote leo mtakufa. Namkumbuka sana. Alimlaghai mtu wangu ili kujua mambo yangu…sasa atayajulia aghera.”
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
John na Max walijuana baada ya Max kusikia kwamba Aminata ameolewa na John. Yeye alikuwa kwenye mafunzo Urusi na hivyo hakuweza kuhudhuria wala hakujua lolote. Aliukumbuka tu urafiki wake na Aminata wakiwa pamoja chuo.
Alipotezea hata lile lengo lake la siku moja kumwambia Aminata kwamba anampenda. Sasa aliamua kuacha mambo ya livyo. Aliamua kuwa karibu nao kwani kazi aliyopewa ilikuwa inawahusu wote na hivyo iliwalazimu kujuana.
Baada ya kurudi walikuwa wakiwasiliana na hapo John alipata kumfahamu na kujua alilokuwa akifanya. Ukaribu wao ulimpa nafasi John kujiingiza katika masuala ya upelelezi hasa baada ya kushawishiwa sana na mke wake Aminata. Aliaanza kujifunza masuala ya jeshi na baadaye alihamia kwenye upelelezi. Alitumia muda mfupi kutokana na kufahamiana na wakufunzi ambao walimfananisha na Antony ambaye aliwahi pia kupitia jeshi. Pia Aminata alimsaidia katika kujua mafunzo ya upelelezi.
Katika jumba la Steve John sasa hakuwa na lakufanya zaidi ya kusubiri kama ataweza kujiokoa mwenyewe. Aliona kweli itakuwa vigumu sana kuokoka katika mikono ya wahuni wale lakini akaapa kwamba lazima atajitahidi kujiokoa. Alijua wakiweza kuchukua silaha zao yeye na Aminata wataweza kujikwamua kutoka kwao.
Alikwisha tambua kwamba genge lile lilikuwa ndiyo lile lililokuwa linasakwa na Serikali na hivyo kutokana na kwamba John alikuwa mmoja wa aliotumwa kulifuatilia alijua itakuwa genge hilo limejua azma ya Serikali juu yao na hivyo kutaka kukomesha matakwa ya Serikali. Alifikiria kama ataweza kuwasiliana na Max lakini hakuona njia yoyote.
Hakuwahi kufika sehemu ambayo alipelekwa na wala hakujua yuko wapi kwa wakati huo hivyo alihofia pia iwapo akijaribu kujiokoa atapita wapi kurudi kule alikokuwepo awali.
*****
Max amekuwa mpelelezi wa Serikali kwa kipindi kirefu na amekuwa akiaminiwa na Serikali juu ya majasusi na maharamia wa nchi ambayo wanataka kuipeleka nchi pabaya. Wauaji na wadhalimu wa mali za walio wengi kwa kutumia mabavu aliweza kuwadhibiti vilivyo kwa kutumia mbinu za kiintelejensia.
Hakupenda udhalimu wala manyanyaso ya watu wachache dhidi ya raia wasio na hatia.
Alifurahi kuwa karibu na John pamoja na Aminata. Kazi walizofanya pamoja za kupambana na uhalifu ziliwafany wawe ni watu walioheshimika sana. hata viongozi wan chi waliwajua kwamba waliweza kazi ingawa kulikuwa na matatizo ambayo yalipelekea wafanye kazi kwa ugumu.
Moja ya kazi ambazo walipewa ni ya kufichua wapi zilipokuwa almasi na kuwashikilia wahusika. Almasi hizo zilikuwa zimefichwa katika kitongoji cha Kigamboni Dar es Salaam.
Hilo lilifanikiwa kwa hali ngumu kwani walikumbana na mashambulizi ya hatari ambayo yalipelekea Max kuvunjika mkono. Mazx aliipenda kazi yake na hivyo baada ya kupona mkono wake aliamua kurudi na kuendelea na kzi hiyo.
Habari za kutoweka kwa John zilitawala kila kona, watu waliweka makundi kujadili juu ya habari hizo. Max naye alizipata habari hizo. Alijua lazima na Aminata atakuwa na John kwani mara nyingi walitoka pamoja hasa wikiendi.
Alijua sasa lazima afanye awezalo ili awasake walipopelekwa. Hakujua juu ya jumba la Steve.
Ndani ya jengo la Steve, Mosses Ndula na Bosi Steve wakati wote walikuwa wakitaka kujua ni kwa nini Serikali inataka kuwafatilia, hivyo waliendelea kumhoji John wakati wote. John alionyesha ujasiri mkubwa kwa kutokuonyesha ushirikiano wowote kwao.
Alipewa adhabu mbalimbali ili aweze kusema lakini hakuwaeleza jambo lolote kuhusiana na Serikali akidai kwamba yeye hakufahamu jambo lolote na hivyo wanamwonea tu.
“Mna uhakika gani kama mimi nimetumwa na Serikali kuja kuwachunguza, kwani ni katika mazingira gani ambayo mmenikamata?”
“Wewe unataka kutuambia hii picha hapa siyo wewe, au tumeifananisha hiyo sura?” Mosses Ndula alimfokea huku akimkaba John shingoni. Alimwonyesha picha ambayo alikuwa na Aminata wakimpongeza baada ya kuhitimu mafunzo ya upelelezi. John alishangaa sana.
“Kama mlinikosa mwanzo…..sahauni kuhusu kunipata.”
“Mimi sina shida na wewe kama unavyofikiria.”
“Sasa mbona unawachelewesha….fanya kama tulivyokubaliana bwana Mosses. Muda unakwenda,” Bosi Steve alitoa kauli hiyo baada ya kuona hakuna ushirikiano wowote ulioonyeshwa na John na Aminata.
Moses alkuwa akiwaangalia kwa hasira wote wawili, alishindilia mdomo wa bastola aliyokuwa ameishika juu ya kichwa cha John huku akimkaba shingo kwa nyuma. Hasira zilikuwa zimempanda sana.
“Leo safari yako ya kuzimu imetimia, lazima ufe ili tuweze kuzima hizo janja zenu za kutaka kutudhibiti, nataka nikuambie kwamba leo wewe na huyo malaya wako mtaongozana kwenda kuzimu kisha itafuata hiyo Serikali yenu. Bosi Steve alimwamuru Mosses Ndula awaarifu vikosi vya mauaji kutekeleza tukio hilo mara moja.
Mosses Ndula bila ya kuchelewa aliwaamuru kikosi cha mauaji kufanya kile Bosi Steve alichotaka.
“Wapelekeni nje ya mji karibu na pori dogo na kisha baada ya kuwaua muache miili yao katikati ya barabara. Aliwaamuru wafanye hivyo wakihakikisha kwamba hakuna mtu yeyote atakayewaona wala kuwadhani wakati watakapokuwa wameshafanikisha tukio hilo.
Bosi Steve na Mosses Ndula walibariki mauaji hayo na kisha kuwaaga askari wa kikosi cha “MALIZA KAZI” ambao ndiyo waliopewa dhamana ya kutekeleza adhabu ya kifo. Walikuwa ni askari watatu waliowachukua John na Aminata mpaka eneo waliloagizwa.
Wakiwa njiani hali ilikuwa ni shwari kwani hakusikika kiumbe wa aina yeyote aliyelia wakati huo, wakiwa wanatoka waliwafunga vitambaa usoni ili wasitambue walikokuwepo na wanakokwenda, iliwachukua takriban dakika arobaini kufika. Waliwashusha kutoka kwenye gari aina ya MARK II nyeusi na kuwavua vitambaa ambavyo waliwafunga ili wasiweze kutambua eneo waliloko.
John alitumia ujasiri wake kutaka kuwalaghai askari wale ambao walikuwa watatu. Aliomba afunguliwe mikono ili aweze kuongea mara ya mwisho na Aminata kisha atakuwa tayari kufa.
Kwa vile askari wale walikuwa wameshika silaha za moto hawakuhofia jambo lolote ambalo John angeweza kusababisha kwani hakuwa na silaha ya aina yoyote wakati huo. Walimfungua John na Aminata kamba walizokuwa wamewafunga mikononi kisha kuwasogeza kando ili waweze kuzungumza maneno ya mwisho kabla ya kifo chao.
“Usijali Aminata niko kwa ajili yako, hakuna baya litakalokukuta usiku huu, kumbuka kwamba tuko wawili na nina imani kwamba tutashinda. Nakupenda sana Aminata,” alimalizia John huku amemshika Aminata mikono.
“Najua unanipenda sana John lakini hadi sasa sioni kama tutasalimika na unaona wamebeba silaha wakati wewe huna hata moja, sijutii kuwa na wewe John hii ni kazi yetu wote, sijui mtoto wetu ataishije bila ya wazizi wake. Najua atapata tabu sana lakini Antony yupo, atakaa na baba mdogo wake. Kwa kuwa nakupenda nitakufuata huko huko kuzi….
Kabla hajamalizia neno alilokuwa anamwanbia John, John aligeuka na ngumi nzito na kumtupia askari aliyekuwa karibu yao akiwasubiri wamalize kuzungumza. Askari yule alianguka chini na kuzirai na mara moja John aliiwahi silaha yake na kuwamiminia risasi askari wawili waliobaki. John alipata nguvu za kukimbia pamoja na Aminata. Aminata hakuamini macho yake. John alikuwa amemkabidhi Aminata silaha moja kati ya tatu na yeye akabakiwa na mbili. Walipita njia za vichaka hadi walipoona eneo lililokuwa na mwanga.
Zilikuwa zimepita saa takriban tatu bila ya jibu lolote toka kwa askari wa Mosses Ndula kuhusiana na kifo cha John. Wala hawakuona dalili za askari hao kurudi mapema. Ilibidi watumwe askari wengine wawili kufuatilia juu ya kinachoendelea. Gari la askari waliotumwa lilifika eneo la tukio saa tano na nusu usiku na kushuhudia damu nyingi ikiwa imemwagika.
Waliona askari wao wakiwa wamelala chini wakiwa hawana hata silaha moja. Walishangaa kuona walikuwa wawili wakati kambini waliondoka watatu. Mara wakasikia sauti ya askari ikilia kwa maumivu makali. Walimfuata na kumbeba na kumwingiza kwenye gari.
Waliwachukua wale maiti wawili na kuwapakia kwenye gari na kuondoka nao kurudi kambini kwani walijua isingekuwa rahisi kwa wao kuwatafuta John na Aminata wakati huo kwani lazima watakuwa wamejificha mbali sana, hivyo waliona ni bora wakatoe taarifa juu ya kilichotokea.
Waliwafikisha wale maiti pamoja na yule askari mwingine majeruhi kwa wakuu wao. Bosi Steve alikasirika sana kusikia kwamba John na Aminata walitoroka baada ya kuwashinda askari wake nguvu. Alimmiminia askari aliyebaki risasi na kumuua.
“Wafuate wenzako mshenzi mkubwa wewe,” alifanya tukio hilo la mauaji kwa askari yule akiwa na hasira sana. Askari wengine waliokuwepo eneo lile walipata woga wakijua kwamba wanaweza wakauawa.
”Nataka John na Aminata warudishe hapa haraka sana,” alifoka Bosi Steve.
Mosses Ndula aliwaamuru askari wavae nguo za kiraia ili waingie katika msako wa kuwatafuta John na Aminata kabla habari hazijazagaa juu ya kutekwa kwao na kutoroka.
Wakati huo John na Aminata walikuwa wamepata sehemu ya kulala na kupumzika ambapo walijua hakuna mtu yeyote ambaye angeweza kutambua sehemu waliko. Walikuwa katika hoteli ya MIDLAND.
Aminata hakuamini kwamba wamepona wakati wote alikuwa anafurahi wakati John yeye alikuwa akitafakari hatari atakayokumbana nayo hapo mbele.
“Vipi John mbona unaonekana una mawazo mpenzi, sijui hata nikushukuru vipi mpenzi wangu kwa ushujaa uliouonyesha na kupelekea kupona kifo kile, nilijua ni lazima wangetuua mpenzi. Nakupenda sana jasiri na shujaa wangu,” Aminata alimkumbatia John kwa nguvu huku akimtupia mabusu motomoto ambayo wakati huo John hakuwa katika hisia hizo kama alizokuwa nazo Aminata.
Aminata alishanga kitendo cha John kubaki akimwangalia tuu asijue la kufanya. Wakati huo John alikuwa katika hali ya majeraha makubwa yaliyosababishwa na kichapo kikali alichopata toka kwa Bosi Steve na Mosses Ndula.
Aminata kuona hivyo mara mija alimtoa John shati alilokuwa amevaa na kuanza kumfuta damu na kuuguza majeraha aliyokuwa nayo japo kuwa nay eye alikuwa akiugulia maumivu aliyoyapata baada ya kupigwa na Steve hadi kuzirai.
Ni furaha ndiyo iliyommaliza maumivu. Alijihisi mwenye nguvu huku akimhudumia mume wake tayari kwa kumweka sawa.
“Nadhani maisha yetu yapo hatarini zaidi kuliko hatari tuliyokutana nayo.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi