HATI FEKI (12)

Zephiline F Ezekiel
Jina: HATI FEKI

SEHEMU YA KUMI NA MBILI
ILIPOISHIA...
Ni furaha ndiyo iliyommaliza maumivu. Alijihisi mwenye nguvu huku akimhudumia mume wake tayari kwa kumweka sawa.

“Nadhani maisha yetu yapo hatarini zaidi kuliko hatari tuliyokutana nayo.

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
Hawa jamaa lazima watutafute hivyo Aminata naomba uwe makini sana na tena ikiwezekana usikae mbali na mim,” John alimwambia Aminata ambaye kwa wakati huo alikuwa akimfuta John damu iliyoenea mwilini na kumuuguza majeraha aliyoyapata.

“Najua John, siko tayari kufa. Ntapambana kama tulivyopambana. Sijasahau kabisa mapambano. silaha tayari tunazo. Tutaweza tu. Huyu Mosses nadhani hatujui… haifai tukamkawiza. Tujipangeni twende.”

”Nakupenda sana Aminata,” alirudia tena John maneno yale yale aliyomwambia Aminata wakati wote, ila safari hii ilikuwa ni kumdhibitishia kwamba yuko tayari kufa kwa ajili yake. Aminata alilia kwa uchungu baada ya kukumbuka kwamba walinusurika kifo pamoja, alimvamia John na kumkumbatia kwa nguvu zote huku akimpa mabusu motomoto yaliyomfanya John asahau hata maumivu ya majeraha aliyokuwa nayo.

Mlango uligongwa ghafla wote wakashtuka. John alificha silaha nyuma na kuelekea mlangoni. Aminata hakujua la kufanya zaidi ya kusubiria kitakachotokea. Alikuwa tayari kashasimama karibu na silaha ingawa hakuichukua. Alikuwa ni mhudumu wa hoteli aliyegonga ili awaulize jambo.

“Hodi kaka yangu, samahani kwa usumbufu, je mngehitaji chakula?” John aliyekuwa amebeba silaha alirudi nyuma na kuiachilia silaha juu ya kiti jambo ambalo haikuwa rahisi kwa yule mhudumu kugundua ni kitu gani. John alimuuliza Aminata kwamba angependelea chakula gani.

“Chochote utakachokula mpenzi mimi nitakula.” Aminata alijaribu kumwonyesha John mapenzi ya dhati ilimradi amfurahishe na ajue wazi kwamba anampenda sana. John alimwomba mhudumu awaletee wali na nyama choma pamoja na glass mbili za juice ya Passion. Baada ya dakika kama tano, mhudumu alikuwa amesharejea na alichoagizwa na John.

Hawakuwa na hela ya kulipia na hivyo John alimkumbuka Max. alitaka amtaarifu aje mahala walipo ikiwa ni pamoja na pesa ya kulipia chumba pamoja na chakula.

“Aminata, nahitaji kupiga simu kwa Max haraka iwezekanavyo kesho nikutane naye ili tujue la kufanya, hawa washenzi lazima tuwaangamize hata kama wanajeshi la watu milioni kumi,” John alimtaarifu Aminata juu ya alichofikiria.

“Bila hivyo Aminata sisi tutakufa na ujue kwamba hapa tulipo tupo kazini kwa hiyo kuwaangamiza hao washenzi itakuwa ni sehemu ya kazi yetu. Sitakubali walete madhara kwa wengine kama walivyotaka kuleta kwetu. Nitahakikisha kwamba wanaangamia wote,” John alizidi kuongea kwa hasira. Alimkumbuka Mosses na Syteve. Alijiapiza ni lazima awamalize.

“Sikiliza John, inabidi tutulie kwanza ili tuweze kuwatafuta wenzatu tujadiliane juu ya hilo suala lakini si kwenda mbio hivyo. Na isitoshe wale inaonekana ni hatari zaidi wanaweza wakatudhuru mpenzi. Mi nna imani akiongezeka Max na Antony tutawamaliza,” Aminata alimsihi John.

Najua Aminata lakini lazima tuanze hili jambo mapema kabla hawajagundua mipango mingine hivyo ni lazima nikutane na Max mara moja ili tujue tutawafanyaje,” John alimhakikishia Aminata juu ya hilo.

“Sawa mpenzi lakini nahofia sana maisha yetu, na mi sitakuacha tutaenda wote kila mahali ukifa na mimi nife hapo hapo,” Aminata alimfariji John.

“Aminata, nimekumbuka kitu,” alisema John.

“Kitu gani tena mpenzi?” Aminata aliuliza.

“Mi naona ungeliacha hili suala kwetu sisi. Sitaki mtoto wetu apate shida ya kuwa bila ya wazazi. Nakuomba usiende. Tuachie mimi na Max. Najua tutaweza,” John alijaribu kumshawishi Aminata ili asijihusishe na mpambano ambao alitaka kufanya na Max na Antony bila ya kuwashirikisha wengine.

NAJUA Aminata lakini lazima tuanze hili jambo mapema kabla hawajagundua mipango mingine hivyo ni lazima nikutane na Max mara moja ili tujue tutawafanyaje,” John alimhakikishia Aminata juu ya hilo.

“Sawa mpenzi lakini nahofia sana maisha yetu, na mi sitakuacha tutaenda wote kila mahali ukifa na mimi nife hapo hapo,” Aminata alimfariji John.

“Aminata, nimekumbuka kitu,” alisema John.

“Kitu gani tena mpenzi?” Aminata aliuliza.

“Mi naona ungeliacha hili suala kwetu sisi. Sitaki mtoto wetu apate shida ya kuwa bila ya wazazi. Nakuomba usiende. Tuachie mimi na Max. Najua tutaweza,” John alijaribu kumshawishi Aminata ili asijihusishe na mpambano ambao alitaka kufanya na Max na Antony bila ya kuwashirikisha wengine.

“Siwezi John, sitakaa kwa hofu juu yako, isitoshe huu mpango ni wa kwetu pia. Unakumbuka ni Mosses pia aliyewaua wazazi wangu na ndugu zangu? Mi sitaweza John. Isitoshe nna hasira sana na huyo Mosses. Najua hajui alilolifanya kwa wazazi wangu limeniuma kiasi gani. Sitakubali nimwone akiendelea kutanua wakati mi nna hasira na maumivu moyoni. Lazima nipambane nao. Bora nife na hata ukinkatalia John.”

“Lakini Aminata, huoni tukipotea wote mtoto atapata shida?”

“Kweli John lakini mi sitaweza kukaa mwenyewe kusubiri kama hutaki kwenda na mimi nitakufuata,” Aminata alimkaripia John kumzuia asijaribu kumwacha kila aendapo.

“Aminata unajua kwamba hili sio jambo la kufanyia mzaha? Wewe unajua tuna mtoto, mimi nikifa unadhani ataishije maisha ya kuwakosa baba na mama? Mimi najua nitaweza pamoja na Max na Antony. Naomba nikuwakilishe maana jambo hapa ni kummaliza Mosses.”

“John kwani hata nisipoenda maisha yangu yatakuwa hatarini kwa vile wameshajua mimi ni mke wako, hivyo popote watakaponiona watataka kunikamata,” Aminata alimwambia John.

“Ila sitakuwa na wewe, nitakupa ramani ya kila tunapokwenda ili kama tukizidiwa utusaidie. Sawa mpenzi.”

“Sawa mpenzi.”

Saa nane na nusu usiku wote walikuwa wamekwisha lala. Asubuhi John alikuwa ndiye wa kwanza kuamka na kwenda moja kwa moja hadi sehemu ya mapokezi kwa lengo la kupiga simu. Alitaka kuwasiliana na Max. alitaka kumjulisha kule walipo ili aweze kuwafuata na gari.

Simu iliitikiwa na Max ambaye alionekana kushtuliwa toka usingizini pasipo kuamini kwamba aliyempigia alikuwa ni John.

“Haloo Max mimi John, njoo mshikaji wangu, hapa Mainland Hotel mida hii niko na Aminata. Siko fresh mshikaji wangu njoo na nguo za kubadilisha, mwambie shemeji aje na nguo amsaidie Aminata tuweze kutoka hapa. Tafadhali naomba usimjulishe mtu yeyote juu ya hili ila we njoo mengine nitakuambia tukishafika kwako. Naomba pia uje na pesa ya kulipia tupo gesti na chakula,” wakati huo Max yeye alikuwa akimsikiliza John kwa makini zaidi ili ajue nini cha kufanya.

“Sawa kaka nimekupata, nipe muda kidogo nitakuwa hapo na shemeji,” Max alifanya kama alivyotakiwa, alimwambia kila alichosikia Michelle ambaye alipatwa na woga. Waliharakisha asubuhi hiyohiyo mapema na kuwafuata walipo.

Walikuwa wamepaki gari nje ya Mainland Hotel tayari kumchukua John na Aminata. Alifika pamoja na Michelle ambaye walikaa pamoja kwa kipindi kirefu bila ya kufunga ndoa.

Michelle alitoka na mzigo wa nguo katika begi na kufuatana na Max mpaka ndani sehemu ya mapokezi, waliulizia na kuruhusiwa kuingia. John na Aminata walikuwa wako chumba namba 143.

Max na Michelle waligonga na kufunguliwa na John.

“Haa! John ni nini nkilichokusibu hivyo shemeji yangu?” Michelle ndiye aliyekuwa wa kwanza kuhoji mara tu baada ya kuingia ndani.

“Karibuni, Max na Shemeji Michelle, is a long story my friends naomba kwanza tuondoke hapa nitawapa kisa kizima huko kwako. Nadhani umekuja na ule mzigo niliokuagiza Max?” alihoji John baada ya kuwaomba wakazungumzie jambo hilo nyumbani.

“Bila shaka John tumekuja nao huo hapo kwa shemeji yako,”

Mishelle aliukabidhi ule mzigo wa nguo kwa John. Wakati huo Aminata alikuwa ameingia bafuni kuoga tayari kwa safari ya kurudi nyumbani. Wakati John akiwa anawakaribisha Max na Michelle.

“Aminata pole sana japo sijajua lolote ila hali halisi inaonyesha hamkuwa katika hali yenye ushwari,” aliamka Max kutoka katika kiti alichokuwa amekaa kumsalimia Aminata.

“Kwani John hajawaelezea yaliyotokea shemeji?” alihoji Aminata.

“We mjeshi gani unataitiwa,” Max aliyemfahamu vizuri Aminata alimtania.

“We acha tu Max, hali ilivyokuwa si mchezo. Kwani hujaelezewa bado na John.

“Hapana Aminata ila ameahidi kutusimulia pindi tutakapofika nyumbani kwangu,” John na Aminata walikuwa tayari wameshavaa, John alichukua kiasi cha pesa alicholetewa na Max.

Alilipia gharama zote za hoteli kuanzia malazi na chakula. Waliondoka hotelini hapo saa mbili asubuhi kuelekea nyumbani kwa Max.

Waliingia moja kwa moja hadi sebule kubwa aliyoitumia Max wakati wa mazungumzo na wageni wake. Michelle aliamka mara moja kwenda kutengeneza chai.

“Naitamani hiyo stori shemeji naombeni niweke chai kwanza ndiyo uanze kusimulia,” Michelle alimsihi shemeji yake John. John, Max na Aminata waliangua vicheko baada ya kuona Michelle akihaha kutaka stori isianze.

Baada ya dakika tano Michelle alikuwa tayari ameshaandaa chai na wote wakiwa wameshakaribishwa na kuanza kunywa.

“Haya shemeji ruksa sasa, ila samahani sana kwa kukuchelewesha japo sijui kama inanihusu mimi,” Michelle alimsihi shemeji yake John. Michelle alikuwa ni mcheshi sana na aliyependa kufurahi saa zote, alionekana ni mchangamfu wakati wote. Hiyo ndiyo sababu hasa iliyomfanya Max kuvutiwa na binti huyo ambaye kwa sura alikuwa ni mzuri wa aina yake.

“Eebwana ilikuwaje kaka mbona sielewi?” Max aliuliza kwa shauku la kutaka kujua ni nini kilichowapata John na Aminata.

“Dah! Kaka kazi yetu tunayoifanya bila ujasiri umekwisha. Tulijikuta tumezungukwa na kundi la watu. Tumepigwa hapo tukafungwa vitambaa na sijui tulipelekwa wapi,” John alisimulia kisa kizima hadi walipofanikiwa kuwaua wale askari wa Mosses na kutoroka.

Walikaa kimya kama dakika mbili huku kila mmoja akitafakari kutafta namna ilivyokuwa. John alakuwa akiwaangalia huku akiangaliana na Aminata ambaye alionekana kufurahishwa sana na uwepo wa John katika maisha yake. John alitabasamu na kuendelea.

“Isitoshe, wale jamaa kumbe wameungana tena wawili… mmoja ndo yule aliyechukua mgodi wa mzee kwa hati feki tukafanikiwa kuukomboa.”

“Si ndo wao nawafatilia kuhusu kuulipua,” Max alidakia kwani ndiyo kazi aliyopewa aitekeleze.

“Nadhani itakuwa ni wao maana wana kisa na sisi. Antony tutampata wapi wakati huu?” anatakiwa kuwa na sisi kwani kipindi kile alikuja tukafanikisha.”

“Kwani alirudi Nairobi?”

“Ndiyo, na sasa itabidi aje tena,” John alisema huku akichukua kikombe cha chai na kubwia kidogo.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni