HATI FEKI (11)
Jina: HATI FEKI Mtunzi: Hassan S. Kajia SEHEMU YA KUMI NA MOJA ILIPOISHIA... “Chanzo cha yote haya ni huyu mpumbavu mwenzako….wote leo mtakufa. Namkumbuka sana. Alimlaghai mtu wangu ili kujua mambo yangu…sasa atayajulia aghera.” Haikuwa rahisi kwa John kuweza kumjulisha rafiki yake Max aje kumwokoa. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... John na Max walijuana baada ya Max kusikia kwamba Aminata ameolewa na John. Yeye alikuwa kwenye mafunzo Urusi na hivyo hakuweza kuhudhuria wala hakujua lolote. Aliukumbuka tu urafiki wake na Aminata wakiwa pamoja chuo. Alipotezea hata lile lengo lake la siku moja kumwambia Aminata kwamba anampenda. Sasa aliamua kuacha mambo ya livyo. Aliamua kuwa karibu nao kwani kazi aliyopewa ilikuwa inawahusu wote na hivyo iliwalazimu kujuana. Baada ya kurudi walikuwa wakiwasiliana na hapo John alipata kumfahamu na kujua alilokuwa akifanya. Ukaribu wao ulimpa nafasi John kujiingiza katika ma…