
Mtunzi: Hassan S. Kajia
SEHEMU YA KUMI NA TANO
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
MAX mara moja alifika eneo la maliwato kumsubiri Steve aingie. Aliwasiliana na John ili aweze kuzuia watu kuingia eneo hilo na badala yake awashauri watumie maliwato nyingine. Wakati huo hakukuwa na watu wakiingia maliwatoni huko na hivyo ilikuwa ni nafasi nzuri ya Max na John kufanikisha mpango wao.
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
Haikuchukua muda Bosi Steve aliingia, Max alisubiri hadi amemaliza na kuchomoa bastola yake na kumnyooshea Steve. Bosi Steve alishtuka kusikia sauti ya Max ikimwambia.
“Usijiguse na simama hapo hapo kama ulivyo,” kabla ya kugeuka kumwangalia aliyetoa sauti hiyo alipigwa ngumi na kuzirai. Max aliwasiliana na John kwamba kashamteka hivyo wajitayarishe kuondoka.
Antony alifungua mlango wa gari na kulisogeza mpaka karibu na mlango wa kutokea na hivyo ilimchukua Max dakika mbili kumfikisha Steve ndani ya gari hali ya kuwa amezirai.
Walifika katika nyumba moja kuukuu iliyoko maeneo ya Mianzini wakiwa wameshamteka Bosi Steve. Nyumba hiyo haikuwa inatumiwa na mtu yeyote. Ilikuwa ni saa moja na nusu usiku.
Baada ya Steve kuzinduka John alikuwa amesimama mbele yake. Alishtuka kumwona John.
*****
Ukumbini Mosses Ndula na Askari wake walikuwa wakimtafuta Bosi Steve bila ya mafanikio. Waliamua kutoka na kuelekea nje ya ukumbi wakidhani atakuwa huko kwani hata simu yake haikupatikana. Walizunguka kila mahali nje ya hoteli wakijua labda anavuta sigara sehemu.
“Atakuwa ametekwa, hivyo wasiliana na kikosi cha anga ili kuzunguka na helikopta kujua watekaji,” Mosses Ndula alimwambia mmoja wa askarti wake ili aweze kuwasiliana na askari wa kikosi cha anga waanze kazi ya kumtafuta Bosi Steve mara moja.
Mosses alijua lazima ni John kafanya mpango huo baada ya kufanikiwa kuwatoroka askari wake.
“Huyu lazima atakuwa ni John na Aminata….Lazima tuwafuatilie,” aliwaza Mosses huku akiingia ndani ya gari.
Max alishauri wampeleke Steve kwenye vyombo vya sheria ili akadhibitiwe huko wakati wao watakapokuwa wakiendelea na zoezi zima la kuivamia ngome yake na kuiteketeza. John aliafikiana na Max na hivyo waliongozana na magari matatu ili kuhakikisha wanamfikisha salama Steve.
Wakiwa njiani kuelekea maeneo ya mjini kati waliona helikopta ikiwazunguka na kuanza kuwatupia risasi. Ni katika barabara ya Moshi Arusha ambapo kina John walikuwa wakielekea kituo cha polisi ili kumshikilia Steve.
“Max jamaa washatuona tutoke tupambane nao, naona wanataka kuzima huu mpango, ni nani kawaambia tumepitia njia hii”? aliuliza John huku akitoa bunduki yake na kuanza kushambulia helikopta ya askari wa Mosses Ndula iliyokuwa ikiwalenga kwa risasi.
Max na John walijitahidi kurudisha mashambulizi. Waliteremka askari wa Mosses Ndula kutoka katika helikopta na kuvamia gari lililokuwa limembeba Bosi Steve na hivyo kufanikiwa kuzima zoezi la kina John la kumpeleka kituo cha polisi. Walifunga barabara na kuzuia gari lililokuwa limembeba Steve. Walifanikiwa kumchukua na kuondoka naye.
“Aaah, hawa jamaa wametuziidi ujanja. Sijui imekuaje… sikutegemea itakuwa hivi isitoshe hatukubeba silaha za maana. Itabidi sasa tujipange upya,” alisema John kwa hasira huku akiiangalia ile helikopta ya Mosses ikitokomea angani.
John na Max waliamua kurudi nyumbani kwa ajili ya kujipanga upya. Walimpigia simu Antony na kumjulisha ya kwamba watakutana tena baada ya kuwa wameshapajua.
John alimpigia siu Aminata na kumjulisha ya kwamba mambo hayakuwa mazuri na hivyo wameamua kurudi nyumbani na kuanza upya mipango yao.
Katikan jumba la Steve, Mosses anazidi kuchanganyikiwa, anawaita watu wake ili kujipanga kwa ajili ya mapambano. Steve aliyekuwa amekaa tu katika kiti kilichokuwa karibu yake hakuongea lolote. Alikumbuka alivyoambiwa na Mosses kwamba asindikizwe ila yeye alikataa.
“Wale washenzi wameshaanza, sasa tusiwakawize. Tuhakikisheni tunawatokomeza,” Mosses alisema hayo huku Steve akitingisha kichwa kukubaliana naye. Amempa majukumu yote Mosses ya kuongea na kutoa amri kwa vikosi vyake na hivyo lolote litakalotokea Mosses ndiye alikuwa mwenye amri zote.
Alikutana na Mosses wakati Mosses alipokuwa akiunganisha watu wake kwa ajili ya kuanza shughuli za mgodi ambao aliuchukua kwa Mzee Amigolas. Urafiki wao ulizidi kuwa mkubwa kwani walisaidiana kutafuta wanunuzi wa madini nje ya nchi pamoja na kushirikiana katika usafirishaji.
Hali ilipokuwa mbaya kwa Mosses, Steve alijua na hivyo aliamua kumtafuta kwani mbali na kuwa akijishughulisha na mgodi, alijua kwamba Mosses alikuwa akijishughulisha na biashara nyingine pamoja na kujulikana na watu wengi maarufu na hivyo alijua akiwa naye ataweza kufanikisha biashara zake. Hivyo alimchukua na kuwa naye kama msaidizi wake katika kupanga na kuamua mambo ya kibiashara na kutafuta madili mengine yoyote. Pia katika kuiimarisha gome yake kwa kuongeza vikosi ambavyo vingedhibiti hali ya wasiwasi ambayo ingeweza kuikumba ngome yake.
Mosses kwa kuwa alikuwa hana la kufanya baada ya kufilisika pale alipotoroka, sasa anakubali kuungana naye. Anataka kuwamaliza kabisa Aminata na John. Zoezi lake la kwanza alishindwa kutokana na askari wake kuzidiwa nguvu na hivyo anaamua kuanza msako wa kuwakamata na kuwaua peke yake.
“Sihitaji mtu yeyote awaue John na Aminata…. Kazi hiyo nitaifanya mimi,” alisema Mosses huku akiitikiwa na Steve aliyekuwa akimsikiliza pamoja na vikosi vyake.
“Tunaanza kazi sasa hivi, popote walipo watafutwe na waletwe hapa.
Askari wote walitawanyika na kuwaacha Mosses pamoja na Steve. Waliingia ndani ya chumba cha silaha na kuanza kuangalia moja moja. Walichukua zile ambazo alijua zitawafaa na kutoka.
“Tusipokuwa makini hawa jamaa watatuharibia mipango yetu. Inabidi tusimame imara. Hata kama wale wanaongozwa na serikali. Kwanza nitaongea na waziri wa ulinzi ili awapunguze nguvu,” Steve alisema huku akifikiria kuongea na Waziri wa Ulinzi ili awazuie askari wake waliotumwa kuja kuvuruga mippango yake.
Alimpigia simu na kuongea naye baada ya kurudi katika ofisi yake.
Alikuwa akisikilizwa na Mosses ambaye hawakuachana. Simu yake kwa waziri wa ulinzi ilikuwa ni kwa ajili ya kuzima mipango ambayo alikuwa hajaelewa dhamira yake.
Waziri wa ulinzi walifahamiana. Hivyo baada ya kumsihi, waziri wa ulinzi alimwahidi kufanya vile alivyotaka. Aliita wakuu wa polisi na kuwaeleza juu ya hali inayotakiwa kuwepo. Mpango huo haukuwaingia John na Max ambao walikuwa pia ndani ya mkutano huo ulioitishwa na waziri wa ulinzi.
Aminata ambaye alikuwa pia katika mkutano huo. Alifahamu kuwa hiyo ilikuwa imepangwa. Wakiwa wanamsikiliza waziri wa ulinzi, walikonyezana na kuamua kutoka nje.
“Huyu waziri naona ana mawasiliano na wale watu, kwa nini atoe kauli kama zile? Huku ni kuzima mipango yetu.
“Itabidi tuanze na huyo waziri….nani sasa atakayemzuia?”
“Hapana, tutamzuia kwa kuwasambaratisha wale wapuuzi. Tuhakikishe kwanza wale watu hawafanikiwi, kama waziri anajinufaisha kupitia kwao, sasa tukiwazima hatoweza. Na tutamfatilia pia. Tukipata hata picha yao ya pamoja tutahakikisha anawajibika baada ya mpango wetu kufanikiwa,” Max alisema huku John, Aminata na Antony wakimsikiliza na kukubaliana naye juu ya mipango yao.
“Nadhani tuondokeni,” John alisema.
“Hapana, tazameni kule…. Wamekutana naye… naona wanampongeza kwa kauli yake aliyoitoa. Sasa tusiwape nafasi. Hakikisheni hawawaoni na kila mmoja aondoke eneo hili tutakutana kesho kwangu,” Max alimalizia kusema huku kila mmoja akiingia ndani ya gari lake tayari kwa kurejea nyumbani na kukutana siku inayofuata kama walivyopanga.
*****
Mosses anaamini tayari mpango wa Aminata na John ambao anaamini wametumwa na serikali umeshazimwa. Hasira zinamkabili kila awakumbukapo. Anahisi bado wataendelea kumwandama kama ilivyokuwa kwenye mpango wake wa mgodi.
“Sitaacha kuwatafuta hadi nihakikishe nawasambaratisha….washenzi wale walizima mpango wangu mkubwa sana…. mimi sio wa kuajiriwa… tayari nilishamiliki mgodi na kuwa mtu mkubwa sana,” aliwaza Mosses huku akiwa ameshikilia sigara yake ambayo ilikuwa ikiteketea taratibu katikati ya vidole vyake. Aliifuata chupa ya mvinyo na kuweka kidogo na kuibwia yote.
Sasa aliondoka na kuufungua mlango kwa nguvu. Alimkuta Steve amesimama akimsubiri.
“Nilikuja kukuchungulia. Ulikuwa unawaza sana. Nini zaidi ndugu?” aliuliza Steve kauli ambayo ilimshtua sana Mosses ambaye aliamini kwamba hakuna mtu yeyote aliyemwona alipokuwa amesimama. Alienda hadi pale alipokuwa Steve.
“Hakuna baya mkuu….ni hawa washenzi wawili… sitamani wawepo duniani… nataka nihakikishe wanatokomea kabisa katika ulimwengu huu.”
“Tuma askari wakawatafute bana….usiwaze na uwezo tunao. Waambie sasa hivi waanze msako. Watu wale hawawezi kutusumbua sisi.”
Mosses alifanya kama alivyoambiwa na Steve. Aliwatuma askari kumi kwenda kuwatafuta na kuwakamata Aminata pamoja na John.
“Ndio mkuu,” waliondoka kwa pamoja na kwenda kuchukua gari moja tayari kwa kuwatafuta na kuwapata John na Aminata kama walivyotumwa.
*****
Wakiwa ndani ya gari la Max, ulikuwa ni usiku saa tatu. Walikuwa wakirudi kutoka kikao kilichowahusisha wapelelezi wa Mkoa wa Arusha na Mwenyekiti wao wa upelelezi kilichofanyika katika hoteli ya Ngurdoto.
Aminata ambaye ndiye alikuwa akiendesha gari, aliyaona magari mawili yaliyokuwa yamesimama na kufichwa ndani ya kichaka. Alibaki akiwa anayaangalia tu huku akipunguza mwendo wa gari. Aliyashangaa yalivyokuwa yamesimama pasipo kuona mtu yeyote.
Ghafla gari moja lilitoka na kusimama mbele yao na askari wengine wakitoka vichakani na kuwaelekezea bunduki zao. Wote walishtuka na ghafla walipunguza mwendo na kusimama. Walichomoa bastola zao na kuziweka tayari.
Haikuwa kazi rahisi kama walivyofikiria kwani walishajua wale ni askari wa Mosses. John alitoa bastola yake na kuanza kuwatupia risasi. Aminata na Max nao walianza kuwashambulia huku Aminata akiongeza mwendo kulipita lile gari lililokuwa mbele yao.
Max alilishambulia na kufanikiwa kumuua dereva wake baada ya kuwamaliza wale waliokuwa wamejificha vichakani. Lile gari lilienda na kugonga mti kisha kusimama. Haraka John na max walitoka na kuwafuata. Waliwaua wote na kuwaacha hapo hapo na kisha kuondoka.
“Jamani mnaona,” alisema Aminata aliyeonekana kupatwa na wasiwasi.
“Usiogope… sasa wamechokoza.” Alisema John.
“Watajua tu watu wao wameuliwa na watajua lazima ni sisi. Sasa tusirudini home sasa hivi. Tutafuteni mahali tujiweke sawa alafu tuende. Zana zote zipo kwenye buti ya gari nlilompa Antony na mabegi mengine yapo kwangu.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi