HATI FEKI (15)

Zephiline F Ezekiel
HATI FEKI (15)
Jina: HATI FEKI Mtunzi: Hassan S. Kajia SEHEMU YA KUMI NA TANO ILIPOISHIA... MAX mara moja alifika eneo la maliwato kumsubiri Steve aingie. Aliwasiliana na John ili aweze kuzuia watu kuingia eneo hilo na badala yake awashauri watumie maliwato nyingine. Wakati huo hakukuwa na watu wakiingia maliwatoni huko na hivyo ilikuwa ni nafasi nzuri ya Max na John kufanikisha mpango wao. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Haikuchukua muda Bosi Steve aliingia, Max alisubiri hadi amemaliza na kuchomoa bastola yake na kumnyooshea Steve. Bosi Steve alishtuka kusikia sauti ya Max ikimwambia. “Usijiguse na simama hapo hapo kama ulivyo,” kabla ya kugeuka kumwangalia aliyetoa sauti hiyo alipigwa ngumi na kuzirai. Max aliwasiliana na John kwamba kashamteka hivyo wajitayarishe kuondoka. Antony alifungua mlango wa gari na kulisogeza mpaka karibu na mlango wa kutokea na hivyo ilimchukua Max dakika mbili kumfikisha Steve ndani ya …