
Mtunzi: Hassan S. Kajia
SEHEMU YA KUMI NA SITA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
“Watajua tu watu wao wameuliwa na watajua lazima ni sisi. Sasa tusirudini home sasa hivi. Tutafuteni mahali tujiweke sawa alafu tuende. Zana zote zipo kwenye buti ya gari nlilompa Antony na mabegi mengine yapo kwangu.
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
Tuyafuateni kwanza.”
“Mi nadhani tungeekwenda hukohuko Mererani tukavamie kabisa. Hapo tutakuwa hatujawapa nafasi, kabla hawajajua kama watu wao wamekufa,” Max alitoa wazo ambalo lilikubaliwa na kila mmoja.
“Lakini…. Nadhani tuwasiliane na Antony kwanza… yeye ndo anapajua.
“Kweli, mpigie simu mwambia aje kamili. Aje usiku huuhuu, mwagize apitie kwangu Michelle atampa yale mabegi aje nayo,” alisema Max.
John alitoa simu yake na kuanza kuongea na Antony.
“Tayari nipo huku. Nyie njooni tu huku.”
“Haa! Ok, sisi ndo tunageuza, uko kwa wapi. Na vipi mabegi tuliyoyapeleka kwa Max.”
“Nliyaweka yote kwenye gari lake kabla hatujaachana nyie mkaenda kwenye kikao. Mimi nipo kwenye hoteli tuliyofikia kipindi kile. Nimefanikiwa kuingia hadi ndani na kutoka.”
“Ndani wapi Antony?” alihoji kwa mshangao John.
“Katika lile jumba lao. Nimeshapaona vizuri.”
“Ilikuajekuaje kaka. Ngoja tuje afu utatuelezea poa,” John alimkatisha Antony asiendelee kuzungumza ili wafike kwanza.
Antony alikuwa tayari ameshafika Mererani. Alifanya juhudi zote ili kuhakikisha anafanikiwa kuingia ndani ya lile jumba ambalo lilikuwa limefichwa. Jumba lililomilikiwa na Steve.
Alifanikiwa kumrubuni askari mmoja wa Mosses na kumteka kisha kumuua na kuchukua mavazi yake. Alijichanganya na kufanikiwa kuingia. Alifanya kama walivyokua wakifanya wao na hivyo asingeweza kujulikana mapema kutokana na kufanana nao.
Alifanikiwa kutoka na kurudi katika chumba chake alichopanga katika hoteli moja maarufu ambayo waliitumia wakati wa mashambulizi dhidi ya Mosses.
*****
Saa tano usiku kina John walikuwa wameshafika na kuungana na Antony. Walimkuta akiwa amevalia zile sare za askari wa Mosses.
“Haah! Vipi tena Antony…umetusaliti nini?” aliuliza John huku akimkagua Antony na kuingia hadi ndani.
“Hapana….kwa hali ilivyo sidhani kama kuna kupumzika….viongozi wao wote wametoka. Kama mtakuwa mmesikia helikopta.
Wametumia helikopta. Sasa tusizubae kabisa.”
“Sawa tuanze na hao vibaraka wao.”
“Usiku huu huu?” alihoji Aminata.
“Ndiyo… kesho asubuhi watahadithia,” Antony alisema. John na Max walicheka.
“Sasa sikilizeni, kutokana na nlichokiona ndani kule… nadhani sio pa kuchanganya. Mimi nitaanza kuingia nao alafu nitaacha mlango wa kuingilia ndani wa upande wa nyuma ukiwa wazi. Nyie mtapitia huko. Mkifika ndani mtakuta mi nimeshasambaratisha baadhi yao.”
“Kweli,” aliitikia John aliyeonekana kuwa na shauku ya kupambana. Aminata alimwangalia na kutabasamu akikumbuka walivyoweza kupambana nao walivyokuwa wakidai mgodi wao.
Alimwangalia zaidi na kumkumbuka mtoto wao ambaye hakujua lolote lililokuwa likiendelea. Alikumbuka pia John alivyomwambia abaki asiende kwenye mapambano ili mtoto wake asije akakosa uangalizi.
“Mimi nitawasubiri hapa hotelini na nikiona mmezidiwa nitawasiliana na vikosi vyetu waje,” alisema Aminata. Kauli yake iliwashtua wote.
“Hakuna tatizo, naamini sisi watatu tutaweza. Hakuna kumwonea huruma hata mmoja. Ni kuwaangamiza wote,” John alisema huku akiikoki bunduki yake na kuifunga vizuri. Max naye lifanya vivyo hivyo. Antony yeye allikuwa tayari amejikamilisha. Bunduki mbili nyuma ya mgongo na bastola iliyojaa risasi pamoja na mabomu mawili ya kurusha kwa mkono.
John alimwangalia na kukumbuka mazoezi aliyokuwa akiyafanya. Anakumbuka pia alivyorudi nyumbani wakati baba yao alivyokuwa hai. Antony alitoroka katika mafunzo ya kijeshi aliyokuwa akifanyia katika kikosi kilichokua na kambi yake Monduli.
Alikuwa amebakiza miezi michache tu amalize mafunzo yake ya kijeshi. Mzee Amigolas alikuwa amefanikiwa sana. hapo pakawa pamemchanganya Antony na hivyo aliamua aachane na kutumikia jeshi na kuamua kuwa karibu na baba yake. Miaka michache baadaye aliweza kupewa na baba yake miradi ya kusimamia ambayo ilikuwa Nairobi nchini Kenya.
Alikuwa akiwasiliana na mmoja wa wanajeshi ambaye alimtumia ili aweze kupata vifaa vya kijeshi. Alifanikiwa kuvipata na hivyo kuvihifadhi tayari kwa mapambano na hivyo aliamua kwenda mwenyewe Mererani ili kufahamu zaidi kuhusu jumba hilo.
“Naona umeshiba tayari kwa mapambano,” John alimwambia Antony huku akimpigapiga begani.
“Niko tayari, sijui nyinyi kama mko tayari tutoke.”
“Nadhani kwa wakati huu ulinzi utakuwa umeimarishwa sana….watatuona. sasa kwa nini tusiteke moja ya magari yao alafu tusogee nalo kabla Antony hajaingia nalo,” John alitoa wazo ambalo liliwafanya Anthony na Max wajilize kama wameafiki.
“Kweli… antony itabidi uwazuie wewe ambaye umevaa sare zao alafu na sisi itabidi tukisha wateka na kuwaua tuchukue nguo zao tuingie nazo,” alisema Max na kukubalika kwa wote.
“Kweli… tena naskia gari zinapita…. Antony toka ukacheki moja ulisimamishe.”
Antony alitoka na kufanikiwa kusimamisha gari moja ambalo lilikuwa lina watu watatu. Magari mengine yaliendelea kwenda wakati yeye akiwa amelisimamisha lile moja. Hawakumwelewa. Walibaki wanamshangaa iweje yupo nje wakati huu.
Hakuna aliyemhoji. Aliwahadaa ili aweze kupoteza muda ili magari mengine yaweze kufika mbali na sehemu walipo. Hakuna aliyekuwa na wasiwasi naye kwani walijua ni mwenzao.
Ghafla Antony alitoa bastola yake aliyokuwa ameifunga kiwambo cha kuzuia sauti na kuwafyatulia wote. Aliwapeleka hadi walipo kina John na Max na kuwaweka katika chumba kimoja na kuwatoa nguo zao ambazo John na Max walivaa na kuchukua pia silaha zao.
Aminata aliachwa nao kwenye kile chumba ambacho kilikuwa nje ya ile hoteli bila ya mtu yeyote kuingia. Aliwataarifu wahusika wa hoteli ile na kuwatolea kitambulisho na kuwaeleza kwamba wako kazini na hivyo wasiogope wala kushiriki kwani ni hatari.
Kuona vile watu waliokuwa kwenye ile hoteli waliamini na kuwapa nafasi ya kufanya wanalolitaka bila kutoa taarifa kama Aminata alivyowaagiza wakae kimya wasubiri kitakachotokea.
*****
Antony, Max pamoja na John walitoka na kuelekea kule yale magari yalikoelekea wakipitumia lile gari alilolisimamisha Antony. Walifika na kufunguliwa mlango mkubwa na walipita bila ya kuwa na wasiwasi wowote. Baada ya kufika eneo la kupaki magari walishuka na John na Max wakaanza kumfuata Antony.
Wakiwa wamebeba mabegi yao na silaha kama baadhi ya askari walivyokuwa wamebeba. Waliwasiliana na kuanza kuyatega mabomu kila upande kuhakikisha wanaliporomosha jengo zima.
Helkopta iliyokuwa imewapeleka Mosses na Steve ilikuwa ikirudi na hivyo askari wote walitakiwa kusimama katika paredi tayari kwa kuwapokea na kusikiliza machache kutoka kwao kama ratiba ya siku hiyo ilivyokuwa ikisema. Kwa John, Antony na Max hilo ililikuwa kazi kubwa sana kwao na hivyo waliamua kukimbia na kwenda kujificha.
Baada ya Mosses na Steve kuingia na kuona vikosi vyote vikiwa vinawasubiri. Mosses aliwapa taarifa juu ya vifo vya askari ambao alikuwa amewatuma kwenda kuwaangamiza kina John. Kinyume na matarajio yake. Walishindwa kufanya hivyo na hivyo wote waliuliwa.
“Tumepoteza wazembe…wazembe ambao nimewapa kazi ya kuwashika watu wawili tu lakini watu hao wawili wamewashinda na kuwaua kabisa….inaonekana ni kiasi gani mlivyo wazembe,” Mosses aliongea kwa kufoka. Hakuamini kama askari aliowatuma wameuliwa. Hasira zilimpanda sana.
Kina John walisikia yaliyosemwa na Mosses. Waliamua kutoroka ili wakishatoka wayaache mabomu yalipuke yenyewe. Walitaka kutafuta njia ili watoke kwani isingekuwa rahisi wao kutoka kwani wangeonwa kwa kuwa askari wote walikuwa wameitwa sehemu moja.
Wakati akiendelea kutoa maneno makali kwa askari wake. Ghafla alisikia sauti ya risasi iliyofyetuliwa na Max kumlenga mmoja wa askari aliyekuwa mlangoni ambaye aliwaona. Hali hiyo iliwashtua na hivyo Steve aliwaamrisha askari kadhaa waende wakaangalie ni nini. Kufika tu, walikutana na kichapo kikali. John na Max waliwamiminia risasi huku Antony akisonga mbele kueleke mlangoni. Ghafla walishangaa askari wengi wakija na kuanza kuwarushia risasi huku wakikimbia. Mosses alijua mambo yameshaharibika.
“Tusitoke hadi tuhakikishe wanaisha…. Sio wengi sana hawa. Wavuteni kwenye maeneo tuliyotega mabomu. Ila tuweni waangalifu maana baada ya dakika ishirini na tano sasa yatalipuka. Itabidi tuwahi kutoka nje.
Risasi zilianza kurindima. Walifanikiwa kuwaua baadhi yao huku wengine wakijaribu kukimbia. Waliwafuata huko huko walikokwenda.
Mosses na Steve walionekana kuchanganyikiwa baada ya kuona mashambulizi ya ghafla yaliyozuka katika jumba lile. Alipiga simu na kuwaarifu vikosi ambavyo vilikuwa mgodini vije visaidie mapambano.
“Nani kawaruhusu hawa wajinga kuingia?” alifoka sana Steve huku akiitoa bastola yake na kuikoki vizuri.
Aliona kama Mosses ndo aliyesababisha yote yale kwani kabla ya kuwa naye hakuna baya lililomtokea. Na sasa vikosi vyake na mipango yake inaharibika. Mosses na yeye alijua kwamba Steve lazima atamgeuka na hivyo aliamua kutoka kwa lengo la kukimbia.
Antony na Max walikuwa wameshaingia na kuanza kushambulia katika chumba alichokuwa Steve na baadhi ya askari.
Waliwaua wote na kubaki na Steve ambaye hakuwa na ujanja wowote wa kutoroka zaidi ya kusalimu amri na kuweka silaha chini. Baada ya kuona askari wengine wakija Antony na Max walianza kuwashambulia pamoja na kumpiga risasi Steve na kumuua palepale huku wakiwashambulia askari waliokuwa wakiongezeka mmoja mmoja.
Antony alipigwa risasi ya begani na hivyo alikuwa akitumia mkono wa kushoto huku akimhimiza Max watoke nje. Max alikuwa amemshikilia na mkono mmoja huku akiendelea kuwashambulia hadi walipotoka nje huku akizidi kuwashambulia.
*****
Aminata na Francis walikuwa njiani wakiwafuata kina John. Huko alikutana na kundi la askari wa Mosses wakielekea kwenye jumba la Steve kusaidia. Waliwashambulia kwa risasi mfululizo hadi kuhakikisha wameisha wote ambao nao walikuwa wakijibu mashambulizi kwao.
Walifika muda mfupi baada ya kusikia mashambulizi yakiwa makali. Aminata na Francis walifika mbele ya lango kubwa na kuwashambulia askari waliokuwa wakiwasubiri kina John.
Alimwona Mosses akiifuata helikopta kwa lengo la kutoroka lakini mara helikopta ile iliondoka na hivyo hakuweza tena kuipata. Aminata aliwahi na kuilenga ile helikopta na kuilipua.
Mosses alishtuka baada ya kuona imemuacha na kisha kulipuka.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi