HATI FEKI (9)

Zephiline F Ezekiel
Jina: HATI FEKI

SEHEMU YA TISA
ILIPOISHIA...
Alitokomea kusikojulikana pamoja na yule mlinzi wake ambaye muda wote alikuwa amechoka baada ya damu nyingi kumtoka baada ya kupigwa risasi ya begani.

Kuona vile, Mosses aliamua kumpiga tena risasi na kumuua kwani aliona atasababisha wakamatwe.

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
Alipita katikati ya mashamba na kutokomea kabisa.

*****

Asubuhi, watu walikuwa wamejazana katika eneo hilo ambapo miili ya polisi ilikutwa hapo. Polisi watatu wakiwa wamelala chini. Walikuwa wameshakufa. Habari zilienea kila mahali.

“Aaah. John,” aliita Aminata kwa ukali.

“Sema mpenzi, nini tena huko?”

“Huwezi amini…”

“Nini?” aliuliza John kwa mshtuko.

“Yule mshenzi, amefanikiwa kutoroka, kawaua wale polisi na sasa hajulikani aliko.”

“Dah….sasa itakuaje Aminata.”

“Dah hata….hata sielewi tuanzie wapi tena…tutampataje sasa?” aliuliza Aminata ambaye alikuwa ameshakata tamaa.

“Ngoja nimshtue Antony,” John alisema huku akiifuata simu yake na kumpigia Antony ambaye alifika pale dakika kumi baadaye ili kujua itakuaje.

“Itabidi tumtafute wenyewe tena.” Aminata alisema huku akinyanyuka tayari kuvaa kwa ajili ya safari ya kurudi mjini Arusha.

Antony alitoka na kwenda hadi kwa wale wachimbaji ili kuongea nao. Aliwataka wakae tayari na kujitayarisha tena kuanza kazi kwani wanafuatilia hati miliki na jina la kampuni ili waweze kuendelea na shughuli.

“Kwa hiyo, tutamtuma kiongozi wenu awataarifu mambo yatakapokuwa mazuri,” alisema Antony huku akishangiliwa na wachimbaji wote.

“Antony wamemubali sana, naona wanamweshimu. Inawezekana jana usiku aliwatuliza sana,” John alisema akimwambia Aminata wakati wakiwa ndani ya gari la Antony wakimsubiri kwa ajili ya safari.

“Unajua mmefanana sana na mzee wenu. Ndo maana wamewatambua haraka. Na pia yule jama aliyetutaarifu.”

“Mbago…au sio?” aliuliza John.

“Yah, huyohuyo, amesaidia sana jitihada hizi,” Aminata alimaliza kuongea. Antony alikuwa ameshafika kwenye gari na kuanza kuingia.

“Nitawaendesha mwenyewe waheshimiwa,” wote walicheka na safari ya kuelekea Arusha ilianza.

*****

Walifika mjini na kuelekea moja kwa moja hadi nyumbani kwa kina John, Njiro. John na Aminata walianza kuyasahau ya mapambano na sasa waligeukia penzi lao usiku huo. walirudi ndani ya penzi lao zito ambalo kwa muda walilisahau.

“Mpenzi, nadhani haina haja ya kuchelewesha mipango yetu. Tuoane kabisa,” John alikuwa wa kwanza kumsihi Aminata juu ya ndoa. Hakujua juu ya siri ambayo ilikuwa ndani ya moyo wa Aminata. Aminata alimwangalia sana John kwa shauku ya kumwambia. Alijua atafurahi sana baada ya kumtamkia juu ya ndoa.

“Sidhani kama kuna pingamizi John. Muda tuliokuwa pamoja ni dhahiri kwamba tumeshajuana na haina haja ya kukawiza,” Aminata alisema huku akimsogelea John ambaye na yeye alimvuta karibu Aminata na kuanza kumshushia mabusu motomoto.

“John,” aliita Aminata huku akiwa bado kifuani kwa John.

“Sema mpenzi wangu,” John aliitikia huku akimweka sawa Aminata kusikia kauli ambayo alikuwa anataka kumwambia.

“Hujui lolote kuhusu mimi?” aliuliza Aminata huku akichezea kideevu cha John aliyekuwa akimwangalia wakati wote.

“Hapana, sifahamu mpenzi. Nijulishe tafadhali,” John alimsihi Aminata amweleze alichokitaka.

“Niangalie vizuri utajua.”

“Aminata….una mimba yangu?” John aliuliza kwa furaha.

“Ndiyo mpenzi.”

John alifurahi kupita kiasi. Alimkumbatia Aminata kila wakati. Furaha aliyokuwa nayo hakutamani kumwachia.

Ilibakia kucheza na kupeana mapenzi motomoto usiku huo. Aminata alijua kuutumia vizuri mwili wa John na hivyo hakumpa nafasi ya kupumzika. Alimshika sehemu zote na kumwonyesha utundu wake. Alitaka kumwongezea furaha zaidi ya ile aliyokuwa nayo ya kufanikiwa kusambaratisha kundi la Mosses na kujua kwamba alikuwa ana mimba yake.

*****

John na Aminata walifunga ndoa na kuishi pamoja. Antony alisimama imara hadi kuhakikisha mgodi unaanza tena kazi.

Miezi mitatu baada ya hali kutulia mgodi ulirudi tena na kuanza kufanya kazi. Waliajiri wataalamu mbalimbali kwa ajili ya kusimamia na kuongeza wachimbaji wengine ambao walikuwa chini ya mbago.

Sakata la Mosses lilikuwa limebaki mikononi mwa polisi ambao walikuwa wakiendelea na msako juu yake popote alipo. Walifanikiwa kuweka vizuizi ktika mipaka yote. Mawasiliano yake pia yalirekodiwa pale ambapo aliitaka kuwasilianana na watu aliowafahamu.

Mosses hakuwa na pakukimbilia zaidi ya kuzunguka tu ndani ya nchi. Hakuna aliyetaka kujihusisha naye kwa kuhofia kukamatwa baada ya kusikia Mosses anatafutwa kwa udi na uvumba na polisi.

Aliamua kuishi kwa kujificha. Hakuwa na hata pesa kwani akaunti zake zote zilifungwa na kiasi alichokuwa nacho mfukoni kilimalizika.

Aliishia kushinda maeneo ya Sinoni ambapo huko alifahamiana na vijana wengi aliokuwa akiwatumia kumfanyia biashara ya kusambaza dawa za kulevya kwa kuziuza kwa wateja wake.

Aliwaza na kumkumbuka Aminata ambaye alishawahi kufika Kambi ya Fisi. Alikumbuka kwamba ni Aminata ndiye aliyesababisha yeye kumuua Dula ambaye ndiye aliyetoa siri za kundi lao.

“Nitakutafuta wewe mwanamama,” aliwaza huku akitngisha kichwa chake kuonyesha dhamira yake ya kumtafuta Aminata.

“Nitakuua kabla ya mimi kufa… lazima ufe wewe mama,” Mosses alisema huku akicheka na kuiweka sigara yake mdomoni tayari kwa kuiwasha.

*****

Wakiwa ndani usiku. John na Aminata wallikuwa wakifurahia mimba ya Aminata ambayo ilibakiza siku chache tu aweze kujifungua. Aminata alikuwa akipenda sana kucheza na John kla wakiwa pamoja.

Alimkumbusha shauku yake ya kutaka kumwona Mosses aiwa yuko jela au amekufa. Hilo lilimwingia sana John ambaye pia hakuridhika kusikia Mosses alikuwa ametoroka na hakujulikana aliko.

“Usijali…cha msingi ni kuwa makini na huyu mtu kwani sidhani kama amekufa bali atakuwa tu mitaani.” John alisema huku akimshika aminata aliyekuw amesuimama akielekea dirishani. John alibaki amesimama huku akimwangalia Aminata akienda kuweka pazia la dirisha vizuri.

Ghafla Aminata alirudi kasi na kumkumbatia John.

“Nini Aminata?”

“Nimemwona mtu….”

“Mtu gani, acha woga. Aminata.”

“Mosses, kweli, nimechungulia tu nayeye akaniangalia afu akakimbia.”

“Sasa we unamwogopa?”

“John, kwa hali hii..sitaki matatizo. Waniache kwanza nijifungue mtoto wangu.” John alicheka sana na kumbeba Aminata hadi chumbani tayari kwenda kulala.

(END OF SEASON 1)

MWISHO WA SEHEMU YA KWANZA

MOSSES ANAFANIKIWA KUTOROKA. ANAUA POLISI NA KUTOKOMEA. TAARIFA ZAKE ZINAVUMA NA MSAKO MKALI JUU YAKE UNAANZA.

ANAJIFICHA KILA SEHEMU KUHAKIKISHA HAKAMATWI.

AMINATA BAADA YA KUWA MJAMZITO ANAOLEWA NA JOHN NA KUISHI PAMOJA HUKU ANTONY AKIRUDISHA HADHI YA MGODI NA KUANZA KAZI.

AMINATA ANAMKUMBUKA MOSSES NA MARA ANAIONA SURA YAKE NA KUOGOPA WAKATI AKICHUNGULIA DIRISHANI….ANAHISI KAMWONA MOSSES.

JE HIYO NI SURA HALISI YA MOSSES AU NI TASWIRA TU ILIYOMWINGIA AMINATA KWA WOGA

HII NI SEHEMU YA MWISHO YA SIMULIZI HII KALI YA HATI FEKI (SEASON 1)

***SEASON TWO***

Katika RIWAYA hii SEHEMU YA KWANZA (SEASON ONE), John, Antony na Aminata wanaingia katika mtihani mgumu wa kulipa kisasi na kurudisha mali yao ambayo ilichukuliwa kwa hila na Mosses Ndula. Wanafanikiwa kuwatokomeza na kuurudisha mgodi huku John na Aminata nao wakionekana kuimarika katika penzi lao. Aminata anapata mimba ya John.

Antony baada ya kufanikiwa kurejesha mgodi anaweka mambo vizuri na kisha anarudi Nairobi kuendelea na shughuli zake ambazo zilisimama kwa muda.

Mosses Ndula, anafanikiwa kutoroka polisi. Anajificha mtaani Sinoni kwa rafiki na vijana wake ambao alifanya nao kazi. Wanamchukua na kumpa hifadhi. Kwa kuonyesha hajaridhika na ushindi wa kina John na Aminata. Anawaza namna ya kuwafuata tena tena na tena.

SEHEMU HII YA PILI (SEASON TWO) Mosses Ndula anaonekana kufufuka upya. Anakutana na mfanyabiashara mkubwa wa madini na tajiri Steve Mikaeli. Anamchukua Mosses na kufanya naye kazi pamoja na viongozi wengine wa serikali.

Je, watafanikiwa kuwasambaratisha kina John ambao ndio wapinzani wao wakubwa katika biashara ya madini kama ilivyokuwa kwa mzee Amigolas.

Endelea…..

*****

Biashara ya madini ilikuwa kubwa sana kwa John na Antony. Kulikuwa na ushindani ambao ulikuwa ukiendelea bila John na Antony kufahamu. Hila za kila aina zilikuwa zikifanywa ikiwa ni pamoj na kuwateka na kuwaibia wafanyakazi wa mgodi wa Amigolas.

Jambo hilo liliwafanya baadhi ya wafanyakazi wa mgodi kushangaa huku wengine wakirubuniwa na kuhamia katika mgodi wa Steve.

Steve Mikaeli, ambaye baada ya kusikia taarifa za Mosses anaamua kumtafuta na kumficha kabla ya kumwibua tena.

Katika taarifa zake za kuonekana katika mitaa ya Sinoni. Steve anawatuma watu na siku hiyo hiyo anaonekana n taarifa zinafika polisi ambapo alikuwa akitafutwa huku wengine wakisema kuwa ametoweka na helikopta baada ya kufuatwa na watu wasiojulikana na kupelekwa kusikojulikana.

Akiwa tayari amefika na kuongea vizuri na Steve na kuelewana. Sasa Mosses alijua mambo yake yatakwenda vizuri ingawa bado hakuwa amemwambia hadi pale Steve alipomuuliza ili ajue ukweli wa yeye kuwa katika hali ile.

“Kuna wajinga waliokuwa wakinifuatilia. Wametaka kuharibu maisha yangu lakini hawakuwezaa,” Mosses aliongea kwa hasira huku akionekana kutaka kupiga chochote au yeyote ambaye atakuwa amesimama mbele yake. Hilo lisingewezekana kwa kuwa aliyekuwa mbele yake alikuwa ni bosi wake, Steve.

Steve alionekana akimsikiliza kwa makini hukun akujua ushindani wake wa ibiashara utaongezeka ikiwezekana kuua kabisa biashara ya madini katika mgodi wa mzee Amigolas kwa kumtumia Mosses. Alitaka kuhakikisha Mosses anawahadaa wachimbaji wa mgodi wa Amigolas na kuwafanya wajiunge na mgodi wake.

Jambo hilo lilionekana kumfurahisha sana Mosses ambaye alijua wazi hiyo itakuwa mbinu moja wapo ya kuwachokoza John na Aminata ili aweze kuwakamata.

Aliamini kwa kuwahadaa huko wangethubutu kujitokeza na kwamba huo ndio ungekuwa mwisho wao kwani angewamaliza kabisa. Alifurahia na kujiona mpya kabisa ambapo ka kipindi kirefu alikuwa amesahaulika. Ujio huu ulimfanya afurahie zaidi kwani aliamini atakuwa na sura na mwonekano mpya kwa wale wasiomjua.

John alikuwa chini ya ulinzi mkali. Ulinzi mkali wa askari wa Mosses Ndula. Hakujua kwa nini wameweza kutekwa kirahisi hadi kujikuta mikononi mwa Mosses. Hawakuweza hata kujiokoa kwani jeshi la Mosses Ndula lilionekana kuwa imara. Alitakiwa kusema ukweli juu ya jambo ambalo Serikali inataka kujua kwani inaonekana kama alitumwa na chombo hicho kikuu cha dola.

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni