HATI FEKI (9)

Zephiline F Ezekiel
HATI FEKI (9)
Jina: HATI FEKI Mtunzi: Hassan S. Kajia SEHEMU YA TISA ILIPOISHIA... Alitokomea kusikojulikana pamoja na yule mlinzi wake ambaye muda wote alikuwa amechoka baada ya damu nyingi kumtoka baada ya kupigwa risasi ya begani. Kuona vile, Mosses aliamua kumpiga tena risasi na kumuua kwani aliona atasababisha wakamatwe. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Alipita katikati ya mashamba na kutokomea kabisa. ***** Asubuhi, watu walikuwa wamejazana katika eneo hilo ambapo miili ya polisi ilikutwa hapo. Polisi watatu wakiwa wamelala chini. Walikuwa wameshakufa. Habari zilienea kila mahali. “Aaah. John ,” aliita Aminata kwa ukali. “Sema mpenzi, nini tena huko?” “Huwezi amini…” “Nini?” aliuliza John kwa mshtuko. “Yule mshenzi, amefanikiwa kutoroka, kawaua wale polisi na sasa hajulikani aliko.” “Dah….sasa itakuaje Aminata.” “Dah hata….hata sielewi tuanzie wapi tena…tutampataje sasa?” aliuliza Aminata ambaye alikuwa ameshakata tamaa. …