KONSTEBO NGUZU (1)

Zephiline F Ezekiel
KONSTEBO NGUZU (1)
Jina: KONSTEBO NGUZU Mtunzi: George Iron Mosenya SEHEMU YA KWANZA "Nimekosa magoli zaidi ya 9000 katika maisha yangu, nimepoteza mechi zaidi ya 300 katika maisha yangu, niliaminiwa mara 26 kuwa nitaipa timu yangu ushindi lakini nikashindwa. Nilishindwa tena na tena na tena katika maisha yangu NDIO MAANA NIKAFANIKIWA- Michael Jordan , mchezaji wa zamani wa mpira wa kikapu." HALI haikuwa shwari katika kota za polisi maeneo ya Mabatini jijini Mwanza , shida ya maji ilisababisha baadhi ya maaskari kwenda kazini pasi na kuiloweka miili yao panapo maji. Umeme nao uliwalazimu wengi wao kuzipiga saluti huku nguo zao zikiwa hazijanyooshwa. Hii haikuwa shida sana kwa kundi kubwa. Majira ya saa tatu kasorobo gari la maji liliwasili, lilikuwa ni agizo la serikali baada ya vilio kuwa vingi kutoka kwa wafanyakazi hawa watiifu. Akina mama wakatoka nje na kuikimbilia ile gari na kujikuta wameunda foleni ya kutisha huku kila mmoja akimuhimiza mwenzake asiruhusu mtu kuingia mbele yake kwani kila mmoja…