KONSTEBO NGUZU (13)
Jina: KONSTEBO NGUZU Mtunzi: George Iron Mosenya SEHEMU YA KUMI NA TATU ILIPOISHIA... Akamalizia na tusi lake la kiitaliano. Lakini kwa mara ya kwanza akajikuta akilitoa tusi hilo kinyonge sana. Inspekta Kobo akagundua kuwa alikuwa yu na uoga wa ajabu mno, JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... uoga ambao hajawahi kuwa nao hapo kabla. Ni hapa alipokiri kuwa yumkini damu nzito kuliko maji lakini penzi ni zito kuliko vyote, maji na damu ukivichanganya pamoja. Inspekta akakiri kuwa katika mapambano ya zamani hakuwa muoga kwa sababu aliingia katika mapigano huku katikati ya uwanja wa mapambano pakiwa hakuna ndugu yake wala mtu anayempenda, hivyo hata akifa mtu kwake haikuwa tatizo. Sasa anawatukana watu walioshika hatamu ya maisha ya mkewe kipenzi. Inspekta akatubu kimyakimya. Wakati anakiri kuwa anawaogopa watekaji, simu yake ikaita. Nambari ilikuwa ngeni, akajua wazi kuwa huyo atakuwa ni mtekaji na sasa anataka kutoa…