KONSTEBO NGUZU (2)

Zephiline F Ezekiel
KONSTEBO NGUZU (2)
Jina: KONSTEBO NGUZU Mtunzi: George Iron Mosenya SEHEMU YA PILI ILIPOISHIA... Huyu alikuwa mrefu wa haja mweusi na ambaye alionekana kuwa mwingi wa mazoezi kwa jinsi umbile la kifua chake lilivyogawanyika. "Nguzu, hapa nd'o ninapojilaza walau siku ziende..." JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Alizungumza mwanadada ambaye Nguzu alipaswa kumtambua kama Zubeda na kusahau kabisa kama aliwahi kulijua jina la Janeth maishani mwake. Nguzu alikuwa amejiandaa kisaikolojia kuanzia awali kuwa yule Janeth wa Mwanza aliyeswekwa rumande kwa sababu ya kumzongazonga mke wa inspekta atakuwa amebadilika mno. Lakini hakudhani kuwa angeweza kuwa anaishi katika nyumba nzuri kiasi kile, kuendesha gari zuri namna ile. Umbo lake nalo lilikuwa limenoga, hakuwa yule kimbaumbau wa Mwanza mabatini. Mate ya matamanio yakamruka Nguzu. Akatamani gari, akatamani nyumba na maisha mazuri kwa ujumla. Lakini angeyapata kwa wepesi g…