KONSTEBO NGUZU (20)

Zephiline F Ezekiel
KONSTEBO NGUZU (20)
Jina: KONSTEBO NGUZU Mtunzi: George Iron Mosenya SEHEMU YA ISHIRINI ILIPOISHIA... Usingizi ulimkuta Nguzu akiwa katika uchambuzi hafifu wa kitabu hiki maarufu, alianza kwa kumpa kongole mwandishi Edwin Semzaba kwa kuandika kitabu hiki, kisha akahamia kwa Ngoswe na Mazoea na hadi anasinzia alikuwa amefikia mahali ambapo Mazoea ameanza kuzoeana na Ngoswe! JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Hii ni baada ya Ngoswe kumuhadaa kuwa atamtorosha waende wote mjini...... Alisinzia akiwa anatabasamu, bila shaka ni vile visa vya Ngoswe vilimpa tabasamu. ASUBUHI ilimkuta konstebo Martin Nguzu katika ofisi ya gazeti mojawapo kati ya yale yaliyoandika habari ya kifo chake na kisha kusemekana aliyeandika ni 'mwandishi wetu. Kama ilivyomkera inspekta Kobo na kujikuta akiponyokwa na matusi ya kiitaliano, kwa Nguzu ilikuwa vilevile lakini hakuwahi hata siku moja kuota ndoto za kiitaliano. Yeye aliponyokwa na matusi mfululiz…