KONSTEBO NGUZU (4)
Jina: KONSTEBO NGUZU Mtunzi: George Iron Mosenya SEHEMU YA NNE ILIPOISHIA... "Kwa hiyo unataka kuigeuza biashara hiyo habari? Na wewe ulipolala na yule dada wa mapokezi nani aligeuza biashara lile tukio lako ama wewe tu nd'o wayaona mabaya ya wenzako..... nilijua umeniitia mambo ya maana kweli mume wangu. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Huo muda ningekuwa nimemfundisha Mariam kuhesabu moja hadi kumi na ameelewa kabisa. Yani we sijui upoje tu..." Akasimama na kutoka nje akiuacha mlango wazi. Juma akabaki kimya kabisa, mkewe alikuwa amemgusa pabaya mno. Hakutaka kuikumbuka kabisa siku aliyofumaniwa na mkewe juu ya suala hilo la kujihusisha kimapenzi na msichana wa ofisini kwao. Ni kweli haikuandikwa popote, lakini hii haikuwa sababu nzito ya yeye kuachana na hili aliloligundua. Ukimya huu haukumaanisha kuwa Juma aliamua kuachana na jambo hili. Akaona mtu sahihi wa kumshirikisha ni Koplo Mtan…