KONSTEBO NGUZU (7)

Zephiline F Ezekiel
KONSTEBO NGUZU (7)
Jina: KONSTEBO NGUZU Mtunzi: George Iron Mosenya SEHEMU YA SABA ILIPOISHIA... "Shangazi, sijui lolote kuhusu huu mpango unaousema, sijawahi kuzungumza na Inspekta juu ya lolote kuhusu Nguzu. Hii ni kweli ya moyo wangu..." "Sawa kama haujui. Mimi naondoka..." alizungumza doktahuku akiyanyanyua mabega yake juu. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Akauendea mlango na kutoweka..... _______ LILIANZA kuwa saa moja, kisha likafuata la pili yalipofika matatu subira ikafikia kikomo. Inspekta Kobo akachukua simu yake na kujaribu kumpigia mkewe amuulize nini kinajiri hadi hajafika nyumbani hadi muda huo. Simu iliita kidogo kisha ikakatwa. Alipojaribu tena haikuwa ikipatikana. Akajaribu kupiga ofisini wakaelezea kuwa Dokta Kobo alitoka kazini tangu saa mbili usiku, wakastaajabu kupokea simu usiku wote huo wa kuuliziwa kwake. Inspekta Kobo ambaye tayari alijiona ni mtu ambaye ameandamwa na majanga ya gh…