MKONO WA JASUSI (19)
Jina: MKONO WA JASUSI Mtunzi: Richard Mwambe SEHEMU YA KUMI NA TISA ILIPOISHIA... “Hujiulizi nimefikaje nyumbani kwako? Je unafikiri ningeshindwa kukuaa kwa bunduki yangu pindi tu ulipoingia? Sikutaka kufanya hivyo kwani nina mazungumzo na wewe kwanza kabla ya kifo chako,” Kamanda akatamba. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... “Ha ha ha ha usinifanye mt0to kabisa, ujanja huo niliufanya zamani sana, kama una mazungumzo na mimi kwa nini hukunitafuta mchana kweupe?” Zebel akacheka na kuuliza. “Mchana nilikuwa na kazi ya kuwafuta duniani wale vibaraka wako uliowatuma Durban wakamuue Lereti, wamemkosa na mkono wangu umewashukia wao,” kamanda akatonesha kidonda. Maneno hayo yalimuumiza sana Zebel, alitamani atoke pale alipojificha na kumchanachana vipande. Wakati yeye akili yake imetibuliwa na maneno hayo ya Amata, naye akatafuta mbinu ya kumvuruga akili ili amuwahi kimapigano; akachomoa simu yake na kupiga kisha…