
Mtunzi: Richard Mwambe
SEHEMU YA KUMI NA TISA
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
“Hujiulizi nimefikaje nyumbani kwako? Je unafikiri ningeshindwa kukuaa kwa bunduki yangu pindi tu ulipoingia? Sikutaka kufanya hivyo kwani nina mazungumzo na wewe kwanza kabla ya kifo chako,” Kamanda akatamba.
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
“Ha ha ha ha usinifanye mt0to kabisa, ujanja huo niliufanya zamani sana, kama una mazungumzo na mimi kwa nini hukunitafuta mchana kweupe?” Zebel akacheka na kuuliza.
“Mchana nilikuwa na kazi ya kuwafuta duniani wale vibaraka wako uliowatuma Durban wakamuue Lereti, wamemkosa na mkono wangu umewashukia wao,” kamanda akatonesha kidonda. Maneno hayo yalimuumiza sana Zebel, alitamani atoke pale alipojificha na kumchanachana vipande. Wakati yeye akili yake imetibuliwa na maneno hayo ya Amata, naye akatafuta mbinu ya kumvuruga akili ili amuwahi kimapigano; akachomoa simu yake na kupiga kisha akiweka loud spika.
“Yeah yupo hapa, fanyeni haraka mkichelewa mtakuta nimekwishamsambaratisha,” akaktya simu.
“Haya jiandae sasa leo tunakunywa damu yako,” Zebel akajibu, wakati huo Kamanda alikuwa kahamanika akajua akichelewesha mchezo ataumbuka kwani alishawajua hao jamaa kuwa kuua kwao ni moja ya misingi ya dini kisha wanakunywa damu yako. Alijirusha sawia kumfikia Zebel lakini kabla hajatua, alipigwa ngumi moja nzito katika uvungu wa paja, haikufika kwenye korodani lakini maumivu yake yalimfanya aiache bastola ikianguka chini paeke yake.
“Kumbe mtu mwenyewe laini namna hii, inaonekana unaua kwa kuvizia,” Zebel akazungumza huku akiinuka kutoka pale alipoketi na kumkimbilia Amata pale chini, kabvla hajafika Amata alijizungusha mtindo wa helkopta, mguu wake mmoja ulipita chini mtambaa panya na ule wa pili ulikuja kimo cha mbuzi huku mikono yake kaiweka chini kwenye sakafu kwa mtindo usiolezeka.
Zebel alililona lile pigo la Amata, pigo la ubunifu, akaruka kwa miguu yake hewani mguu wa Amata uliopita mtambaa panya ukamkosa lakini ule uliopita kimo cha mbuzi haukukosea hesabu, ulimpata na kumbwaga chini kama mzigo lakini Zebel alijitahidi asianguke kizembe namna hiyo, aliruka sarakasi na kushangaa Amata yuko hewani na kutandikwa teke moja kali lililompeleka chini na mguu mwingine ukatua sawia kwenye koo kwa uzito mkubwa. Kamanda Amata akajiviringa kama umbali wa mita moja na kuchomo kisu kisha akachoma katika nyama ya paja la Zebel, kikazama, akakitembeza kwa nguvu na kuchana nyama kama sentimita tatu kuja gotini. Zebel alipiga yowe kali la maumivu na kujipinda, akampiga kichwa kizito Amata kilichompepesua na kumtupa chini upande wa pili.
Zebel aliinuka na kukichomoa kile kisu, hakujali maumivu lakini kwa jinsi alivhokunja sura, utajua tu alikuwa na maumivu makali.
“Aaaaaaiiiiggghhhh!!! Bastard!” alipiga ukulele wa hasira na uchungu huku akimwendea Amata. Kamanda akatazama huku na kule akaivuta meza moja ndogo ya kioo kwa mguu yake na kuisukuma kumwelekea Zebel, akaruka ikampita chini, alipotua akajikuta anashindwa kusimama akaanguka chini, nukta hiyo hiyo Amata akaiwahi bastola yake na kumnyoshea.
“Tulia fala wewe! Haya nambie nani bosi wako zaidi ya Don Angelo?” akamwuliza huku domo la bastola likiwa limemtazama Zebel.
“Aaaaiiighhh! I will kile you bastard,” (nitakuua mwanaharamu), ZEbel aligugumia huku damu zikivuja pajani mwake.
“Kabla hujaniua, utakuwa ushakufa wewe, niambie nani boss wako zaidi ya Don?” kamanda aliongea kwa ukali.
“Nahesabu mpaka tano, nakuua, Moja…!”
“Never, I cannot tell you…” (Kamwe siwezi kukwambia)
“Ok, kumbe kuna mwingine zaidi ya Don Angelo, haya nitajie ni nani? Mbili…”
“Son of Bitch, I swear I will break your neck…” (Mtoto wa Malaya, naapa nitakuvunja shingo yako)
“Tatu! Kifo chako kimekaribia,” akamwambia huku akikanyaga kwa nguvu lile jeraha, maumivu makali yalimpenya Zebel.
“Ok, ok, ok pal, set me free, I will tell you everything,” (sawa, sawa, sawa rafiki, nitakueleza kila kitu)
Kamanda Amata akatikisa kichwa juu chini, akalegeza mguu kwenye lile jeraha, Zebel akatumia nguvu zake zote kujigeuza na kuipiga bastola ya Amata, ikamtoka mkononi, maumivu makali yalipenya kwe nye mifupa ya mkono wa Amata. Alipotahayari, alimwona Zebel akimjia kama mbogo aliyejeruhiwa. Kamanda akaruka hewani na kutawanya miguu yake, mateke mawili ya mfuatano yalimpeleka Zebel kwenye meza nayo ikafunjika vipande viwili. Zebel alinyanyuka na kuchukua mguu wa meza tayari kwa kumshambulia Kamanda Amata. Amata aliinua alikwepa na kumsindikiza kwa kipepsi maridadi cha uti mwa mgongo kisha akachomo kisu kiingine kidogo kwenye mkanda wa suruali yake na kumshindilia kichwani. Zebel alijibwaga chini kama mzigo na kutokwa na damu nzito.
Kamanda akainuka haraka na kumpekua pekua hapa na pale akakuta flash moja ndogo, sksichuyku ns kuitis mfukoni mwake, akachukua funguo na kuuendea mlango ulioonekana wa ofisi kwa jinsi ulivyo. Akacheza nao na kuufungua, hakupata tabu, juu tu ya meza aliliona faili analolihitaji. Akalinyakua bila kuuliza, akaiendea kompyuta kubwa ya mezani, akainua ile system unity, akafyatua loki zake na kung’oa hard disk. Alipohakikisha hivyo anavyo akaelekea jikoni na kufungua mtungi wa gesi kisha akaiacha imwagike kwa kasi. Wakati huo alisikia gari zikisimama huko nje, akajua wameshafika kusaidia wenzao. Hakupenda waingie, alichukua kiberiti cha gesi na kukiwasha kisha akakitupia humo na ile nyumba ikalipuka mlipuko mkubwa, akatoweka eneo lile.
KLINIKI YA KWAZULU NATAL – DURBAN
LERETI KHUMALO ALIZINDUKA na kurudiwa na fahamu zake, alishangaa kuona jopo kubwa la madaktari na wauguzi wakiwa wamezunguka kitanda chake, aliwatazama bila kujua nini kinaendelea.
“Dah! Asante Mungu,” Daktari wake ambaye daima ndiye anayemtibia alishukuru Mungua na kila mmoja mle ndani alikuwa akimpongeza.
Mara baada ya Lereti kupata maswaibu yale hakukuwa na jinsi, daktari wake ambaye anafanya kazi katika kliniki hiyo akishikirikiana na madaktari kadhaa ilibisi wasimamishe shughuli nyingine na kuhakikisha wanarudisha maisha ya Lereti. Kwa kutumia dawa aina ya Methylethylglutarimide waliweza kufifisha nguvu ya dawa kali ya barbitulate paralytic na kumrejesha Lereti duniani.
Akaendelea kuwatazama wote waliomzunguka, hakujua nini kimetokea.
“Pumzika Lereti, hali yako ilibadilika ghafla sana,” Daktari wake alimwambia.
“Hapana kuna daktari wenu alikuja na kuweka dawa Fulani kwenye drip mara nikaanza kuhisi usingizi na viungo v yangu kuwa havina nguvu, kutoka hapo sikujua kinachoendelea, yuko wapi Cinderella?” Lereti alieleza anachokumbuka na mwisho akmwulizia mfanyakazi wake anayempenda.
“Lereti, Cinderella hatunaye duniani,” alijibiwa na hapo akaanza kulia kwa uchungu.
“Aliyekuwekea ile dawa hakuwa daktari wetu Lereti, walidhamiria kukuua, lakini Mungu mkubwa umepona,” walizidi kumweleza na wakati huo bado Lereti alilia kwa uchungu sana. Hali yake ilipokuwa nazuri kwa siku hiyo alihamishwa chumba na kupelekwa chumba kingine ambacho alikaa na mwuguzi muda wote, hakuruhusiwa mtu kuingia hata mlinzi wake mpaka apewe ruhusa na daktari mkuu.
“Lini nitaondoka humu ndani? Nina kazi ya kukamilisha huko nje,” alimwuliza daktari wake pindi tu alipokuja kumtembelea jioni ile.
“Kwa hali ikiwa hivi, kesho utaruhusiwa kutoka, usiwe na wasiwasi,” akajibiwa na kisha Lereti akajilaza vyema kitandani akimwomboleza Cinderella. Kwa mapendo aliyokuwa nayo aliomba familia yake isifanye maazishi mpaka atakapotoka hospitalini.
§§§§§
Kama kawaida, kamanda Amata, akahifadhi ile hard disk kwenye safe box ndani ya gari yake kisha akaondoka eneo lile. Maisha ya Amata sasa yalikuwa hatarini zaidi kwani alikuwa akisakwa kila uchochoro na alijua wazi kuwa akirudi hotelini au kuingia mgahawa wowote basi ingekuwa ni hatari kwake. Aliamua kutoka nje ya mji kabisa, moja kwa moja akaelekea kwa Yule babu ambako alimuokoa Jesca, akaegesha gari mahala salama na kuteremka, mkononi akaibeba ile hard disk na kuingia katika mitaa hiyo ya watu weusi.
Moja kwa moja akakuta bar moja kubwa iliyokuwa bado wazi, akaingia ndani. Mziki mkubwa ulikuwa ukipigwa, na vijana waliokwishapata kinywaji walikuwa wakicheza kurandana na midundo hiyo. Kamanda Amata akajiegesha katika moja ya viti virefu vya kaunta, akaagiza kinywaji na kuletewa, akanywa polepole huku akitazama vijana wale waliokuwa wakicheza kwa ufundi kabisa wimbo wa Chicco Twala, unaokwenda kwa jina la Money Pesa.
Mara ule muziki ukazimwa na Yule mwanadada aliyekuwa pale kaunta akaongeza sauti ya luninga; ilikuwa ni taarifa ya dharula iliyoonesha jumba la kifahali lililokuwa likiteketea kwa moto.
“Wacha waungue tu, hawana mana hao boers,” aliskika kijana mmoja akibwata kipombepombe.
“Wewe weka muziki huko ni shayia time,” mwingine alidakia. Mara mdundo mkubwa ukaendelea, mara hii uliwekwa muziki wa Chaka Chaka, Im burning up na wale vijana wakaanza tena kulisakata ngoma.
“Hey Man, ninunulie kinywaji kwanza ndio nikukaribishe,” sauti ya mwanadada ikifuatiwa na mguso wa kidole sehemu za mbavu za Amata ukamgutusha na kumlazimisha kugeuza sura yake kumtazama msichana huyo.
“Ninunulie kinywaji leo utakuwa bebi wangu mpaka kucheee,” akaongeza na Kamanda Amata bila kujali akamwagizia Heineken mbili. Alipopiga mafundo matatu akazunguka na kusimama mbele ya Amata.
“We sijawahi kukuona hapa Soweto, we mgeni wewe, maana mimi ni Stimela nabeba kila mtu, hivyo nawajua wote,” akaendelea kubwabwaja.
“Hujakosea mpenzi,” kamanda akajibu.
“Mambo si hayo bwana,” Yule mwanadada aliyeonekana kuchoka kwa pombe alizokunywa alijibu kilevilevi. Kamanda akatazama saa yake, tayari ilikuwa ni saa tisa za usiku, akateremka katika kiti chake.
“Wapi tena bebi, hapa Soweto ndio kunakucha saa hii, ona watu ndo wanaingia,” Yule mwanadada akaendelea.
“Sikiliza, unapenda kukaa hapa?” akamwuliza naye akajibu kwa kutikisa bega.
“Sasa nataka unisaidie kitu kimoja, tukifanikiwa, utachagua wapi unataka nikupeleke nitakupeleka.”….
wakatoka nje wakiwa wameshikana mikono, walipofika katikati ya giza nene ambapo hapakuwa na taa yoyote, kamanda akamsimamisha Yule mwanadada.
“Sikia, nataka kompyuta, desktop kuna kazi nataka kufanya kama nusu saa hivi,” akamwambia Yule mwanadada.
“Aaaa hilo tu? Twende kwa kaka yangu hapo mtaa wa pili atatusaidia”.
Wakakokotana mpaka mtaa huo, Amata akaonana na yule kijana, kweli, akamkaribisha na kumpa kompyuta yake ya mezani aitumie. Akaibomoa mfuniko wake na kuipachika ile Hard Disk ili kupata vilivyomo.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi