
Mtunzi: Richard Mwambe
SEHEMU YA ISHIRINI
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Wakakokotana mpaka mtaa huo, Amata akaonana na yule kijana, kweli, akamkaribisha na kumpa kompyuta yake ya mezani aitumie. Akaibomoa mfuniko wake na kuipachika ile Hard Disk ili kupata vilivyomo.
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
Wkati akiendelea na kazi hiyo Yule mwanadada akapitiwa na usingizi, alkadhalika Yule kijana.
Ndani ya disk ile kulikuwa na mafaili mengi ya ajabu ambayo yalkimfanya Kamanda kusisimkwa na mwili, mipango michafu ya kuua na kupoteza, mipango ya ibada za kishetani za kundi hilo, mikataba ya ulaghai walioifanya na makampuni mbalimbali pale Afrika ya Kusini na kuwadhulumu kwa mtindo huohuo wa kuua na kubadilisha mikataba wakitoa vitisho na rushwa kwa watendaji wa serikali.
Kulikuwamo na mafaili ya sauti ambayo yalirekodiwa ama katika mikutano Fulani au vikao vya siri, yaliyozungumzwa humo yalikuwa ni mazito, yanatisha, hayafai kusikiwa na mtu mwenye moyo wa nyama.
Kamanda Amata akaendelea kupekuwa na katikati ya madokumenti hayo ndipo alipopambana na faili lililobebwa na kichwa habari ‘Top Secret’ yaani Siri Nzito, akaingia na kulisoma, ndani yake ndiko alikokuta mpango dhalimu wa ambao viongozi wa wengi wa Afrika wameingina mikataba na hawa jamaa bila kujijua, wakipeleka madini na mali mbalimbali ili kukingwa na kubaki katika nyadhifa zao. Katika faili hili ndiko alikokuta mazungumzo ya siri kwa njia ya sauti juu ya mgodi wa Tanzanite huko Mererani, akatikisa kichwa.
Kurasa ya mwisho kabisa katika faili hilo akakuta mpangilio wa uongozi na picha za watu hao, Top Secret Service Hiarachy, jina la juu kabisa lilikuwa la Robinson Quebec kisha yakagawanywa majina kadiri ya kanda walizogawana, kanda ya Afika Kusini alikuwa ni Don Angelo, akawasoma wote watano yaani wa Kusini ambaye alikuwa akiishi Johanesburg, na mwingine alishika ukanda wa Mashariki huyu aliishi Antananarivo huko Madagascar, mwingine alishika ukanda wa Africa ya Kaskazini yeye aliishi Tunis katika nchi ya Tunisia na alisifiwa kwenye mkataba huo kwa kufanya kazi yake vyema kuwachonganisha watu wa huko na kuwafanya wapigane wenyewe kwa wenyewe.
Zaidi ya hao alikuwepo aliyeshika ukanda wa Afrika ya Maghalibi, huyu aliishi Abuja, Nigeria, yeye pia alifaulu kuanzisha vikundi mbalimbali vya ugaidi na kupora mali ya wananchi kama mafuta na gesi. Kulikuwapo na aliyeshika ukanda wa kati huyu aliishi Djamena, Mali, nay eye alikuwa na kazi hiyohiyo.
Mipango ya kazi na siri nzito zilikuwa katika faili hilko, serikali zipi za kupinduliwa, marais wepi wa kuuawa na wepi wakuwekwa madarakani. Jamaa hawa walikuwa na ratiba ya chaguzi zote za Afrika hivyo waliyaweka mambo yao kisomi zaidi. Kamanda Amata alijikuta akizama katika kusoma hayo mambo na hasira ikizidi kupanda, akashtuliwa na jogoo lililowika kutoka katika nyumba ya pili.
‘Sasa nina watu wawili tu mkononi mwangu, Don Angelo na Robinson Quebec,’ akajiseme kisha akaing’oa ile disk na kurudisha iliyokuwepo. Akachomoa noti za dola hamsini hamsini, moja akaichomeka mfukoni mwa suruali ya Yule mwanadada na nyingine akaipachika kwenye vfulana mchinjo ya Yule kijan akisha yeye akatokomea zake.
ONTARIO – CANADA
SIR ROBINSON QUEBEC alifura kwa hasira, hakutaka kusikia la mhazini wala mnadi swala, kichwani mwake alijawa na jina moja tu la Amata Ric.
“Ni nani huyu Amata sijui kamanda hata akisumbue kichwa changu namna hii?” alibwata hadi wasaidizi wake wakashtuka.
“Hakuna mtu au kundi la watu la kutusumbua sisi hata serikali yoyote haiwezi kututikisa, huyu ni nani?”
“Anaitikisa ngome yangu, ngome imara ya chuma, kaua vijana wetu karibu kumi na mbili, na kijana wangu mahiri Zebel, niliyemfundisha mwenyewe sanaa ya mapigano, shiiiit!” akang’aka.
“Johnson, nataka uniitie viongozi wote wa kanda kuu ya Afrika, wafike hapa mara moja,” akamwagiza katibu wake naye akaondoka hapo mara moja. Robinson akavuta hatua na kuingia kwenye kiti chake maalumu kinachotembea kwenye reli na kumpeleka popote ndani ya kasri lake hilo, akaondoka zake na kuwaacha wasaidizi wake wakibaki kutazamana bila kujua la kufanya.
Mpango dhalimu wa Robinson Quebec ulionekana kugonga ukuta kwa mara ya pili, mara ya kwanza ni pale alipotaka kupenyeza mbinu chafu kwa serikali makini ya Tanzania lakini kitengo maalumu cha kijasusi kilifanikiwa kuwaondoa watu wake Tracy Tasha na George McField. Na mara hii ni katika ukanda huohuo anakutana na kikwazo kingine katika mpango uleule aliouanza tangu miaka kumi iliyopita.
‘Kuna shida!’ aliwaza mwenyewe akiwa kajifungia ndani kwake. Mara simu yake ikaita alipotazama namba hizo moja kwa moja akajua inatoka kwa Don Angelus, akaiweka sikioni na kusikiliza huku akiwa ameikunja sura yake kwa hasira.
“Huyu ni Kamanda Amata, kwenye rekodi yetu ni Yule aliyemuua Tracy Tasha, ni Mtanzania kitengo cha siri cha usalama wa Taifa,” aliyekuwa upande wa pili akahema.
“Hebu, nataka taarifa kamili za kiumbe huyo, na natuma watu sasa waje kummaliza hapo hapo, hawezi kutufanya sisi wapumbavu kiasi hicho, tusumbuliwe na mtu mmoja!” aliongea kwa jazba huku akifuta jasho uso wake na ile simu ikakatika.
‘Huyu kijana anaonekana mahiri sana katika kazi yake, kama alimuua Tracy, George na sasa Zebel, mh! Ananipanda kichwani lazima hatua za haraka zichukuliwe,’ akajisemea kisha kwa kughafirika akapiga meza kwa ngumi nzito.
DURBAN – AFRIKA YA KUSINI
LERETI KHUMALO aliingia kwenye jumba lake saa tatu asubuhi mara tu baada ya kuruhusiwa kutoka kliniki, daktari nwake alichukua hatua hiyo mara baada ya kuona hali ya mtu huyo imeimarika lakini alimtaka kupata mapumziko zaidi, asifanye kazi walau wiki mbili. Wazo hilo kwa Lereti lilikuwa jema sana, alikubaliana nalo na akaamua kujipanga kwa safari hiyo ya dharula, mawazoni mwake aliona nchi bora kwake kwenda kupumzika ni Tanzania akiwa na lengo sasa akamtafute Amata mguu kwa mguu, aliwapa taarifa vijana wake nao walikubaliana naye na alikwishachagua vijana watatu wa kufuatana naye katika safari hiyo.
Alipoingia nyumbani kwake moja kwa moja alikwenda katika ofisi yake ambayo ndani yake kuna simu inayohifadhi ujumbe wa kila simu iliyopigwa, alipoufungua mlango akapigwa na butwaa kuona koti la suti likwa limetundikwa kwenye kiti, akasogelea na kuliangalia bila kushika, alipotupa jicho katika meza yake yenye kompyuta akakutana na kijikaratasi chenye ujumbe; akakinyakua na kukisoma.
‘…usihofu ni mimi nilikuja, nimechukua kabrasha zako kwa kazi maalum nitakurudishia pindi tu kazi yangu ikitengemaa. Nakuomba kama utatoka usiliache koti langu kwani nimelisahau. Kamanda Amata.’
Ule ujumbe ulikatika hapo. Hakukuwa na namba ya simu wala nini, Lereti akapigwa na mshangao, sura yake ikabadilika kutoka katika mshangao na kuanza kutoa machozi ya furaha. Moyoni mwake alijikuta amani na imani vijijenga pamoja. Lakini alihuzunika kuona Kamanda Amata hakumwachia mawasiliano yoyote.
Akachukua lile koti na kuvaa kisha mikono yake akaifumbata kifuani huku tabasamu likichanua moyoni na usoni.
Akatoka na kwenda chumbani kwake, akajibwaga kitandani na kukumbatia mto wa kulalia huku maneno ya mapenzi yakibwabwajika kinywani mwake akajisahau kama anaongea na mto. Nusu saa baadae akatoka na kuifuata simu yake. Akawasiliana na shirika la ndege la Afrika ya Kusini kuona kama kuna ndege itakayomwondoa katika nchi hiyo kwa muda mfupi ili akapate mapumziko.
Akapewa jibu la kuwa ndege ipo siku hiyo hiyo usiku wa saa tatu; aliporidhika akatafuta na hoteli ya kufikia jijini Dar es salaam, ijapokuwa moyoni angependa sana kuonana na Amata lakini ilibidi atii maelekezo ya daktari wake. Siku hiyo aliitumia kupumzika kidogo na kujiandaa kwa safari.
JOHANESBURG – AFRIKA YA KUSINI
KENGELE YA SIMU YAKE ilimwamsha katika usingizi mzito usiokuwa na ndoto. Kamanda Amata akauvuta mkono wake na kuitazama saa iliyokuwa mkononi, saa ya kidigitali yenye kufanya kazi nyingi usizoeza kufikiri; akaitazama na kutabasamu, ilikuwa saa tatu na dakika hamsini asubuhi, akajua Lereti keshatoka hospitali na ameupata ujumbe wake, kwani ndani ya koti lile aliweka GPS button ili likihamishwa saa yake ingempigia kengele na kumjuza limeelekea upande upi, alifanya hivyo makusudi ili kama Lereti akiufuata ule ujumbe kuwa ahakikishe haliachi basi angejua kila alipo mwanamke huyo.
Siku hiyo Kamanda alilala ndani ya gari yake kwani aliona ndiyo sehemu salama kuliko zote, akajinyanyua na kuketi sawia kitini, akashuka na kujinyoosha, kisha akachukua maji na kujiswafi japo usoni maana gari yake aliiegesha porini nje ya mji wa Johanesburg, alipoona yuko sawa aliingia barabarani na kuondoka eneo lile kuelekea mjini.
HOTELI YA MICHELANGELO
DON ANGELO alikuwa tayari kwa safari, aliwaita wasaidizi wake wa karibu.
“Naondoka naenda Canada tuna kikao cha dharula na kikao chicho kimetokana na tatizo hili hapa kwetu, naomba huyo anyejiita Kamanda Amata muhakikishe mnammaliza leo hii, lakini mtafuteni kwa siri sana,” akawapa maagizo.
“Sawa boss, tumeweka ulinzi hotelini kwake hawezi kutuponyoka, pia tumeimarisha uwanja wa ndege, hivyo hana njia ya kututoroka, tutakupa taarifa,” mmoja wasaidizi akajibu.
“Ok, sawa lakini muwe waangalifu huyo jamaa ni mkorofi sana.” Akawajibu kisha akamtazama kijana mwingine mwenye misuli minene aliyesimama pembeni bila kuongea.
“Jefferson, utakuwa mkuu wa idara ya usalama mpaka nitakaporudi, asanteni,” akatoa maagizo na kuondoka zake huku akifuatana na vijana wengine watatu ambao daima haacahani nao, walikuwa walinzi wake wa karibu.
§§§§
Kamanda Amata akashusha darubini yake ndogo iliyomuwezesha kuona wakati Don Angelo akitoka ndani ya hoteli ile na kufuatana na vijana wake, akaingia katika Mercides Benz new model na nyuma yake akafuatiwa na vijana wale latika gari nyingine, wakaondoka.
‘Unakimbia sio?’ kamanda alimuuliza mawazoni kisha akawasha gari na kuunga msafara uliokwenda kuishia Uwanja wa Ndege. Walipoteremka na yeye akateremka na kuendelea kuwatazama, alikuwa na nafasi kubwa na nzuri ya kufanya lolote lakini aliacha kwanza aone…
DON ANGELO na vijana wake wawili waliingia katika jengo la uwanja huo na kupotelea ndani, Kamanda Amata kwa mwendo wa hadhari ili asionekane na wale wengine alitembea taratibu kuelekea kulekule ndani. Kwa mbali alimwona Don akifanya uhakiki wa tiketi zake, jicho la Kamanda likatua kwa mwanadada aliyekuwa akiifanya kazi ile, ‘Bingo!’ akajisemea kisha akasubiri Don na vijana wake waondoke katika eneo lile ili naye akafanye yake.
USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi