MKONO WA JASUSI (22)

Zephiline F Ezekiel

SEHEMU YA ISHIRINI NA MBILI
ILIPOISHIA...
“Tungemmaliza lakini sijajua anatuzidi vipi akili, kila tukipanga hili, yeye yupo sekunde kadhaa mbele,” Robinson akaeleza. Kikao hicho cha dharula kikaendelea kwa dakika kadhaa na kumalizika kisha kila mtu kurudi katika shughuli zake.

JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈

ENDELEA...
KAMANDA AMATA aliegesha gari yake nje ya jengo kubwa la ofisi za shirika moja la simu, katikati ya jiji la Ontario. Mbele yake alikuwa akiitazama gari iliyombeba Lereti na watu wake ambao waliingia Ontario kwa tofauti ya saa tatu tu na Amata. ‘Ni yeye!’ alijiwazia alipomwona Lereti akiingia ndani ya gari hiyo huku walinzi wake wakimlinda kama kawaida. Walipoondoka naye akawafuatia nyuma nyuma bila wao kujua mpaka pembezoni kidogo mwa jiji hilo ambapo kumesheheni mahoteli makubwa ya kifahari.

Ontario Paradise, ilikuwa hoteli ya kisasa nje kidogo ya jiji hilo, Lereti alichagua eneo hilo kuweka makazi yake ya siku hizo chache huku mwanasheria na katibu wake nao wakiwa pamoja naye. Moja kwa moja aliongozwa chumbani kwake ambako pamoja na kila kilichomo alikabidhiwa bahasha moja kubwa na mwanadada mhudumu wa hoteli. Alipoisoma ilikuwa ni kadi maalumu ya mwaliko wa mkutano huo way eye na wadau wake ambao ungetukia saa nne tu baada ya hapo. Aliitazama saa yake, ilikuwa saa sita za mchana kwa saa za Canada. Akaamua kuingia maliwatoni ili kujiswafi kisha kupumzika kidogo.

Ni wakati huo ambao alikuwa akioga na kujifungia mlango wa bafu hilo la ana yake lililojaa starehe za kila aina ndipo Kamanda Amata alipofungua taratibu mlango wa chumba hicho kwa kutumia kadi yake maalumu kwa kufungua vitasa kama hivyo.

Alipojua Lereti kuwa anaoga, hakuwa na haja ya kunshtua au kumsubiri, alitembeza macho kwa haraka na kuiona ile bahasa, akainyakua na kuifuangua ndani haraka, akasoma na kuupata ujumbe hasa alioukusudia. Akatoka katika chumba hicho kabla ya Lereti kutoka bafuni mle.

Ndani ya gari lake aliinua simu na kupiga namba Fulani.

“Yeah ni leo saa 10:30 jioni katika jengo la Quebec High Tower namba 749,” akaongea katika simu ile.

“Ok, maelekezo yanakuja dakika tatu zijazo,” ile sauti ikajibu, naye akatulia garini.

Kama alivyoahidiwa, dakika tatu ile simu ikaita akainyakuwa na kuiweka sikioni.

“Sikiliza kwa makini Kamanda, utatoka hapo ulipo na kuifuata barabara ya Hamingway, moja kwa moja kama unaelekea uwanja wa ndege lakini katika ile njia panda kubwa kunja kushoto, mbele yako mita kama 250 hivi egesha gari kulia, usubiri mtu atakayekuletea ujumbe, haongei na wala wewe usiongee,” ile sauti ikamaliza na Amata akaondo agari kufuata maelekezo kama alivyoambiwa.

Akiwa kaegesha eneo lile aliloelekezwa, gari nyingine kubwa aina ya GMC ikasimama mbele yake, kulikuwa na vijawa wawili walioonekana wapo kisharishari, kijana mmoja akateremka akiwa kavalia kaptula ya jeans, shingoni mwake mikufu ya dhahabu ikimning’inia mkononi mwake alikuwa na kitu kama koba gumu lenye urefua kadiri ya mita moja hivi. Akasogelea gari ya Amata na kumkabidhi bila kuongea chochote, Amata akaingiza lile koba ndani katika siti ya pili naye akaketi nyuma ya usukani. Lakini kabla ya kuondoka akalifungua ndani yake na kuona kilichomo.

“Shiiiiit” akajikuta akiongea peke yake.

Bunduki kubwa la kudungulia, lenye uwezo wa kudungua umbali usiopungua mita 900 lilikuwa limelala ndani yake vipande vipande. Pembeni yake kulikuwa na darubini ya jicho moja na ile ya macho mawili, rimoti ya kuliongoza dude hilo kama hutaki kuwapo eneo la tukio, seti moja ya vifaa vya kusikilizia. Akavichukua na kuvipachika sikioni muda huohuo kuona kama kuna lolote.

“…Saa kumi na dakika ishirini, katika ghorofa kubwa ya Stateway, chumba namba 740 ndipo utakapofanya mapenzi na msichana huyo, mara tu utakapokamilisha kazi sufanya haraka kuteremka utapata maelekezo yote kutoka kwenye hikihiki kifaa na watu wa kukuondosha watakuwa tayari eneo hilo…”

Akawasha gari na kuondoka zake. Katikati ya mji wa Ontario kulikuwa na mgahawa mhubwa wa McDonald akaingia japo kupata chochote akisubiri muda kuwadia.

§§§§§

ONTARIO - Saa 9:45

LERETI aliondoka kwa gari aliyoikodisha yeye na watu wake kuelekea eneo la tukio. Aliketi kwa utulivu katika kiti cha nyuma yeye na katibu wake huku kiti cha mbele akiwapo mwanasheria wake, gari ya pili nyuma kulikuwa na vijana wake makini wakiangalia usalama wa msafara huo.

Moyoni mwake alikuwa akiwaza sana juu ya tukio hilo ambalo linategemewa kutokea dakika chache zijazo, alipatwa na furaha sana moyoni.

§§§§§

Majengo makubwa na marefu mawili yalimkaribisha Kamanda Amata eneo hilo, mojawapo la upande wa kulia lilikuwa na maandishi makubwa juu yake ‘QUEBEC HIGH TOWER’ na lile la kushoto liliandikwa ‘STATEWAY’ na katikati yake barabara kubwa ilikuwa imeyatenganisha, kwa muonekano hayakuwa na uhusiano kabisa . Amata akaegehsa gari yake na kuteremka na ule mkoba. Moja kwa moja akaingia mlango mkubwa na kutumia lifti akapanda mpaka ghorofa ya saba. Hakukuwa na maofisi mengi lakini mahala Fulani penye mlango mkubwa wa kioo palibeba kibao kidogo namba 740, akauendea na kuusukuma ulikuwa wazi. Kamanda Amata alikuwa ndani ya mavazi ya kazi, suruali ya jeans lakini iliyoweza kuvutika, fulana na jacketi lililobeba silaha mbalimbali na mgongoni mwake alikuwa na kijibegi kidogo, kofia ya mzula ilikifunika kichwa chake, gloves ziliificha mikono yake na viatu vyenye soli yenye vyuma vikali nyuma na mbele vilitulia miguuni mwake.

Akatazama huku na kule hakuna mtu, alikuwa peke yake, akaanza shughuli ya kuliunganisha dude hilo kubwa, baada ya dakika sita tayari lilitokea bunduki kubwa lenye bomba refu na lililoonekana kuwa na nguvu ya ajabu, lilisimama kwa miguu yake miwili na kitako chake kujikita chini upande wa nyuma. Kiboksi chenye risasi mbili kubwa kilikuwa mkononi mwake.

“…Unatakiwa kumuua Robinson bila kukosea, mara tu baada ya kumuua uondoke eneo hilo na gari ya kukuchukua itafika katika mlango ulioingilia nukta hiyohiyo…. On your mark,…” sauti ikasikika katika kile kisikilizio, Kamanda Amata akalala sakafuni na kulikamata lile bunduki kwa ustadi wa hali ya juu. ‘Sijazoea kuua kwa mtindo huu, ni nimezoea kupiga mkono kwa mkono, kusimama na windo langu mita zisizozidi kumi…’ aliwaza, mara ghafla sauti ikasikika katika ile mashine sikioni mwake.

“…Katika jopo hilo lililoketi ni Yule mwenye suti nyeusi na miwani ya macho, aliyekamata makabrasha kadhaa mkononi mwake…”

Kamanda Amata alikuwa bado hajapachika jicho katika lensi ya bunduki lile akafanya hivyo na kumwona bwana huyo kwa uzuri kabisa.

§§§§§

ONTARIO – Saa 10:30 jioni

LERETI aliketi katika chumba cha mkutano na jopo la watu kadhaa akiwemo Don Angelo, yeye na mwanasheria wake walikuwa wameketi pamoja na upande ule Robinson na mwanasheria wake pia walikuwamo mashahidi kadhaa katika kikao hicho, kila mmoja upande wa Robinson alionekana kuwa na wasiwasi na maamuzi ambayo bwana huyo amechukua juu ya kampuni hiyo. Ukimya ulikuwa ni moja ya sehemu ya mkutano huo kwa wakati huo. Baada ya mazungumzo mafupi kati ya makundi hayo mawili, yale makabrasha yakatandazwa mezani na watu wa pande hizo wakayasoma kwa umakini, baada ya hapo wanasheria wa pande zote mbili wakasomeana tena kwa sauti na kupitia kipengele baada ya kipengele.

Lereti alikuwa amsikilizaji tu, alipojiridhisha na hati ile akaridhia kuitia saini mbele ya mashahidi, karatasi zikawekwa mbele ya Lereti lakini mwanasheria wake akazuia boss wake kusaini akitaka Robinson asaini kwanza, kukatokea ubishano kati yao.

§§§§§

Saa 10:55

“Natakiwa kumlipua wakati gani?” kamanda akauliza.

“…Nataka umlipue sasa, usichelewe kwani tunaweza kugunduliwa kisha ikawa shida…” ile sauti ikamjibu kupitia katika vile visikilizio, Kamanda aliongea na mtu asiyemjua wala kumwona.

“Subiri kidogo…”

“…no! shoot now!” ile sauti ikang’aka.

“Subiri, time bado bwana,” Amata naye akaonesha ukali.

“…Amata, shoot now this is an order…” (Amata, lipua sasa hii ni amri) .

Hata hivyo Amata alitulia tulia akiendele kuangalia mtu mmoja baada ya mwingine ndani ya chumba kile.

“Yeeeessss! Do that,” (Ndiyo fanya hivyo) Amata alisema kwa sauti ndogo alipoona lile kabrasha likirudi kwa Robinson naye kuchomoa karamu kwenye kijaruba chake na kusaini ule mkataba.

“Go, Lereti go!” (haya Lereti haya) . Lereti akaweka saini katika hati ile na jicho la Robinson lilikuwa baya waziwazi kwake, aliposaini na wale wanasheria wakasaini baada ya mashahidi wote kusaini ile hati ya kuvunja mkataba wa ubia kati ya zile kampuni mbili.

Walipomaliza tu mlango ukafunguliwa na warembo wawili wakaingia na kitoroli kilichojaa vinywaji na kuanza kusambaza kwa kila mmoja. Chupa moja pekee alimiminiwa Lereti na wale watu wake na ikarudishwa.

“Why?” (kwa nini?) Kamanda akajiuliza.

“…umepoteza hesabu zote Amata, hutompata tena Robinson, na wewe kutoka ndani ya Ontario ni ndoto, wamekuona wanakufuata, kwaheri…”

Ile sauti ikamwambia Amata na kisha kijisauti cha mawasiliano kukatika kikasikika kikibipu mara tano na kuzimika.

“Shiiiit, Im out,” akajisemea kwa sauti ndogo, na kurudisha jicho kwenye lensi ya lile bunduki, moja kwa moja akapepesa jicho kumtafuta Robinson asimwone.

“Come on! Where are you bastard?” ( uko wapi mwanaharamu?) alijiuliza mwenyewe kwa sauti na mara akamwona tena Robinson akiagana na wageni wake, akaweka shabaha yake vyema. Na wakati huohuo alimshuhudia Lereti akianguka chini sakafuni. Kamanda Amata akajikuta katikati hajui afanye nini, kitendo cha Lereti kuanguka kilimpa kigugumizi cha mikono, aliposhtuka alikutana uso kwa uso na Robinson aliyekuwa akiangalia kule aliko Amata tena kwa darubini.

“Limeniona, goodbye,” akajisemea na kupachika dole la shahada kwenye kifyatulio kisha akavuta bila huruma.

“Go baby go..” Amata alifyatua na lile bunduki bila kutoa mlio mkali likaachia risasi moja nzito iliyotawanya kifua cha Robinson na kumtupa ukutani kwa nguvu na kuacha doa kubwa jekundu katika ukuta ule.

“Hapo hapo ulipo!” sauti ikatoka nyuma yake, Kamanda Amata hakujiuliza, aligeuka haraka na tayari bastola zake mbili zikiwa mikononi, kitendo cha sekunde tu alifyatua bastola zake na kuwapata vijana wawili waliokuwa nyuma yake, wakatupwa kando wakiwa wanaokoteza uhai wa mwisho. Kamanda Amata akasimama na kutazama huku na kule, tayari mtafaruku ulianza huko chini, na ndani ya chumba kile alichouawa Robinson kulikuwa ni heka heka.

Akaondoka eneo lile na kuruka kwenye kikorido cha chini yake,

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA

Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi

Chapisha Maoni