
Mtunzi: Richard Mwambe
SEHEMU YA ISHIRINI NA TATU
ILIPOISHIA...
ILIPOISHIA...
Kamanda Amata akasimama na kutazama huku na kule, tayari mtafaruku ulianza huko chini, na ndani ya chumba kile alichouawa Robinson kulikuwa ni heka heka.
Akaondoka eneo lile na kuruka kwenye kikorido cha chini yake,
JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media?
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI
👉GUSA HAPA KU-INSTALL👈
ENDELEA...
akavua mkanda wake wa kiuno na kuupachika kwenye waya wa umeme akakamata huku na huku akazungusha miisho yake katika viganja vya mikono kisha akajiachia na kupita hewani kuelekea jingo lile walilokuwamo akina Lereti.
Nyuma yake alisikia milio ya risasi ikimfuatia. Aliteremka kwa kasi na alipofika umbali wa mita mbili kutoka katika lile dirisha kubwa la kioo ambalo ndani yake kulikua na kile kikao, akajiachia na miguu yake ikatangulia kwenye kile kioo na kukitawanya vipande vipande kisha yeye akatua ndani yake na kuwatawanya watu walio karibu yake kwa mateke mawili makali.
Alipotua sakafuni akakutana uso kwa uso na Don Angelo.
“Zamu yako inakuja!” akamwambia kisha haraka akapiga risasi hewani na kumnyayua Lereti kutoka pale chini akiwa hajitambui. Akambeba kwa kumkumbati na kutoka naye pale dirishani kuelekea chini. Mkono mmoja akimshika Lereti kwa nguvu na ule mwingine akafytaua parachute lilikouwa ndani ya begi lake na kuteremka taratibu.
Alipofika chini tu, gari moja aina ya GMC ilifunga breki ghafla.
“Twendeeeee!!!!” Scoba akiwa nyuma ya usukani alimwita Amata naye bila kuchelewa, alimpakia Lereti kisha akajipakia nay eye na kuondoka kwa kasi eneo lile huku wakifuatiwa na ving’ora vya polisi. Scuba aliendesha gari ile kwa ustadi wa hali ya juu na kuwachenga polisi waliokuwwa na gari za kisasa. Baada ya kupita mitaa kadhaa, Scoba alitoka barabara ni na kuegesha pembeni. Kisha akabofya vidubwasha Fulani na sakafu ya chini ya gari ile ikafunguka. Chini barabarani kulikua na funiko kubwa la bomba la maji machafu, mara likafunuliwa, na Chiba akaonekana ndani yake, Amata akamshusha Lereti na kisha akaingia yeye mwisho akamalizia Scoba, wakajifungia na kupotelea ndani ya bomba hilo ambalo halikuwa na maji hata kidogo.
Huko nje, polisi walipoliona lile gari limeegeshwa wakalikaribia na gari zao lakini wakasimama umbali kidogo na kuteremka wakiwa na bastola zao mikononi, wakitoa maonyo ya walio ndani kujisalimisha. Kabla amri hiyo haijatiiwa mlipuko mkubwa ulitokea na ile gari ikawaka moto na kuzua kizaazaa.
§§§§§
“Nilikutafuta sana Amata, nikashangaa pale nilipoandika mawasiliano yako kwenye kitabu changu, karatasi imechanwa na kuondolewa,” Lereti alilalamika akiwa chini ya pua ya Amata kwenye kitanda kikubwa cha sita kwa sita huku moto ukiendelea kuwaka kwenye chemba maalumu na kufanya kajoto ka wastani ili kupunguza baridi kali iliyolikumba jiji hilo.
“Pole sana, nilikiondoa mimi mwenyewe pindi tu ulipokwenda kuoga na kukiacha ndani ya mkoba wako,” Amata akajibu.
“Tabia mbaya, mi nateseka mpaka nataka kufa, nakutafuta nashindwa kukupata,”
“Sasa mbona nimekuja kukusaidia? Tena kutoka Afrika Kusini mpaka Canada na ushindi umepata, mgodi wa baba yako umerudi mikononi mwako, hakuna utapeli tena, nilisubiri tu Yule bwege asaini na wewe usaini na wanasheria na mashahidi kisha nimmalize kama ilivyokuwa,” kamanda akamweleza.
“Ha! Ni wewe uliyemuua?” Lereti akauliza na kujiinua huku akimsogeza Amata pembeni.
“Ni nani mwingine mwenye mkono wa nguvu kama mimi? Huu ni mkono wa jasusi ukikuandikia kifo utakufa tu,” Amata akajibu.
“Oh, asante, nikupe nini mpenzi zaidi ya hiki? Umenilipizia kisasi mara mbili, umenirudishia kitu kikubwa sana moyoni mwangu, amani, hata Mzee Khumalo huko aliko anafurahi hili,” akamtazama Amata usoni na kuvuta karibu akambusu kinywani kwa sekunde kadhaa.
“Kamanda najua hauna motto, nataka kukupa motto,” Lereti akaongea huku chozi likimtoka.
“Utanipa wangapi? Maana kazi hii bado haijaisha…”
“What?”
§§§§§
Msafara wa maazishi uliojumuisha gari kama hamsini hivi za kifahari ulikuwa ukienda taratibu katika makaburi ya watu wazito yaliyojengwa nje ya jiji la Ontario. Ilikuwa ni safari ya mwisho ya kibopa Robinson Quebec.
Vyombo vya habari zikiwamo redio, magazeti na televisheni vilikuwa vikirusha habari ya tajiri huyo aliyeuawa kwa kudunguliwa, vikisifu ulinzi aliokuwa nao na kuponda jinsi alivyokufa kizembe, lakini mpaka nukta hiyo hata wao walikuwa hawajui ni nani aliyetekeleza mauaji hayo walibaki kudhani tu, labda … labda.
Kamanda Amata alishusha gazeti alilokuwa anasoma na kuyaruhusu macho yake kumwona Don Angelo aliyekuwa kati ya vijana watatu sambamba ah ii wakivuta hatua fupifupi kuingia katika uwanja wa makaburi yale.
Idadi ya watu haikuwa kubwa kama misiba ya kwetu, takribani watu 100 walikuwapo na kila mmoja akiwa kwenye nguo nyeusi na kuketi kitini ibada ikiendelea.
“Tangu lini unatembelea fimbo?” Lereti alimuuliza Amata.
“Nimezeeka sasa, ah ii fimbo inanisaidia sana katika kutembea,” akamjibu huku akimwangalia usoni, kutoka pale walipoketi karibu kabisa na mlango wa kuingia katika yale makaburi, hakuna aliyewagundua kama kijana huyo ndiye aliyesababisha mauti ya huyo anayezikwa kwa jinsi alivyojibadili sura yake. Walipoona sasa watu wanatawanyika na maziko yamekamilika wao wa kwanza kutoka na kuingia kwenye gari yao yenye rangi kama za wale yaani nyeusi kisha wakatazama vizuri Don Angelo ataingia katika gari ipi.
Scoba akageuza gari na kuendesha kwa mwendo mdogo mpaka usawa wa dirisha la gari aliyomo Don Angelo, Kamanda Amata akashusha kioo taratibu na kumtazama Don Angelo, wakakutana macho, akiinua fimbo yake na kuiweka dirishani ncha yake ikimtazama Don.
“Na sasa ni zamu yako kama nilivyokuahidi,” akamwambia kwa sauti ambayo ilimfikia bila kikwazo.
Don Angelo akakodoa macho, akahisi koo limemkauka ghafla, akameza fundo kubwa la mate huku macho yamemtoka kama anameza jiwe, kufumba na kufumbua kitu kama msumari kikatua katika paji la uso na kufanya jeraha dogo lililokuwa likichurizika damu. Don akabaki kakodoa macho uhai ukimwondoka bila hiyana.
Scoba bakaondoa gari bila mtu yeyote kujua nini kimetokea.
“Shiit, hiki ni nini Amata?”
“Fimbo ya kutembelea,” akajibu.
‘Asante Bill Van Getgand kwa fimbo hii,’ akawaza na kutikisa kichwa huku kioo kikipanda juu taratibu.
MWISHO
Share CnZ Media App kwa Wapenzi wa Kusoma Simulizi Ili Tuwe Wasomaji Wengi