NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI (1)
Jina: NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI Mtunzi: Nyemo Chilongani SEHEMU YA KWANZA Ukimya ulitawala ndani ya Jiji la Dar es Salaam , yale magari yaliyokuwa yakipita kwa kasi katika barabara nyingi jiji humu yalikata kabisa. Watu wengi waliokuwa wakienda huku na kule hawakuwa wakionekana kama nyakati za mchana. Kila kitu kilibadilika usiku huo, katika mitaa mingi ya Kariakoo hakukuwa na watu kabisa, ilikuwa ni vigumu kuamini kama nyakati za mchana kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakipita huku na kule. Katika muda huo, nilikuwa katika Mtaa wa Kongo . Hapo, ndipo kulipokuwa na maisha yangu, niliyaendesha humo, si kama mfanyabiashara bali nilifanya kazi hapo katika kusafisha barabara kila siku usiku. Kwa jina ninaitwa Edward Francis . Nimeamua kukusimulia maisha yangu yalivyokuwa, najua kuna watu wanamuona mtu fulani amefanikiwa halafu wakahisi kabisa alitoka kwenye familia ya kitajiri, leo watu wanavyoniona nina nyumba kubwa, magari ya kifahari na hata biashara nyingi wanadhani kwamba nilizaliwa kwenye fami…