NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI (6)
Jina: NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI Mtunzi: Nyemo Chilongani SEHEMU YA SITA ILIPOISHIA... Nilimwambia kuhusu kile kilichotokea usiku wa siku ile, watu wale walitumwa kwa sababu walikosa walichokuwa wakikifuata kwa baba yake ila sikumwambia ni kitu gani, nikaongezea kuwa kulikuwa na walinzi wenzangu ambao waliuawa na bila shaka watu wale ndiyo waliokuwa wamewaua kwa sababu niliwasikia wakiongea kuhusu hilo. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Ilikuwa ni stori fupi lakini iliyomsisimua mno. Akanisogelea na kunibusu shavuni, yaani hilo busu likanipa nguvu ya ajabu kupita kawaida. Kuanzia siku hiyo akaanza kuja hospitalini hapo kuniona akiwa na ndugu zake wengine ambao walinionyeshea thamani kwa kuwa niliyaokoa maisha ya baba yao. Kichwa changu kilikuwa kikifikiria kuhusu ile almasi iliyokuwa chumbani kwangu, nilitamani sana niiuze, nipate mamilioni na kuendelea na maisha yangu. Nilikaa hospitalini hapo kwa wiki moja…