NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI (7)

Zephiline F Ezekiel
NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI (7)
Jina: NYUMBA ILIYOJAA DHAMBI Mtunzi: Nyemo Chilongani SEHEMU YA SABA ILIPOISHIA... Mzee yule hakutaka kujibu kitu, bado alikuwa akinishangaa, kwake nilionekana kuwa kama kituko fulani hivi. Akatuambia kwamba alikuwa akiiuza kwa shilingi milioni themanini kwa kuwa alitaka kuondoka hapo na kwenda kuishi Mbagala , maisha ya mjini eti yalimchosha. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... “Mbona nyingi sana?” nilimuuliza mzee huyo. “Si unaona Juma! Nilikwambia umeniletea mhuni unabisha! Sasa milioni themanini ina wingi gani?” aliuliza baba mwenye nyumba. Maneno yake yalinikera sana, nilitamani ninunue nyumba yake na nimnunue mpaka yeye mwenyewe. Ila pamoja na kuumia hivyo, sikutaka kuonyesha hasira zozote zile zaidi ya tabasamu pana. “Basi sawa! Nitakulipa hizo milioni themanini,” nilimwambia ili kuepusha maneno. Nilichomwambia ni kutaka kuona hati ya nyumba hiyo. Hilo halikuwa tatizo, akamuita mtoto wake wa kike aliyei…