CHUZI NDIO HILO, HAKUNA KUONJA (12)
Jina: CHUZI NDIO HILO, HAKUNA KUONJA Mtunzi: Global Publisher SEHEMU YA KUMI NA MBILI ILIPOISHIA... Ndani ya saa moja, Maua alimkaribisha baba Shua chumbani… “Njoo upaone mahali anapolala ubavu wako,” alisema Maua. JE UNAISOMA SIMULIZI HII NJE YA APP YA CnZ Media ? IPAKUE ILI KUPATA MWENDELEZO KWA WAKATI 👉 GUSA HAPA KU-INSTALL 👈 ENDELEA... Baba Shua akiwa ameshakunywa wine glasi mbili, hivyo amechangamka kidogo, alimfuata Maua kwa nyuma hadi chumbani… “Da! Chumba kama cha waziri wa fedha,” alitania baba Shua, Maua akacheka. Ni kweli kilikuwa chumba kizuri, kilichosheheni kila kinachohitajika kwa ajili ya chumba. Kitanda cha kisasa kilichozibwa na godoro kubwa, kabati kubwa la nguo, redio yenye kutumia CD sita na kiyoyozi cha ndani kwa ndani, vyote hivyo vilikifanya chumba hicho kuvutia zaidi. Baba Shua alifikia kujitupa na kunesanesa kidogo huku akimsifia Maua kwa kujitahidi kutengeneza maisha yake vizuri… “Da! Umejitahidi sana baby wangu…hongera sana…” “Asante sweet, lakini siku zile tukiwa bado wote…